Kwa namna hii EMAC wanaua elimu ya nchi hii

Kwa namna hii EMAC wanaua elimu ya nchi hii

Herbert Nkuluzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2015
Posts
2,866
Reaction score
3,065
Ndugu zangu kuna jambo linashanganza sana katika elimu. Tutasingizia walimu lakini matatizo ya elimu yameanzia juu kabisa. Kwa kawaida kitabu kinapoandikwa hukaguliwa kabla ya kwenda katika matumizi shuleni au vyuoni sasa inakuwaje mwandishi anakosea na hata wathibitishaji wa vitabu kutumika (EMAC) nao washindwe kuona makosa hayo?

Nilikuwa napitia kitabu cha Kiswahili darasa la sita maana mama yangu ni Mwalimu cha ajabu nimekutana na haya katika kitabu cha Kiswahili darasa la 5
[emoji116]
Kiswahili 5, Ben&Company Ltd, 2013, Dar es Salaam, kitabu cha mwanafunzi
uk 177

ZOEZI
F:Majadiliano
Taja magonjwa yenye dalili zifuatazo na jinsi ya kukabiliana nayo.

1 Ugonjwa unaoenezwa na mbu. Dalili zake ni kupata homa kali na joto la mwili kuongezeka

2 Ugonjwa unaotokana na kula vyakula vichafu au maji yasiyo salama

[emoji115]
NI KITABU CHA MWANAFUNZI NA MAJIBU YA MASWALI HAYO ETI NI HAYA HAPA
[emoji116]
Majibu
Kiongozi cha mwalimu uk 222

Zoezi
F :Majadiliano

1 Majadiliano
2 Malaria


WIZARA YA ELIMU HAWAKUYAONA MAKOSA HAYA AU ILIKUWA NI BIASHARA TU KAMA BIASHARA NYINGINE ZENYE UJANJAUJANJA NDANI YAKE?

Tanzani bora itajengwa na watu bora, makosa haya yanaondoa ubora wa elimu wanayoipata wanafunzi shuleni na hivyo kuwa na taifa la watu wasio bora kitaaluma.
 
Samahani nakumbuka EMAC walifungiwa na kutumbuliwa kama sio 2012 basi 2013 so hawapo tena
 
Hizo Ni Typing Error Ndogo Ambazo wanaofanya Uhakiki wanaweza Kui skip.

Ndo Maana wanafundisha walimu waliosoma ..Swala Kama Ilo Mwl Lazima okosoe Kidogo ..

Ndo Maana Kila Mtu Sio mwalimu
 
Honest kumbe EMAC ni marehemu, basi sawa ila mbona hata Taasisi ya Elimu nayo imezingua kitabu cha English std 3?
 
Hizo Ni Typing Error Ndogo Ambazo wanaofanya Uhakiki wanaweza Kui skip.

Ndo Maana wanafundisha walimu waliosoma ..Swala Kama Ilo Mwl Lazima okosoe Kidogo ..

Ndo Maana Kila Mtu Sio mwalimu
Km mwalimu nae alikuwa ni mzee wa chabo inakuwaje hapo?
 
Back
Top Bottom