MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
1.ASKARI WA WANYAMA PORI KUFYEKA MAHINDI YA WANANCHI HUKO MBOZI.
Huu ni uonevu wa hali ya juu ambao hauwezi kuvumiliwa hata kidogo, hivi serikali hauwezi kufikiri kua Wananchi wakulima wa mahindi wa MBOZI ndio mahindi yao pia yamejaza Ghala la akiba ya chakula kwenye hifafhi ya chakula ya taifa?Ni nani aliyewatuma askari hao kwenda kufyeka mahindi ya wa Wananchi ambayo yalikua tayari yamekwisha stawi vizuri? Kwa unyama huu ni nani atakayesema kua Serikali ina nia njema na Wananchi wake? Kufyeka mahekari ya mahindi ambayo Wananchi wanahangaika pembejeo kwa nguvu zao wenyewe ni kuwasaidia au kuwafanyia unyama?
Kama hawakua sahihi kulima katika maeneo hayo hao askari walikua wapi wakati wanapanda mahindi hayo? Huu unyama una baraka za nani?
Nilishawahi kunena kuna watendaji watamhujumu Rais Magufuli na hawa ndio mfano wake, sidhani kokote alipo Mh Rais kama amefurahishwa na kitendo hicho!
Njia pekee ya kuwasaidia wanyonge hao ilikua tusubiri tu wavume mahindi yao na halafu baadaye kutumia utaratibu wa kisheria kuwazuia kuendelea kulima.
2.BOMoABOMOA MKOANI DAR.
Hili nalo ni janga lisilofaa linalofanywa kwa Mabavu bila kufuata taratibu za kisheria, mtu unajiuliza hivi ni kwanini serikali ina hasira na Wananchi kiasi hichi? Wameifanyia nini serikali?
Inawezekanaje unamvunjia mtu nyumba yake huku hukumlipa fidia ya kumhamishia,kiwananja unakompeleka hujampa na vielelezo vyote anavyo. Kama mtu anavyo vielelezo vyote vyenye ushahidi wa kutosha unambomolea nyumba yake kwanini tusiite kua huu ni uonevu?
Amesikika Kaimu mkuu wa mkoa wa DSM akisema kwa wale ambao wamebomolewa na hawakulipwa fidia au stahiki zao watafidiwa, hivi kabla hawajaenda kubomoa walishindwa nini kufanya uhakiki ili kujiridhisha kabla hawajabomoa? Watawahifadhi wapi wale ambao kwa sasa hawana makazi?
Hii kauli mbiu ya "hapa kazi tu" inatumiwa vibaya sana watendaji mizigo wa serikali waliozoea kuonea wanyonge pasipo kufuata taratibu za kisheria.
Sidhani kwamba kauli mbiu ya Mh Rais ya "HAPA KAZI" ilikua na maana ya kuanzisha uonevu kwa wanyonge wasiokua na watetezi badala ya kuwasaidia.
Kwa haya matukio mawili ni rai yangu kua wahusika wachukuliwe hatua za kinidhamu, Taasisi za haki za binadamu ambazo naona kama zimelala zifanye kazi zake za kuwatetea wanyonge badala ya kutumia migongo yao kujinufaisha wao binafsi.