Kwa Hili Wanasongea hatuna MP?

kuku dume

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
414
62
Kikwete alihamua kuwapooza Wanaruvuma kwa kumteua Bw. Emmanuel Nchimbi kuwa waziri.

Hii ilimfanya kujisingizia majukumu ya uwaziri na kututenga Wanaruvuma.

Ni mwezi wa pili tuliandamana kupinga mauaji ya raia wasiokuwa na hatia yaliyokuwa yakifanywa na watu wasioeleweka.

Bwana Nchimbi hakufuatilia kujua chanzo cha raia kuuawa na wala hakufika kuwapa pole wahanga wa vipigo vya polisi.

Miundombinu ni mbovu sana. Kwa mfano tazama picha ya Kituo kikuu cha mabasi mjini Songea.

Huduma za kijamii hazipo na kama zipo hazikidhi.

Wanasongea tumehamua kuiweka Chadema madarakani. Tunasubiri uchaguzi tumsapoti Bw. Edson Mpogolo. Tunaamini kwamba atatusaidia kujikwamua KIMAISHA.
 

Attachments

  • St.jpg
    St.jpg
    28.5 KB · Views: 55
bora wewe umeshtuka mapema.......
wahimize na wenzio.......
 
Ndiyo umejua leo?

Mboana tangu 2005 Songea haina mbunge! Hata vikao ya RCC hahudhurii.
 
Majukumu ya diwani hayo, Nchimbi ni mambo ya kitaifa

Kwani huwa mbunge siyo mmoja kati ya wahudhuriaji wa vikao vya halmashauri?

Mmbona majembe kama akina Lema, Sugu na wengineo wanafanyaga kweli kwenye vikao?
 
Majukumu ya diwani hayo, Nchimbi ni mambo ya kitaifa

Mkuu
Mambo ya kitaifa ni yepi??

Mbona kila siku mnaleta nyuzi hapa kuwasakama kina Mnyika?? Hua mnasahau kwamba kuna madiwani sio?? am hua mnafanya makusudi?? Mkiguswa nyie mnaleta double standard zenu hapa!!

Kwa hiyo wananchi waliouawa Songea halikuwa jambo la Kitaifa?? Vipi kuhudhuria vikao vya RCC??

CCM ni janga kabisa na wanchama wake ni misukule!!
 
Back
Top Bottom