Mtu akipewa ujuzi huu anaweza kujiajiri Tanzania na hata nje ya nchi kwa ufanisi sana

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,889
Wakuu ajira imekuwa shida sana na inauma kuona mtu akiteseka sababu ya kukosa ajira. Mi nilikuwa na wazo kuwa zianzishwe centre za kufundishana huu ujuzi wa kitaani tulio nao ili mtu akiienda sehemu akaufanye vizuri/ kujiajiri vizuri.

Hizi kozi ziwe fupi tu, mwezi mmoja hadi miezi mitatu. Ni kama chuo(street university) na ada ihusike.

Kuna sehemu unakuta mbaya lakini watu wa maana na magari makali wanapaki kupata huduma. Tufundishane hizo siri

Nafikiria kozi zifuatazo.

1. Kuchoma chips. Wachoma chips wengi ni kama wanakisiakisia tu. Inatakiwa kujifunza aina nzuri ya viazi, namna ya kutengeneza pilipili nzuri nk. Wenzetu wanaotumia umeme wanajua hadi kwa joto fulani viazi vinatakiwa kukaa dk fulani ili asitoe chips kavu sana au rojorojo sana. Lazima ujifunze kutoa zege zuri, lililoiva na lisiloungua nk. Ukienda Lusaka na umemaster mambo hayo vizuri lazima upige hela. Wakisema kwa fulani kuna chips nzuri basi kuwe kwako.

2. Kupika vitumbua, bagia, chapati, maandazi nk. Wote tunajua kuna sehemu wanapika chapati za ukweli na kungine wakipika za ajabuajabu. Inatakiwa tufundishane ili mtu akienda kutoa chapati iwe chapati kweli, laini, haijaungua, imeiva na ina layers. Huwezi enda Lubumbashi na kujiajiri kupika chapati na unapika chapati zimeungua na zina konakona. Ujuzi wa kupika chapati nzuri watu wanao ila hawana jinsi ya kuupitisha kwa watu wengine.

Kuna mama nilimuona kwenye gazeti anauza sana vitumbua, alipoulizwa siri akasema ni kuwa haweki mafuta mengi, sasa huu ujuzi kuwa vitumbua vinataka hiki na havitaki hiki tunatakiwa kufundishana vizuri ili mtu akitoa kitumbua kiwe kitumbua kweli. Hata akienda Kampala na kuanza biashara ya vitumbua basi a standout. Vivyo hivyo, maandazi na bagia vinaprinciple zake ili vitoke bora.

3. Kuchoma nyama/ mishikaki. Kuna sehemu unaenda unakula mishikaki mitamu na milaini. Sehemu nyingine unakuta hovyo kabisa. Tunatakiwa kufundishana ujuzi huu kuanzia kuchagua nyama , kuiandaa, moto wa kuichomea nk. Lazima tujue chachandu ya kulia nyama iweje. Huu ujuzi tunaweza kufundishana vizuri na kuutumia kujiajiri. Huwezi jiajiri na ukafanikiwa kama unachoma mishikaki migumu. Watu wakisema kwa fulani kuna bonge la mishikaki na nyama choma basi kuwe kwako.

4. Kuchoma kitimoto. Wote tunajua kuna sehemu kuna kitimoto mbaya na sehemu nyingine nzuri. Basi tufundishane huo ujuzi wa kuchoma kitimoto nzuri. Kuandaa nyama, kuchoma ndizi na kuminya!, roast, Kupika ugali fresh, chachandu nk. Mtu afundishwe principle za mambo hayo yote. Ukienda South watu wamiminike kuja kula kwako, hata mahotel makubwa yakugombanie.

5.Tufundishane kutengeneza pombe. Tufundishane namna ya kuandaa pombe za kienyeji, namna ya kufanya distillation nk. Leo mtu ukienda Msumbiji na kuanza kupika gongo basi utoe kitu cha uhakika.

6.Uuzaji wa duka. Wengi huwa tunauza maduka kimazoea bila kujua principle zake. Mtu aliyepata kozi ya mwezi mmoja ya namna ya kuendesha biashara ya duka hawezi kuwa sawa na anayeuza kimazoea.

7. Upishi wa vyakula mbalimbali. Inabidi tujifunze kupika pilau, ugali, mbalagha, biriani nk, kiprofesheno. Huwezi ajiriwa hotelini kupika pilau kama unapika kimazoea. Hata ukijiajiri kwenye mgahawa basi pilau kali iwe kwako.

8. Kutengeneza matents na stage.

9. Kutengeneza boxer, chupi, soxs nk. Ili siku hata wachina wakianza kuhamishia production africa basi tuwe tayari.

10. Kutengeneza juice kiprofesheno.

11. Kutengeneza vyombo vya udongo.

12. Kuuza counter ya bar.

13. Kutengeneza pipi, big G, biscuits, chokolate nk.

14. Honey processing.

Mi nimeandika sana kuhusu misosi. Unafikiri ni ujuzi gani mwingine wa kitaa ambao mtu anaweza kujifunza kwa muda mfupi lakini ukamsaidia kujiajiri/kuajiriwa ndani na nje ya nchi.
 
Hizo projects zinafanyika sana Kenya na ndo zinawatoa vijana mpaka kumiliki kampuni, mfano hiyo ya soksi Kuna tunamashine tunafuma soksi sasa hivi shule za private ndo zinaenda kununua huko alafu wanawauzia wazazi. Hizo projects ukiweza kuzi implement zinakutoa.
 
Kuna point kubwa sana hapo nilifika Congo kama unaweza kuanzisha mgahawa na mapishi mazuri lazima upate faida maana kwenye mapishi wako nyuma sana kule.
 
Hizo projects zinafanyika sana Kenya na ndo zinawatoa vijana mpaka kumiliki kampuni, mfano hiyo ya soksi Kuna tunamashine tunafuma soksi sasa hivi shule za private ndo zinaenda kununua huko alafu wanawauzia wazazi. Hizo projects ukiweza kuzi implement zinakutoa.
Nipe nondo hapo mkuu kuhusu upatikanaji wa mashine hizi na malighafi tufanye kautafiti tulipuke.
 
Nimepita sehemu nimekuta hawa jamaa wameanzisha hii kitu.
Screenshot_20210202-181048.png
 
Back
Top Bottom