Kwa hili wataalamu uwezekano upo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa hili wataalamu uwezekano upo?

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Thinker96, Sep 14, 2012.

 1. Thinker96

  Thinker96 JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2012
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 294
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Niwashukuri wakuu na MUNGU wangu awape nguvu, naomba mnipe msaada me binafsi namiliki laptop ya enzi hizo Dell latitude D620 na ina sifa zifuatazo Processor 2GHz, 40 HDD,1GB RAM sasa basi kutoka na mapinduzi ya technology nataka nibaki na kimashine changu lakini nataka nibadili sifa zote na niweke za kiwango cha juu yaani Processor 3.5ghz,Hard disk 250gb,RAM 4gb. Je kipi kinawezekana na wapi naweza kupata na kwa bei gani?
   
 2. leh

  leh JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 846
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  vyote ulivyotaja vinawezaekana. bei itategemea na aina ya vifaa vilivyo ndani. kwanza kubadilisha hard disk (HDD) ya laptop ni mteremko, hata kama hujawai fungua laptop. cha msingi tu ni kujua kama ni ya SATA au IDE, hazi ingiliani. kujua ipi ni ipi, nenda kwa device manager, fungua disk drives zako na uangalie watakuwa wameandika ATA au IDE. ya kwangu hapo chini kama unavyo ona ni ya ATA

  [​IMG]

  utatafutana na HDD ya ATA au IDE ya laptop madukani na umemaliza

  ukifika kwa RAM, kuna jinsi nyingi za kujua speed yake, ila sasa hapa bongo mafundi wengi hawaelewi speeds za RAM ni nini kwa hiyo, itabidi ucopy zile number ambazo zipo kwenye RAM (maelezo kuhusu kujua number hapo chini)

  kwenye kubadilisha Processor, hapo ni story ningine. kwanza nitakushauri usibadilishe kwasababu mbili
  1. gharama ni kubwa, bora ununue mashine mpya
  2. inabidi uwe mtaalamu wa kutosha

  ukitaka badilisha processor, lazima ujue MOBO (motherboard) ya laptop yako because processor zinatumia meno kama za hdd vile ila sasa zina meno mia tofauti sio kama hdd ambazo ni aina mbili tu. hivi basi, unakuta MOBO ina meno ya processor tofuti tofauti na hazi ingiliani. baado bei. utakuta bei za processor ya laptop ni laki mbili na kuendelea. hapo bado RAM na HDD, si bora mashine mpya. kuna kitu kinaitwa overclocking ambapo ni kufanya processor au RAM ikimbie zaidi ila kwa laptop sishauri coz hazina matundu ya kutosha kutolea joto na ukioverclock computer inatumia joto zaidi na basi unaweza unguza processor. itabidi uridhike na hiyom processor kwa sasa.

  tufike kwa kubadilisha. laptop zote zinafungwa mara mbili (with a few exceptions). sehemu ya kwanza panapofungwa laptops mafundi wapaita expansion area na ndo utadeal napo. ukigeuza laptop yako, utaona kuna sehemu zimefungwa screw ampapo ni kama box ndogo (kiswahili kinanipa chenga) na hapa ndo ukifungua utaweza kuona HDD yako na RAM.
  [​IMG]

  kuna laptop zinafungwa RAM box tofauti na HDD tofauti. kama unavyo ona hapo juu, ukifungua laptop cover ya RAM utaweza kuona namba zimeandikwa kwenye RAM. copy hizo namba ukaulizi madukani bei. kitu cha msingi kujua ni kuwa sana sana kutakuwa na RAM sticks mbili mle ndani na mmoja huwezi fikia inakuwa imewekwa ndani mpaka ufungue mashine yote ili uweze badilisha, kitu ambacho kama we sio fundi sikushauri. kuhusu kubadilisha, ni kazi tu ya kufungua pin zilizobana pembni na kupachika mpya

  kwa HDD, kubadilisha ni vile vile. unakuta HDD ya ndani wameweka chuma au plastic, itabidi urudishie hiyo plasticc kwa hiyo HDD mpya, inakuwa ni ya kusaidia kuprotect from shock
  baada ya hayo yote, ningekushuri ununue bidhaa zote then umtafute fundi akufungie ila umsimamie ili na we uweze kujua. kazi rahisi, utakuwa mtaalamu baada kuona mara moja
  [​IMG]
   
 3. leh

  leh JF-Expert Member

  #3
  Sep 14, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 846
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  nimesahau kusema, kabala hujafungua laptop yako, chomoa charger na battery!!!! zingatia mno huu ushauri
   
 4. Thinker96

  Thinker96 JF-Expert Member

  #4
  Sep 14, 2012
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 294
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mungu wangu akuzidishie ujuzi kweli nimependa sana ulivyonieleza ngoja nianze practical. Kwa hyo kwenye suala la processor niwe mvumilivu maisha yangu na dell yangu nashukuru sana. kwani me mgonjwa wa external hdd ndo maana nikasema ni kheri nitafute hdd ya kukaa humo humo maana external sijui ni mbovu au mimi ndo nina matunzo mabovu sijui hata.
   
Loading...