Kwa kweli Mungu ni mkuu

Kwa kweli Mungu ni mkuu

Killeville

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2015
Posts
410
Reaction score
1,218
Katika uumbwaji wa viumbe, binaadamu ni kiumbe cha mwisho kabisa kuumbwa. Hata baada ya kukamilika uumbwaji wake, kisha kuletwa duniani, mahitaji yake ya kimwili na kimazingira yalishakuwepo ili kumsapoti.

Ni katika hekima za uumbaji, ambapo kiumbe kimeumba na kuwekewa mifumo na taratibu zinazoendana nacho, mfano kutembea, kula, kujamii n.k.

Kiukweli, yapo mambo(kwa wenye kutafakari) ukiyaangalia kwa mapana yake, unaiona hekima ya muumbaji, mfano, mimea ya kutambaa chini kuzaa matunda makubwa na miti kuzaa matunda madogo, mfano mwingine ni wanyama wakubwa kwa wadogo kunyimwa utashi kama wa binadamu(pata picha wangepewa hali ingekuwaje).

Lakini jingine, ni namna dunia ilivyoumbwa, sehemu kubwa ya dunia (75%) imejawa na maji na kuacha sehemu ndogo tu (25%)ya ardhi, lakini pamoja na hilo kuna sehemu katika ardhi mvua ni ndoto za aliyemacho, bi maana ni nadra sana kunyesha mvua katika maeneo hayo. Hebu jaalia kuwa hii 25% ya ardhi ndiyo ingekuwa maji na 75% ya maji ingekuwa ardhi.

Hapo ndipo tunapoona hekima na ukuu wa Mungu.
 
Mambo yote hayo ila ajabu kuna watu wengine hadi sasa hivi hawajua kwanini watu wanaamini mungu,wanadhani ni jambo la kurisishana.
 
TAFUTA MTI WA FENESI ANGALIA MAFENESI YANAPOOTA NA MWEMBE ANGALIA MAEMBE YANAPOOTA HALAFU TAFAKARI NDIO UTAJUA HEKIMA YA MUUMBA
 
Au angalia tu kwenye kichuguu mchwa wanavyogawana kazi. Au ndege anavyomlisha mtoto wake kwa upendo: utafikiri ni mama anamnyonyesha mtoto wake kwa furaha...
 
Yapo mengi sanaa ya kutukuza Ukuu wa Muumba/Mungu aisee, mi nikiufikiriaga Ubongo na Akili huwa nastaajabu sana

Wale wanaoamini eti binadamu alitokea kwenye evolution inabidi wajitafakari haswa
 
Hata hiyo evolution/revolution nayo ilianzaje?

Yote ni maajabu ya Mungu hakika!!
Yapo mengi sanaa ya kutukuza Ukuu wa Muumba/Mungu aisee, mi nikiufikiriaga Ubongo na Akili huwa nastaajabu sana

Wale wanaoamini eti binadamu alitokea kwenye evolution inabidi wajitafakari haswa
 
Histori ni uongo sana na uzandiki ndio maana nilipata D kwenye Histori nilacha kusoma form ll ila nikafanya nalo mtihani nilikuwa najaza uongo sana
 
Ukifikiria kwa hakika MUNGU ni Mkuu .Majira ya Mwaka ,Upevukaji wa Mwanaume na Mwanamke na utofauti wake kwa ujumla .Geographia ya Dunia na Nguvu ya kupambana na Roho Waovu .
 
Back
Top Bottom