Nsaji Mpoki
JF-Expert Member
- Nov 5, 2007
- 396
- 65
Tunawaomba siku hizi mbili kabla bunge halijaahirishwa pitieni mgao wa bajeti za mikoa na halmashauri za wilaya. Mnaweza kutumia mfano wa vitabu vyenu vya mikoa.
Kimsingi kwa mwaka ujao wa fedha serikali haitaweza kabisa kutoa huduma kwa wananchi hata kwa mwezi mmoja. Tumeongeza ukubwa wa serikali kwa kuanzisha miundo isiyo na tija bila kuangalia uwezo wa mapato. Hivi sasa kwa mfano fedha za uendeshaji wa hospitali za rufaa za mikoa zimeshuka toka tshs mil. 420 kwa mwaka hadi kufikia tsh mil 240 kwa mwaka wakati viwango vya posho za madaktari zimepanda kufuatia ahadi ya PM.
Hali hii ni ya hatari. Inaweza kusababisha manung'uniko zaidi. Tafadhali mawaziri wa fedha, utumishi na Tamisemi watakiwe kutoa maelezo jinsi watakavyookoa hali hii. Kwa namna mfumuko wa bei ulivyo kutoa nusu ya bajeti ya mwaka jana yaani kutoka tsh. Bil 2 kwa mkoa hadi kufikia tsh milioni 800 usitegemee usimamizi wa lolote