commonmwananchi
JF-Expert Member
- Mar 12, 2011
- 3,377
- 1,954
WanaJF,
Mimi napenda kujadili bila matusi bali hoja na mijadala mipana.majuzi chama cha mapinduzi (CCM)kilifanya mkutano wake mkuu maalum huko dodoma.
Moja ya ajenda kuu ilikuwa ni kujadili na kupitisha marekebisho ya katiba ya CCM ya mwaka 1977,bila shaka toleo la 2012,ikiwa ni pamoja na kanuni za chama na jumuia zake.
Kwenye mabadiliko hayo kuna walioumizwa kwa kufukuzwa uanachama na wengine kupewa makaripio,na pia wengi wamepoteza nyadhifa kadhaa walizokuwa nazo hapo awali.kutokana na muundo mpya wa CCM na kamati zake.
Hasa lile la kofia mbili kwa maana ya nyadhifa nyingi kwa mtu mmoja.
Hili peke yake limetuonyesha ukomavu wa demokrasia ndani ya chama chao.
Kwani angalau wameitisha mkutano mkuu,wamejadiliana na hatimaye kupitisha mabadiliko ya katiba yao.sambamba na kuadhibu waliokiuka taratibu za chama chao kwa hilo binafsi nawapongeza.
Ingawa sina uhakika na kitakachojiri baada ya hapo lakini ni ukweli usippingika kwamba takribani ukiangalia vyama vyetu vyoote vya upinzani Tanzania .
Jaribio la kufanya kilichofanywa na CCM huko dodoma wiki iliyopita linaweza kutishia kukiuwa chama husika na mifano hai tunayo.
Angalia wapinzani wakuu wa CCM,yaani CHADEMA wameshindwa hata kuitisha mkutano ili kutathmini kilichowaangusha katika uchaguzi uliopita,
Si hilo tu bali hata ile turufu yao kuu ya vita dhidi ya ufisadi,Richmond,EPA nk ambayo ndio ilikuwa turufu yao kubwa kisiasa,nayo wameitupa bali sasa kiaina flami wanakuwa watetezi wa walewale walokuwa wakiwashutumu hadharani.
Na si uongo kwamba sasa ukawa kwa ujumla wanancheza ngoma ya CCM,wapinzani wamekuwa kama kamati fulani ya ccm.
Sera zao rasmi hazieleweki,wako busy kujadili matukio ya ccm na viongozi wao,badala ya kuwa makini na mustakabali wa vyama vyao.
Hakuna mwananchi anayeweza kukujibu swali ukimuuliza nini agenda rasmi ya CUF,CHADEMA na UKAWA kwa ujumla hivi sasa,zaidi ya kubeza jitihada za mheshimiwa Rais JPM.
Na kwa kuzingatia kwamba baadhi ya vyama vya upinzani democracy iko midomoni mwa viongozi na si mioyoni mwao,tunayo kumbukumbu ya kina mabere na mrema,kina lamwai,huko mwanzoni na hata hivi karibuni tunao kina zitto Kabwe,kitilya mkumbo na kina professor safari.
Na bila kusahau
Lipimba vs maalim nk!
Je kwa mtaji huu mna ndoto za kuiondosha madarakani CCM kwa mtaji upiiii.
Wale mnaohoji kupunguzwa idadi ya wajumbe wa vikao vya CCM,mnasahau kwamba kuna idadi kubwa pia ya nyadhifa za kichama ambazo zinapaswa kuzibwa na haohao baada ya uamuzi wa kofia moja?
Tanzania itajengwa na wenye uzalendo wa kweli
Ahsanteni naomba kuwakilisha