Kwa mnaojua mambo ya sheria na katiba tu!

Jumanne Mkota

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
2,917
1,660
:A S 465:Asalaam aleukum wana JF wote.
Naomba watu msinielewe vibaya kuuliza si ujinga kuna mambo mawili ambayo yanachanganya taasisi mbili muhimu hapa nchini!
taasisi ya kwanza ni Bunge kama mhimili wa pili wa dola . na pili ni taasisi ya Urais.
Wadau ninapochangayikiwa ni hapa nisaidieni:-

1. Wananchi hasa wanaokaa mijini wasomi na wasiokuwa wasomi ambao wana access na internet, kusoma magazeti nk wanasema Bunge limepoteza sifa kwa mambo mbalimbali kama vile uasi unaodaiwa kufanywa na mibunge ya CCM dhidi ya Mkuu wa Kaya. Wananchi hawa wanasema Rais avunje Bunge ili tufanye uchaguzi mpya ! Sawa kabisa ! swali langu je ni kweli Rais ana uwezo wa kuvunja Bunge? na yeye ataendelea kuwa Rais au ni kitu gani kitaundwa badala ya Bunge?

2. Wabunge nao wanaishutumu taasisi ya Urais kuwa ni legevu! kigeugeu (vita ya Posho,Sakata la Jairo ) na serikali pia ni legevu kwamba muda wowote wanaweza kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais! (Rejea post moja humu Jamii Forum inayomhusu Bity shelu.) wakipiga kura hii wao watakuwa na nafasi gani baada ya kutokuwa na imani na Rais aliewanyanyua mikono na kusema wao ni safi na kutuomba tumpe watu hao (mibunge ya CCM) ili akafanye nao kazi? Je wabunge kutokuwa na imani na Rais ndio kuwa tutafanya uchaguzi mpya nadi ya 90dayz!

Sasa ni nani zaidi hapo naomba mnielimishe si kwa hasira wala ushabiki wa vyama vyenu vya siasa . nataka kujua tu ili nami nichague pakuunga mkono!:juggle:
 
kwaninavyojua mimi bunge kuvujwa hakuna maana ya kuwavua wabunge ubunge wao.kinachovunjwa ni uongozi wa bunge kwa maana spika katibu na ofisi nzima ya bunge.ila akishavunja bunge nilazima avunje baraza la mawaziri.nb;hatua zote hizi bado haziwezi kuathiri nafasi ya rais kwakua kikatiba rais yuko juu ya katiba.ila ikitokea wabunge wakapiga kura ya kutokumwamini rais rais atakua chini ya katiba na anaweza kujiuzulu.
 
Mkuu,
Umepotoka kidogo kudai kuwa Rais yuko juu ya Katiba na akipigiwa kura anakuwa chini ya Katiba hiyo hiyo! Nakujulisha kuwa hakuna wakati ambao Rais yuko juu ya Katiba, ndio maana aliapa kuilinda na kuitetea!
 
kwaninavyojua mimi bunge kuvujwa hakuna maana ya kuwavua wabunge ubunge wao.kinachovunjwa ni uongozi wa bunge kwa maana spika katibu na ofisi nzima ya bunge.ila akishavunja bunge nilazima avunje baraza la mawaziri.nb;hatua zote hizi bado haziwezi kuathiri nafasi ya rais kwakua kikatiba rais yuko juu ya katiba.ila ikitokea wabunge wakapiga kura ya kutokumwamini rais rais atakua chini ya katiba na anaweza kujiuzulu.
Mkuu kuvunja bunge ni kuvunja serikali. Kunakuwa hakuna bunge kwa maana ya kwamba mchakato wa uchaguzi wa wabunge unaanza upya na siyo kumuondoa spika tu.
Bunge linaweza kumvua Rais Urais baada ya kumshitaki bungeni na kupiga kura ya kutokuwa na imani naye ila haka kamchakato ni kagumu kidogo japo kikatiba kanawezekana.

Hapa ni timing tu. Rais akiwataimu wabunge basi anawamaliza na Wabunge wakimtime Rais wanammaliza
 
=Kimbunga;3293112]
Hapa ni timing tu. Rais akiwataimu wabunge basi anawamaliza na Wabunge wakimtime Rais wanammaliza
OK, suppose wabunge wanaamua kumng'oa rais kwa kuwa amekataa kupitisha ongezeko la posho wanazotaka, hii haikinzani na matakwa ya demokrasia kwa rais aliyepewa ridhaa na mamilioni ya wananchi?
 
Back
Top Bottom