Kwa mtindo huu kijana baraka mfilinge ataukwaa ubunge jimbo la kilolo-2015.

Mar 1, 2012
61
10
Baraka mfilinge ni kijana wa miaka 25 sasa na amemaliza kidato cha sita mwaka 2011 katika shule ya sekondari kigurunyembe ambapo pia alikuwa co-ordinator wa YUNA(YOUTH UNITED NATIONS ASSOCIATION) pale shuleni kigurunyembe, baadaye alitunukiwa cheti cha utambuzi wa mchango wake kwa TAIFA kwa kuwa mhamasishaji wa utalii wa mambo ya ndani. Tangu alipomaliza shule amekuwa akijituma kujenga chama cha chadema jimboni kilolo ambapo mpaka sasa ametembelea kata 14 kati ya 22 na ukitaka kujua kuwa huyu kijana atachukua jimbo hili, kawauliza wananchi wa r.mbuyuni, mahenge, ilula, mlafu, udekwa, ilole, lugalo, mtitu, ng'uruhe, ukumbi, utengule nk. watakwambia mfilinge atakuwa mbunge wetu! jamani naomba kwa mtu yeyote anaejua uwezo wa kijana huyu katika kuukwaa ubunge ajitokeze hapa ili tujue nguvu yake nje ya mipaka ya jimbo kwani kwa uwezo wa kujenga hoja jukwani humuwezi! nawasilisha ili nayeye kama yupo hapa jf atoe comment.
 
Hawezi lolote maana wako kwenye magenge ya nyanya .... singida ni ngome la CCM
 
Mi nadhani apambane kuongeza elimu yake kwanza ubunge baadaye
 
kijana wa miaka 25 sasa na amemaliza kidato cha sita mwaka 2011 katika shule ya sekondari kigurunyembe

Tuseme amemaliza form 6 akiwa 24. Alichelewa wapi?
 
Mi nadhani apambane kuongeza elimu yake kwanza ubunge baadaye

swali langu la kwanza lilikuwa, ina maana kaishia form six? Siyo kwamba hawezi kuongoza,ila lazima tuwajenge watu wawe na kazi zao ili isiwe rahisi kurubuniwa. Ndo maana wakikosa ubunge wanazimia. Siasa kila mtu anaweza kufanya,tafuteni kazi ya kujishikisha ukikosa ubunge ili uwe na uwezo wa kusimama kivyako na siyo kunyanyaswa na chama! Ukiangalia kauli za deo utagundua ni mtu mwenye uwezo wa kusimama na anaweza kuishi hata nje ya siasa ndo maana anasimama kutetea wananchi badala ya chama.
 
wanajamvi shule si sababu ya kumkatisha mpambanaji huyu katika harakati zake kikubwa tumpe support katika harakati zake za kulikomboa jimbo la kilolo hizi ni harakati za kuelekea 2015 na ikija M4C ni kusafisha masalia yanayobaki kama shule ni baadaye kijana endeleza harakati zako mie nakupa go ahed.
 
Mi nadhani apambane kuongeza elimu yake kwanza ubunge baadaye
Mkuu nakuunga mkono huyu Bwana Mfilinge apambane kuongeza elimu aende university, kama hana uwezo wadau wamsaidie huko huko vyuoni atahamasisha Watanzania walioko vyuo ili kuleta ukombozi!!!!!! Elimu kwake ni muhimu kama anataka kuwa kiongozi bora msomi kam kina Mhe Mnyika!!!!

Baraka mfilinge ni kijana wa miaka 25 sasa na amemaliza kidato cha sita mwaka 2011 katika shule ya sekondari kigurunyembe ambapo pia alikuwa co-ordinator wa YUNA(YOUTH UNITED NATIONS ASSOCIATION) pale shuleni kigurunyembe, baadaye alitunukiwa cheti cha utambuzi wa mchango wake kwa TAIFA kwa kuwa mhamasishaji wa utalii wa mambo ya ndani. Tangu alipomaliza shule amekuwa akijituma kujenga chama cha chadema jimboni kilolo ambapo mpaka sasa ametembelea kata 14 kati ya 22 na ukitaka kujua kuwa huyu kijana atachukua jimbo hili, kawauliza wananchi wa r.mbuyuni, mahenge, ilula, mlafu, udekwa, ilole, lugalo, mtitu, ng'uruhe, ukumbi, utengule nk. watakwambia mfilinge atakuwa mbunge wetu! jamani naomba kwa mtu yeyote anaejua uwezo wa kijana huyu katika kuukwaa ubunge ajitokeze hapa ili tujue nguvu yake nje ya mipaka ya jimbo kwani kwa uwezo wa kujenga hoja jukwani humuwezi! nawasilisha ili nayeye kama yupo hapa jf atoe comment.

unamwomba aje wakati kakutuma! cha msingi asome kwanza, siasa ipo tu, kama kweli anaipenda siasa afuate nyayo kama za kina zitto na mnyika walijitahidi wakafika chuo na sasa hawababaiki
 
Back
Top Bottom