bomouwa
JF-Expert Member
- Jun 19, 2014
- 1,149
- 798
Habari wanajamvi?
Katika mechi ya leo,kwa wale waliobahatika kuangali watakubaliana na mimi ya kua Yanga wamecheza mchezo mzuri na wa kiwangi cha juu mpaka kuwafanya waarabu washangae na kuanza hujuma za kuwasha fataki kusambaza moshi katika upande wa lango la Yanga.
Najua wapo watakaosema kua Yanga wangetoka tu!lakini ama kwa hakika,mchezo wa leo umedhihirisha pasi na shaka kua Yanga ni team nzuri iliopo kimkakati na pengine isingekua goli la kushtukiza la dakika ya 95 ya mchezo basi Yanga ingefika mbali.
Pongezi nyingi zimuendee Thaban Kamusoko ambae ameumudu mchezo vizuri kama kiungo lakini pia Oscar Joshua ambae alimudu kasi ya mchezo vizuri sana.Kwa upande mwingine,Dida alifanya kazi ya ziada sana pamoja na.mabeki wake maana mda mwingi makosa yalipojitokeza alionekana akielekeza kama pro player na si mropokaji.
Nadir Haroub ama hakika ni nahodha wa kisawasawa maana ameonyesha umakini wa hali ya juu achilia mbali hasira na zile harakati za fujo alivokua mbele kutuliza makamanda wake lakini pia Donald Ngoma nae sifa zimfikie naona kabisa katika usajili ambao team ya Yanga haikikosea ni kwakijana huyu.
Najua watu wataongea sana lakini uzi huu haimaanishi kua mimi ni mwana Yanga lakini nimebahatika kuangalia mechi mwanzo hadi mwisho kwakweli nimevutiwa mnoo na soka walilolionyesha team ya Yanga.
Asanteni.