KWA NAIBU WAZIRI WA UTALII

KWA NAIBU WAZIRI WA UTALII

Mouse3

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2013
Posts
1,454
Reaction score
1,301
Kwanza nitoe pole kwa wizara na kwa wadau wa utalii kwa ujumla kwa tukio la ajali lililotokea. MUNGU NIMWEMA ATALETA FARAJA KWA PANDE ZOTE.

Nielekee kwenye hoja.
Mh.Naibu waziri wa utalii ninakero na kero hii nadhani hainisumbui mimi tu ila nahisi hakuna aliyekuwa na wazo la kuiweka wazi. Mimi ni mdau wa utalii na utalii naoufanya nikushawishi watalii waje Tanzania, sioni kosa lolote kufanya hivyo na Mara nyingine watalii hao hunipa masharti ya kuwasindikiza katika mbuga hizo, ombi langu nihili ,naomba tupewe support na wizara na vitengo vyake hususani tuwapo ndani ya hifadhi na watilii au wageni hao,kwani huwa tunalipa viingilio sahihi Kama watanzania na sii vinginevyo,sisi sio wahalifu wakuhisiwa vibaya na kuhojiwahojiwa kila saa uhalali wangu wa kuwa mule hifadhini! Ikimbukwe nimejitolea Kama mzalendo kwa nchi yangu nikazunguka huku na kule kwa gharama zangu pengine hata kuitwa nyani huko ughaibuni na sijali ilimradi tu naipeperusha bendera ya nchi yangu vyema na kuitangaza,ikumbukwe nipatapo wageni niwazi nimetengeneza ajira kwa watanzania wenzangu na kuiletea nchi yangu pato na fedha za kigeni!
Ombi, kuwe na dawati litakaloimarisha au kuunganisha wadau wa utalii wa aina yetu ambao hufanya shughuli za kuitangaza nchi na vivutio vyake nje ya nchi au tuwe na vitambulisho special vitakavyo tutambulisha ili kutuepushia hizi bugudha za kuhojiwa passport na kuhisiwa eti nakwepa kulipa ada ya kuingilia hifadhini hii inakera na kudhalilisha mheshimiwa! Na wageni wanauliza ulikuwa unahojiwa nini na kwakuwa hulka yangu nikukataa uongo inabidi niwaeleze sababu ni nini.kwakweli inakatisha tamaa.
Ningefurahi kuona wageni wanaona uhalisia wa ukarimu na utanashati wa watanzania popote walipo Kama tunavyowaambia nakuwashawishi waje kutalii huku nyumbani.
Nitoe pongezi kwa Balozi na ubalozi wa UK kwa juhudi za kitutia moyo na kushirikiana na sisi huku ughaibuni na matunda yanaonekana ila yakisha fika huko nyumbani yanaanza kuharibwa hata kabla hayajatoka nje ya airport. Mheshimwa this is serious issue wageni wanalalamika! Ongezeni migration officers kwenye tellers za visa! Haiwezekani ndege inatua ina wageni 200 na ushee alafu watu wa kudeal na visa wako wawili! Wageni walitoka ndani after 4 hours tokea walipo tua na wamelalamikia hilo!

Nihayo tu kwa Leo Sina shaka nitaona mwanga wa mabadiliko siku sio nyingi kwa utendaji wa JPM!
 
Back
Top Bottom