Kwa hili,utafanyaje?

Ndalilo

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2013
Posts
3,674
Reaction score
8,313
Salaam Waungwana,

Mwanaume unamtongoza binti,kwa utashi,akili,utimamu,utahayari na uelewa wake anakukubali na kuanza mahusiano ya kimapenzi na wewe. Wote mnakuwa na furaha na mahusiano yenu na mnapanga mipango mingi ya kimaisha pamoja na kapeana ahadi za kuishi pamoja kwa ndoa. Lakini katikati ya furaha ya mapenzi unagundua mwenzio ametongozwa na ameridhia kuwa na mwingine zaidi yako. Kama alivyokukubali wewe ndivyo alivyomkubali na huyo mwingine na kwakujua kuwa ukijua hutoafiki,anakuficha.

Kwa hili, kuna sababu ya wewe kuchukia,kuwa mkali au kuanzisha bifu na mwanaume mwenzako au kumchukia mwanamke huyo? Akiomba msamaha ili muendelee, utamsamehe? Tena pengine akwambie alipitiwa na shetani,je usingegundua angekuwa anapitiwa na malaika?

Nini cha kufanya kwenye hali kama hii?
 
Kwa mtazamo wangu huwa siafiki kitu kinachoitwa kupitiwa na shetani anyway ngoja nirudi kwenye mada. Ktk hali kama hiyo huyo mdada hakupendi bali anajaribu kuangalia maslahi zaidi na kuwacompare ili ajue yupi kati yenu atamfaa. Au pengine yuko kikazi zaidi si unajua mjini kuna mengi ndugu yangu. Unapoonyeshwa tabia ya namna hiyo mapema jua kuwa mtu huyo hata ukijilazimisha kumsamehe elewa kua hatobadilika sana sana unataka kujiingiza kwenye pressure za ajabu tu. Lakini waswahili wanasema kipendacho roho.........Naogopa kusema muache aendelee na wengine. Pia hakuna sababu ya kugombana na mume mwenzio hapo mwenye tatizo ni mdada pengine hata mume mwenzio hajui kadanganywa kama wewe. Eti Kaunga unasemaje na FP hebu njoo utoe mtazamo wako ktk hili
 
Last edited by a moderator:
Ukiona msichana aliye kwenye mahusiano anatongozeka kuna haya:
1. Ni kicheche
2. Kuna kasoro kaiona kwako mwanaume ambayo kwake ni kero na hana namna ya kuibadili.
3. Haoni "future" yoyote na mwanaume aliye naye hivyo wakati wote hujiona yupo mtegoni.
4. Ana kutimiza malengo yake hivyo kuona kama muda unamtupa mkono (Hili hutukia sana).
5. Mwanaume hana thamani kiuchumi
 
Kwenye mapenzi kuna mengi, kuna watu kabla ya hicho kinachoitwa kukubaliana kimapenzi anaweza tumia gia kubwa kuliko uhalisia, ilimradi apate kufanikisha mpango wake, hapa namanisha uongo. Sasa pindi uongo huo unapothibitika kwa kweli hapo mapenzi hayo lazima yawe mashakani, kifupi wanaume wengi hatupo wakweli mwanzoni.

Tunaweza kutumia gharama kubwa mwanzoni kwa ajili ya kumnasa mtoto wa kike na kumuaminisha kuwa hiyo ndiyo life style yetu, na kwa vile naye hana mapenzi ya dhati atavutika kwa muda huo ili hali akipima upepo, once hiyo kitu ikianza ku-decay taratibu naye atakuwa anaona, na kwa vile watoto wa kike kutongozwa si kitu kigeni inakuwa rahisi kukubali mitongozo mipya na mwisho wa siku anavunja ule aliokuwa nao mwanzo.

Sio tabia nzuri kubadili mahusiano kama nguo, maana inajenga mazoea fulani kwenye maisha ya mtu na mwisho wa siku inakuwa majuto kwenye maisha. Hii hali imewafanya watu wengi kwa jinsia zote ME & KE kushindwa kuwa wavumilivu hata wakati wako kwenye ndoa halisi na kujikuta ndoa zao zikivunjika pasipo sababu za msingi sana.

Mwisho tuwe wawazi hasa kiuchumi kwenye mahusiano yetu hasa mwanzoni ili kuepuka kueleweka tofauti kwa wale tuwatakao, ukiona dalili za matatizo mwanzoni kabisa mkalishe chini mwenzako mzungumze ili kama mnashindwana iwe mapema kuliko kupotezeana muda na mali na kwa kufanya hivyo machungu ya kuachana sio makubwa pia.
 


Sasa mkuu unadhani ukiogopa kusema utakuwa na msaada wowote?
 
mambo mengine shetani wanamsingizia kutongozwa na kumkubaki mtu mwingine shatani kahusikaje hapo
afu kutongozwa ni jambo moja kugegedwa nae je ushafikiria hilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…