Kwa hili; serikali ifikirie kwa mapana zaidi

Emanuel Didas

New Member
Sep 19, 2011
3
0
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia idara yake muhimu ya kukusanya mapato (TRA) ilihamua kuboresha mfumo wake kukusanya mapato kwa kutumia kifaa cha kielectronic ambacho pindi mfanyabiashara aingizapo bidhaa aliyouza ripoti yake hufika moja kwa moja makao makuu. Katika mfumo huu kunajumuisho la VALUE ADDED TAX (VAT) ambayo ni asilimia 18%. Hii asilimia kumi na nane inalipwa na kila mtu atakaye kuwa anatumia mashine hiyo.

Mashine hizi zimegawanyaka kwa kila tabaka la kibiashara;

1. WAZALISHAJI WA BIDHAA

2. WAUZAJI WA JUMLA NA

3. WAUZAJI WA REJA REJA.
Kwa sababu hizi mashine zote zinahusisha kodi ya ongezeko la thamani (VAT); MIMI NAINGIWA NA SHAKA NA KUJIULIZA MASWALI YA FUATAYO;-

KWANZA SOMA MFANO HUU ILI IWE RAHISI KUELEWA MASWALI YANGU.


AZAM COMPANY limited wamezalisha bidhaa ( azam ngano, soda n.k) na wakamuuzia muuzaji wa jumla kwa bei ambayo inajumuisho la VAT yaani 18% ya bei ya bidhaa hiyo, na huyo mfanyabiashara wa jumla naye ana mashine yake ambayo pia itaenda kumkata VAT pindi anapomuuzia muuzaji wa reja reja, pia na huyo wa rejareja ana mashine yake ambayo itaenda kumkata VAT (18% ya bei ya kuuzia) pindi anapomuuzia mtumiaji wa mwisho (final consumer).

MASWALI YANGU NI HAYA;-


1. Je kodi ya ongezeko la thamani inapaswa kulipwa mara ngapi kwa bidhaa moja?

2. Je wauzaji wa jumla na wale wa rejareja hawachukui bidhaa ambazo tayari wazalishaji wake wameshalipa hiyo kodi ya ongezeko la thamani? Iweje basi wote wawe wanalipa kodi ya ongezeko la thamani kwa hiyo hiyo bidhaa moja kwa wakati tofauti?

Je SERIKALI haioni kama inataka KUWAUWA wananchi ambao wengi wao mjini wanajishughulisha na biashara za wastani na ndogo ndogo?

MAONI YANGU


ILI KUWA NA MAFANIKIO NA MFUMO BORA KABISA WA KUKUSANYA MAPATO;

SERIKALI KUPITIA TRA;-

1. Ingehakikisha kodi ya ongezeko la thamani (VAT) inalipwa mara moja kwa kila BIDHAA moja isipokuwa zile bidhaa ambazo hazitozwi kabisa kodi hiyo kutokana na sehemu zinakotumika (JESHINI)

2.Kama mashine hiyo itaendelea kutumika basi suala la VAT LISIHUSISHE wale wauzaji wa jumla na rejareja wanaonunua bidhaa ambazo tayari zimekatwa VAT badala yake wazitumie hizo mashine kwa ajili ya kuhifadhia kumbukumbu na kufanya iwe rahisi kwa TRA kupata mwenendo wa kibiashara na kufanya makadirio sahihi ya kiasi gani huyo muuzaji wa jumla na rejareja wanapaswa kulipa kama kodi (mapato) kwa TRA.

TRA; PAMOJA TUNAJENGA UCHUMI WETU
.
 
Back
Top Bottom