Kwa madaktari tu na wizara ya elimu

Kwa madaktari tu na wizara ya elimu

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
17,930
Reaction score
17,356
Zamani Vyuo vingi vikuu vya kufundisha udakaktari vilijengwa ndani ya hospitali kuu (za rufaa) kama vile Muhimbili, KCMC, na Bugando, na vilikuwa vinafundisha wanafunzi wachache sana. Lakini hivi sasa vyuo vya kufundisha madaktari na wauguzi vimejengwa hata nje ya hospital na vinachukua wanafunzi wa ngazi ya digree ya kwanza ya udaktari na uuguzi wengi sana kuliko vitendea kazi, walimu na wangonjwa wa kujifunzia.

MaSwali kwa madaktari na Mawaziri wa Elimu na Afya ni:

1. Je, nilazima daktari wa shahada ya kwanza asomeshwe kwa miaka 5?

2. Je, nilazima walimu watumie cadaver kumfundisha mwanafunzi wa udaktari au uuguzi wa shahada ya kwanza? Je, Kutahitajika cadaver ngapi zinazotoka wapi ili kutosheleza ongezeko la wanafunzi wa mwaka wa kwanza udaktari na uuguzi nchini kwa mwaka?

3. Kuongezeka kwa wanafunzi wa udakatari na uuguzi nchini kunamaanishaa kuongezeka pia kwa cadavers, walimu, wagonjwa, na hospitali za kufundishia wanafunzi hao?

4. Hakuna njia mbadala ya kumfundisha mwanafunzi wa mwaka kwanza udaktari bila ya kutumia cadavers na kuacha cadavers zitumike kwa wanafunzi wa Masters wa upasuaji?
 
Kwa kuwa mimi sio daktari naomba nikaimu nafasi ya mtu kwanza
 
Cadaver muhimu utaambiwaje Sternocleidomastoid kimaneno neno tu bila hata ya kuiona.
Theory na practical lazima vifuatane maana anaenda kudeal na maisha ya mtu.
 
Utajifunza ufundi makenika bila magari?, kadava ni muhimu kujua viungo mbalimbali kwa uterus kwa wanawake au prostate kwa wanaume
 
Cadaver ndio utajifunza anatomy vizur ,pathology vizur wliotangulia walikua na utashi wa kuona mbali sana...imagine unasoma nervous system kwenye vitabu tu then iishie hapo inakuaje? Cadaver ndio msingi
 
Cadaver muhimu utaambiwaje Sternocleidomastoid kimaneno neno tu bila hata ya kuiona.
Theory na practical lazima vifuatane maana anaenda kudeal na maisha ya mtu.
Kutokana na kuongezeka kwa technolojia duniani hivi hakuna njia nyingine ya kumuonyesha mwanafunzi deltoid muscle iko wapi mwilini na inafananaje mpaka utumie cadaver? Kumbuka kuwa sio wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza watamaliza mwaka wa tano, sio wote waliomaliza mwaka wa tano wataenda kutibu wagonjwa na sio wote wanaotibu wagonjwa watafanya upasuaji. Huduma za afya zinavyoendelea kuimarika nchini ndiyo hivyohivyo na kadava zinavyoendelea kuadima pia. Kwani wenzetu huko ng'ambo wanafanyaje? hebu tule desa kutoka kwao.

Pia tukumbuke kuwa kadri idadi ya wanafunzi wa shahada ya pili udakatari (MMed) inavyozidi kuongezeka madakatari wenye shahada ya kwanza watakwenda kufanya kazi za kawaida tu kwenye zahanati na vituo vya afya. Shortage ya madaktari bingwa nchini ndiyo iliyokuwa ikisababisha dakatari wa kawaida (MD) kufanya upasuaji mdogomdogo kama heniorathy, C/S, na incisions kuokoa maisha, lakini sio kazi yao kabisa.
 
Kutokana na kuongezeka kwa technolojia duniani hivi hakuna njia nyingine ya kumuonyesha mwanafunzi deltoid muscle iko wapi mwilini na inafananaje mpaka utumie cadaver? Kumbuka kuwa sio wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza watamaliza mwaka wa tano, sio wote waliomaliza mwaka wa tano wataenda kutibu wagonjwa na sio wote wanaotibu wagonjwa watafanya upasuaji. Huduma za afya zinavyoendelea kuimarika nchini ndiyo hivyohivyo na kadava zinavyoendelea kuadima pia. Kwani wenzetu huko ng'ambo wanafanyaje? hebu tule desa kutoka kwao.
Unajuwa ukiingia kwenye technology wenzetu wako juu sana tofauti na sisi halafu unapoisoma Anatomy hasa basi cadaver ni muhimu sana. Hata ukiangalia vyuo vya nje utakuta bdo wanatumia cadaver
 
Kujifunzaa kwa practical ni bora zaidi
Wengine tunaelewa kwa kuona
Unaniambia tuuu this is satorius muscle kwenye slide ...ukipewa mgonjwa unashangaaa
Ni ngumu sana medicine bila cadaver
 
Hahaha stenoclenomastoid muscle aka girlfriend muscles..
 
