Kwa kifurushi hiki cha bufee pack TTCL mmetisha sana

PendoLyimo

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
879
956
Nukuu Mbalimbali za Mkurugenzi wa Biashara TTCL Ndugu Vedastus Mwita kwenye Uzinduzi wa Kifurushi kipya kutoka @ttcl_corporation kinachoitwa BUFEE PACK.

"Kifurushi hiki ni cha watumiaji wote wa mtandao wa TTCl hakina ubaguzi wowote ni kwa ajili ya watumiaji wetu kuanzia wanafunzi, wanahabari, wanamichezo, na watu wote ambao ni watumiaji wa mtandao wetu wanakaribishwa kujiunga na kifurushi hiki kwa kupiga *148*30# Kisha chagua namba 6" Vedastus Mwita Mkurugenzi wa Biashara Ttcl

"vituo vyetu vyote Tanzania vipo Tayari kuwasajili wateja wote nchi nzima na tunawakaribisha kujiunga na Mtandao wetu huu wa TTCl Ili kuweza kupata huduma bora ambazo zitaendana na kile ambacho unahitaji kutokana na kifurushi Chetu kipya cha Buffe pack ambacho kina dhamira ya kuchagua kile unachotaka" Vedastus Mwita Mkurugenzi wa Biashara Ttcl

"Tunatoa shukrani kubwa kwa wateja wetu ambao wamekuwa wakitumia huduma zetu kwa ajili ya mawasiliano kwenye maeneo mbalimbali nchini kama Shirika tunaendelea kushirikiana nao vyema kwa kutoa huduma bora ambazo zitaendana na matumizi sahihi ya mawasiliano na vifurushi vyenye ubora mzuri" Vedastus Mwita Mkurugenzi wa Biashara Ttcl

"Ni kawaida yetu Kama TTCl tunapoelekea katika kufunga mwaka tumekuwa tukiwapatia zawadi wateja wetu ambapo kwa mwaka huu tumeona tuje na zawadi kubwa ambayo itaongeza chachu katika matumizi ya Mawasiliano na zawadi hiyo ni kifurushi chetu kipya cha BUFEE PACK" Vedastus Mwita Mkurugenzi wa Biashara Ttcl

"Suala hili la uzinduzi wa kifurushi hiki linakwenda sambamba katika kuelekea kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora ya Mawasiliano ambazo mteja atakuwa huru kuchagua kile anachotaka kwa ajili ya kuwasiliana na kuinua wigo wa mawasiliano nchini" Vedastus Mwita Mkurugenzi wa Biashara Ttcl

" Kifurushi hiki cha Bufee pack ni kifurushi ambacho ni bomba na kitakachomsaidia mtumiaji kutengeneza kifurushi anachotaka yeye kuanzia kiwango cha dakika, Message
IMG_20211126_123414_764.jpg
IMG_20211126_130512_687.jpg
 
Hamna lolote hapa, Eti 1 GB inauzwa Tsh 2560 😂😂😂😂😂😂😂
Kweli nimeamini huu mtandao ni wa watumishi wa Umma tu sio kwa ajili ya wananchi wote.
 
Back
Top Bottom