kadendu
JF-Expert Member
- Mar 30, 2014
- 643
- 497
kwanza tunakupongeza kwa namna ulivyoanza vema kushughurikia swala mauaji ya kijana saimon mapunda (24)yaliyotokea jana kwenye kituo cha polisi mtera,hakukuwa na ulazima wowote askari mwita kumshambulia yule kijana akiwa chini ya ulinzi tunaomba kama alivyotuambia leo rco dodoma kwamba mwili wa marehemu utafanyiwa uchunguzi basi haki itendeke akuna asiyejua mtera yote kwamba saimon alipata kipigo haswa na askari mwita,ikumbukwe kwamba mwaka juzi diwani wa kata ya mtera alimlipoti askari mwita tabia yake hii ya kujichukulia sheria mkononi kwa ocd mpwapwa na sio mala moja tunaomba awajibike kwa matendo yake huna sababu ya kumlinda askari wa aina hii nikutakie kazi njema.