Mi nilichokuwa namaanisha ni kuwa hawa jamaa wa utumishi wamekuwa fair sana si kama zamani enzi za kamlete! ile ya kushikwa mkono na kupewa ofisi! Pia wameondoa ile kasumba ya kuajiri kwa kuangalia VYUO, mana mimi niliyesoma IFM kama ingekuwa ni zaman nisingepenya kwa watu wa UD hata kama uwezo ninao mara nyingine hata kuliko wao!
Tuwe wakweli jaman, watu walinasema chuo kikuu cha taifa ni UD, na watu wanaojua vitu ni wa UD. Enzi izo za nyuma kidogo ulikuwa ukiingia kwenye interview na mtu wa UD au Mzumbe jua umeshaumia! Ila nimekuja kugundua kuwa ni uongo mtupu! Nina data kamili, kwenye mitihan ya uhasibu, internal auditor, assistant lecturers, tutorial assistant, watu karibia wote wa UD na Mzumbe walikuwa wanachujwa mapema kwenye mtihan wa mchujo! CBE, IFM, TIA na AIA walikuwa wanang'aa ajabu! kudhibitisha hilo chukuen majina ya walioitwa kazini na uangalie watu utakaowajua wa UD au Mzumbe, kwa kazi zenye nature ya uhasibu!
Kumbe tulikuwa tunadhan UD ndo kila kitu na akina SENETOR walikuwa wanajigamba tu hapa kumbe ni upuuzi mtupu!
Kwa leo nimeongelea hilo, ila mkinichokonoa nitaongeza point nyingine!
Utumishi hoyeeeeeeeeee............!