GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,212
- Vijana na Mabinti hawawaheshimu tena Wakubwa zao na wanaona wanalingana.
- Vijana na Mabinti 99% ya stori zao ni Kungonoka tu au kwenda kula bata huku wengine wakiwa " vyura ".
- Vijana na Mabinti hawapendi tena kusoma na kupata MAARIFA ila wanapenda sana kukaa kupiga tu porojo, majungu na kuwasifia wenzao ambao wamewazidi maendeleo kwa mbali sana.
- Vijana na Mabinti wanakosa kabisa uwezo wa kujiamini na kujenga hoja mbele za Watu au jambo fulani.
- Vijana na Mabinti si tu hawawezi bali hawataki pia kuthubutu.
- Vijana na Mabinti wanajua sana idadi ya Vijiwe vya kuvutia Bangi / Unga na Zanahati za kwenda kutolea mimba walizopachikana.
- Vijana na Mabinti ambao ukiwa unatizama nao TAARIFA ya Habari ambayo ina umuhimu mkubwa wao wanakununia kama siyo kuondoka pale sebuleni lakini ukiweka tu Channel za Miziki au Bongo Movie wanarudi kwa kasi kuketi na kuangalia tena kwa bashasha zote.
- Vijana na Mabinti wakiwa shuleni au vyuoni wanatumia muda mwingi kutengeneza " Nyenzo " au " Mizola " au " Vibomu " vya kuingia navyo katika vyumba vya Mtihani ili wavitumie kujibia maswali lakini vitabu library vimeshika vumbi na vingine mende wakianza kuvitafuna.
- Vijana na Mabinti wanaona UFAHARI kupata Division One tena zile za Distinctions kabisa au FIRST CLASS Degree za KUKARIRI lakini katika APPLICATION ya kile walichokisomea 90% ni ZERO kabisa.
- Vijana na Mabinti wanaona SIFA kabisa KUAPIZANA kuwa wamalizapo tu kusoma huko Mashuleni au Vyuoni na kupata AJIRA basi kipaumbele chao ni KUIBA na KUJINEEMESHA.
- Vijana na Mabinti ambao wao Kazi ni zile tu za KUAJIRIWA Maofisini lakini kufanya KILIMO wanaona ni NUKSI, KUJICHORESHA na KUJISHUSHIA hadhi.
Karibu utoe lako la moyoni juu ya Kizazi hiki cha sasa kinachopotea cha GOLDEN GENERATION na kama kwa aina hii ya Vijana tulionao sasa wanaweza kurudisha GOLDEN GENERATION miaka 30 au 50 ijayo. Binafsi I am worried!