Kujifunzaa kwa practical ni bora zaidi
Wengine tunaelewa kwa kuona
Unaniambia tuuu this is satorius muscle kwenye slide ...ukipewa mgonjwa unashangaaa
Ni ngumu sana medicine bila cadaver
kuna technolojia ya 3D na 4D inaonyesha tissues zooote kama mtu kabisa na kupitiliza
 
Zamani Vyuo vingi vikuu vya kufundisha udakaktari vilijengwa ndani ya hospitali kuu (za rufaa) kama vile Muhimbili, KCMC, na Bugando, na vilikuwa vinafundisha wanafunzi wachache sana. Lakini hivi sasa vyuo vya kufundisha madaktari na wauguzi vimejengwa hata nje ya hospital na vinachukua wanafunzi wa ngazi ya digree ya kwanza ya udaktari na uuguzi wengi sana kuliko vitendea kazi, walimu na wangonjwa wa kujifunzia.

MaSwali kwa madaktari na Mawaziri wa Elimu na Afya ni:

1. Je, nilazima daktari wa shahada ya kwanza asomeshwe kwa miaka 5?

2. Je, nilazima walimu watumie cadaver kumfundisha mwanafunzi wa udaktari au uuguzi wa shahada ya kwanza? Je, Kutahitajika cadaver ngapi zinazotoka wapi ili kutosheleza ongezeko la wanafunzi wa mwaka wa kwanza udaktari na uuguzi nchini kwa mwaka?

3. Kuongezeka kwa wanafunzi wa udakatari na uuguzi nchini kunamaanishaa kuongezeka pia kwa cadavers, walimu, wagonjwa, na hospitali za kufundishia wanafunzi hao?

4. Hakuna njia mbadala ya kumfundisha mwanafunzi wa mwaka kwanza udaktari bila ya kutumia cadavers na kuacha cadavers zitumike kwa wanafunzi wa Masters wa upasuaji?
Mkuu wewe unasoma master's degree nikiwa na maana kwamba ushagraduate!
Vipi wakati wewe unasoma anatomy undergraduate ulitumia cadaver?
Je kwa uelewa ulionao sasa hivi ungeweza kuupata kama usingetumia cadavers?
 
khabar wadau, nimechaguliwa dipl ya ICT hapo Udom but me napendelea EDUC au LAB. nifanyaje?????
 
Msikurupukie teknolojia ....mfano ni kama half cooked doctors from(KC.mmc) sorrry but truth be said.

Usiige kwa kukurupuka mkuu...jiulize huko uingereza au abroad wanapofundishiwa midoli wanashika mtu baada ya miaka mingapi ya training?

Je una muda wa kusubiria hizo teknolojia na nguvukazi? ilihali hospitali za rufaa bado zina AMOs?
 
anatomy&physiology ndio msingi wa udaktari hapo cadever ni muhimu.(study of human structure ndiyo anatomy & study of human function ndiyo physiology)
 
Mkuu wewe unasoma master's degree nikiwa na maana kwamba ushagraduate!
Vipi wakati wewe unasoma anatomy undergraduate ulitumia cadaver?
Je kwa uelewa ulionao sasa hivi ungeweza kuupata kama usingetumia cadavers?
Cadaver ni nzuri sana maana ni kitu halisi, shida yake kwa sasa ni upatikanaji wake kukidhi ongezeko kubwa la wadahiriwa, pili usafirishaji wake, tatu utunzaji wake, nne magonjwa yanayoweza kuambukizwa kama uangalifu kwenye kuwa treat na tano harufu yake. Kama siku hizi tunatumia teleconference na online examinations kufundishia wanafunzi ili kutatua tatizo la uhaba wa walimu, madarasa na kusahihisha mitihani kwanini tusifikirie kwa sauti kutumia njia mbadala kama manikins kutatua shida ya cadavers vyuoni? nani afe wewe ujifunzie?
 
Msikurupukie teknolojia ....mfano ni kama half cooked doctors from(KC.mmc) sorrry but truth be said.

Usiige kwa kukurupuka mkuu...jiulize huko uingereza au abroad wanapofundishiwa midoli wanashika mtu baada ya miaka mingapi ya training?

Je una muda wa kusubiria hizo teknolojia na nguvukazi? ilihali hospitali za rufaa bado zina AMOs?
Mbona huko mzee ndiko hukohuko tunakopeleka matezi dume ya vigogo wetu?
 
Cadaver ni nzuri sana maana ni kitu halisi, shida yake kwa sasa ni upatikanaji wake kukidhi ongezeko kubwa la wadahiriwa, pili usafirishaji wake, tatu utunzaji wake, nne magonjwa yanayoweza kuambukizwa kama uangalifu kwenye kuwa treat na tano harufu yake. Kama siku hizi tunatumia teleconference na online examinations kufundishia wanafunzi ili kutatua tatizo la uhaba wa walimu, madarasa na kusahihisha mitihani kwanini tusifikirie kwa sauti kutumia njia mbadala kama manikins kutatua shida ya cadavers vyuoni? nani afe wewe ujifunzie?
Huna hoja dhaifu kabisa!
 
Back
Top Bottom