Kwa kashfa hizi, CCM haifai kuongoza tena

Kwa kashfa hizi, CCM haifai kuongoza tena

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Watanzania tuseme inatosha. Sisi wazalendo tuliopo CCM tunataka mabadiliko. Mabadiliko ya kiuongozi. Kashfa ya ngapi hii? Hamchoki dharau zetu na kujiamini kwetu? Hamchoki wizi wetu na kulindana kwetu? Ufike wakati mchoke na kukipumzisha chama chetu ili tujute na kujipanga upya.

Amini nawaambia,ndani ya CCM ufisadi hautaisha. Fedha za watanzania zitaendelea kuliwa bila huruma. Hata Serikali ivunjwe na kuundwa mara ngapi,hakutakuwa na jipya. Teuzi katika tafsiri za kichama ni zamu ya kuvuna. Hakuna kiongozi ndani ya chama hiki asiye na vimelea vya ufisadi. Ni kuzidiana tu

Chaguzi zimekaribia. Watanzania fanyeni maamuzi. Maamuzi ya kukipumzisha chama tawala. Mazoea yananoga. Mkikiacha chama hiki,msilalame tena juu ya ufisadi huu au ule. Tanzanians...power to us!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Wataendelea tu kuongoza kwa kwa kuchakachua kura kwa kuwa hakuna tume huru ya uchaguzi.
 
Haihitaji kumung'unya maneno! CCM ni wezi.
1) EPA
2) RichMond
3) Rada na chenji yetu
4) Meremeta
5) Back then Uuzwaji wa NBC
6) Meno ya Tembo
7) Twiga wetu wale waliopanda ndege
8) Sasa Escrow!
9) Etc.
10) Etc
11) Etc
Hawawezi kuwa serious! Hili ni Pango la majangili wa nchi hii.....formula ilivyo ni kwamba kila Jangili ili mambo yake yamuendee vyema anajiunga na haya Majangili menzake.
Inasikitisha na inatisha sana kwa mambo yanayofanywa na hawa Magamba! Imefika wakati wa kusema HAPANA.
CCM inanuka uozo! Uozo ambao hata baba wa Taifa afufuke Leo HAWEZI kuusafisha! Hawasafishiki hawa majamaa!
 
Ingekuwa nchi yetu inaendeshwa kidemokrasia kama nchi nyingine zilizokomaa kidemokrasia, kwa uzito wa kashfa hii ya Escrow account, ingelazimu serikali yote ya CCM iwe imeshajiuzulu na nchi ingepaswa kuingia kwenye uchaguzi mkuu, kabla ya muda wake uliopangwa wa mwaka 2015!

Tofauti kubwa ya nchi yetu ni kuwa mhimili wa bunge, ambao ndiyo unaoisimamia serikali kwa niaba ya wananchi, unaingiliwa mno na mihimili hiyo mingine, ambayo ni mahakama na serikali, ikiwemo Ikulu yenyewe!

Sasa wananchi ndiyo tunazidi kupata mwanga zaidi ni kwa nini BMK chini ya Samuel Sitta waliamua kuvinyofoa vifungu vya kwenye Tume ya Warioba, vilivyotaka uadilifu na uwajibikaji viwe miongoni ya tunu za Taifa, na vile vile kupunguza madaraka ya Rais ya uteuzi wa nafasi zote, zikiwemo za majaji wa mahakama kuu.

Tumejionea athari zake kutokana na skandali hii ya Escrow/IPTL kuwa miongoni ya waliopata mgawo wa Escrow, ni majaji wa mahakama kuu, mawaziri, makatibu wakuu na mwanasheria mkuu wa serikali, ambapo nafasi zote hizo, ni za uteuzi wa Rais.

Ndiyo sababu kuu, inayofanya kwa sasa zinafanyika juhudi kubwa sana ya vyombo vyote vya dola, kama vile usalama wa watawala wa CCM, policcm, mahakama na Ikulu yenyewe, kuhakikisha kuwa ripoti hiyo ya Escrow account, haipati nafasi hata ya dakika moja kujadiliwa bungeni wiki ijayo!

Kwa kuwa watawala wa CCM kwa sasa wanajua kuwa, kuruhusu mjadala wa wazi bungeni wiki ijayo, ni sawa na CCM kujitwalia kamba na kuitandika darini na kuzitundika shingo zao ili wajinyonge!

Kwa hiyo kwa watawala wa CCM wako tayari kwa njia zozote za haramu kuzuia ripoti ya CAG isijadiliwe bungeni, hata kama wanajua kuwa uamuzi wao huo wa hatari sana, unaweza kusababisha, machafuko makubwa hapa nchini, hadi kupelekea umwagikaji wa damu!
 
Kweli kabisa. Tunashindwa na nchi kama Burkina Faso? Huku ni kulala kwa namna gani? Hata kama wakichakachua, ifike mahali tusome basi, liwalo na liwe, ala!!!
 
Ccm ni janga tena kubwa, niwakati sasa wananchi wakuchukua Maamuzi magumu tunaitaji mabadiliko makubwa sana
 
Watanzania hawajui hilo...wenyewe poa tu .. Ccm nambari one. T shirt na kofia zinatosha.. Usishangae ccm ikizoa kura za kishindo dsm
 
Kweli kabisa. Tunashindwa na nchi kama Burkina Faso? Huku ni kulala kwa namna gani? Hata kama wakichakachua, ifike mahali tusome basi, liwalo na liwe, ala!!!

Vijana Wa Tz hamwezi bwana, nyie kalieni kuiga milegezo tu!!
 
Ikitoka kashfa hii,itakuja nyingine.Ni bandika bandua

Mzee Tupatupa
 
Yatupasa kujua kuwa tatizo si lowassa,au mwingine yoyote ndani ya CCM, bali swali la kujiuliza kama watanzania ni tunategemea nini kipya matumaini nchi hii chini ya utawala wa ccm wa miaka hamsini na tatu ( 53)?!

Yatupasa kujiuliza tangu wawe madarakani ni huduma gani ya kijanii angalau moja ambayo inapatikana tanzania nzima bila mizengwe , yes namaanisha moja.

Wakitujibu hilo tunaweza kuwafikiria kidogo,kinyume na hapo hatuna sababu ya kuwasikiliza tena.
 
Back
Top Bottom