Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,673
- 149,860
Nilikuwa napitia Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania sura ya tatu inayohusu Bunge la Jamuhuri ya Muungano.
Katika kuipitia sura hiyo, nimeshangazwa au niseme nimejkuta napata utata baada ya kusoma Ibara ya 71-(1) inayozungumzia mambo yanayoweza kumfanya Mbunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kukoma kuwa Mbunge.
Ibara hiyo ya 71-(1)(a) mpaka (g) inaeleza mambo/sababu zinazoweza kumfabya mbunge akome kuwa Mbunge wa Bunge hilo la Jamuhuru.
Kifungu 71-(1)(e) chenyewe kinasomeka hivi(ikiwa ni moja ya sababu inayoweza kumfanya Mbunge apoteze sifa ya kuwa Mbunge):
71-(1) (e)
Ikiwa Mbunge ataacha kuwa mwanachama wa chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa Mbunge.
Swali:
Mbunge anaevuliwa uanachama anakuwa ameaacha ubunge au ameachishwa?
Kwanini badala ya neno "ataacha" lisingetumika neno "atakoma"?
Je,hapa hakuna utata/loophole?
Au kuna sheria inatamka wazi kabisa kuwa mbunge akivuliwa uanachama kwasababu yoyote ile na ubunge wake anapoteza?
Kama hakuna sheria inayotamka bayana hivyo,je hatuoni kwa kuna tatizo hapa?
Kwakuwa Katiba ndio sheria mama, mbunge alievuliwa uanachama na chama cha siasa akipata Wakili smart na kwa kutumia kifungu hiki cha Katiba,hawezi tetea ubunge wake
Nimeuliza hivi kwasababu tumekuwa tukisikia kuwa mbunge akivuliwa uanachama wa chama cha siasa basi na ubunge wake anaupoteza pia.
Ipo siku isiyo na jina utata huu wa kikatiba unaweza kuja kuibuka kwa mbunge atakaekuwa amevuliwa uanachama na akaamua kwenda katika Mahakama ya Katiba kuomba ufafanuzi wa kipengele hiki cha Katiba.
.