kalulukalunde
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 1,056
- 1,083
July 15 2016 ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ‘Muhimbili‘ imeweza kufanya matibabu ya kumuwekea mgonjwa kifaa cha kusaidia moyo kufanya kazi zake kwa mtoto wa miaka mitano, kifaa hicho kinaitwa pacemaker operation hii ni ya kwanza kwa Tanzania kufanyika kwa mtoto.
Mtoto huyu alikuwa na ugonjwa unaoitwa concenital heart block uliokuwa unasababisha mapigo ya moyo kuwa chini sana na kumsababisha kushindwa kumudu maisha ya kawaida kwa umri wake.
Uongozi wa taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete ‘Muhimbili’ wamewataka watanzania watambue uwepo wa huduma hiyo katika taasisi na kwamba kwa wale ambao wanashida juu ya mapigo ya moyo, wanaweza kwenda kwenye taasisi na kufuatilia matibabu.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
Maoni yangu
Pongezi kwa madakatari waliofanikisha zoezi hilo na taasisi hiyo kwa ujumla wake, Pongezi poiia kwa Raiais Mstaafu JK kwa kuhakikisha taasisi hii inafanikiwa kwa kuiwezesha kwa kila hitaji katika utawala wako.
Pongezi pia kwa utawala wa awamu ya tano chini ya Dk. Magufuli kwa kuendelea kuingalia taasisi hii kwa jicho la karibu na kuwasaidia wataalam wetu hawa kwa kila hitaji lao.
Hakika hili ni jema na litakaloiletea heshima kubwa taifa letu.
Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Afrika