Kwa hili, secretariet ya ajira Tanzania nimewakubali! Hongera sana!

Mi nilichokuwa namaanisha ni kuwa hawa jamaa wa utumishi wamekuwa fair sana si kama zamani enzi za kamlete! ile ya kushikwa mkono na kupewa ofisi! Pia wameondoa ile kasumba ya kuajiri kwa kuangalia VYUO, mana mimi niliyesoma IFM kama ingekuwa ni zaman nisingepenya kwa watu wa UD hata kama uwezo ninao mara nyingine hata kuliko wao!
Tuwe wakweli jaman, watu walinasema chuo kikuu cha taifa ni UD, na watu wanaojua vitu ni wa UD. Enzi izo za nyuma kidogo ulikuwa ukiingia kwenye interview na mtu wa UD au Mzumbe jua umeshaumia! Ila nimekuja kugundua kuwa ni uongo mtupu! Nina data kamili, kwenye mitihan ya uhasibu, internal auditor, assistant lecturers, tutorial assistant, watu karibia wote wa UD na Mzumbe walikuwa wanachujwa mapema kwenye mtihan wa mchujo! CBE, IFM, TIA na AIA walikuwa wanang'aa ajabu! kudhibitisha hilo chukuen majina ya walioitwa kazini na uangalie watu utakaowajua wa UD au Mzumbe, kwa kazi zenye nature ya uhasibu!
Kumbe tulikuwa tunadhan UD ndo kila kitu na akina SENETOR walikuwa wanajigamba tu hapa kumbe ni upuuzi mtupu!
Kwa leo nimeongelea hilo, ila mkinichokonoa nitaongeza point nyingine!
Utumishi hoyeeeeeeeeee............!
 
Jamani acheni kupotosha mambo,sekretarieti ya ajira iko fair sana na interview zao hazina porojo ni proffessional question only,ukiitwa kwenye interview kajibrush vya kutosha,hakuna kubebana ni uwezo 2.suala la mshahara linategemea unapoenda kufanyia kazi,kwenye government agents kama atomic commission,EPZA na vyuo mishahara ni mikubwa.ila serikali kuu na serikali za mitaa ndo level za TGS D.
 
Hongera mkuu, lakini hapo kwenye mshahara 1.8M graduate fresh from chuo ajira hzhz znazopitia utumishi!!!?
Hapo Umetuokota, labda umeiconvert kwa hela ya Zimbabwe

Hapo umenena. nadhani amepata ile nafasi ya office Manager, ubalozi wa Tanzania nchini Zimbabwe. Mke wangu ana zaidi ya miaka mitano serikalini (senior Officer), tena kwenye Agency, ndio kwanza amepata mshahara huo juzi, sembuse aliyetoka shule juzi!!! Jamani acheni uongo kwenye mitandao
 
acha mbwembwe kaka nenda uchape kazi, usingepata nafasi ungesema secretariet ya ajira hawako fair, kutaja kiwango cha mshahara wako hapa JF ni kuleta udaku tu.
 
Nadhani huyu jamaa Kikomeloallishawahi kuleta haja yake HII HAPA mwaka jana miezi kama hii, Mungu kamsikia.
Ambao hamkubahatika msiiponde tume vibaya sababu tu hukubahatika mwaka huu. kuwa mvumilivu kama ndugu huyu.

mkuu FM stereo umekata mzizi wa fitna hutawaona tena wakikoment jamaa ana kila la kupata hiyo kazi ,na kwa kuhisi ni assistant lecturer.ndio mishahara yao hiyo.
 
Last edited by a moderator:
mimi bado nazidi kuwapa heko secretariat ya ajira. Kwa jinsi wanavyofanya mambo yao hata wakidai nyongeza ya fungu la uendeshaji wa hii secretariate bungeni naomba wapewe mara moja bila kuhoji.

Taasisi nyingi za serikali haziko kama hii secretariate kiutandawazi na matumizi ya computer na internet. BIG UP!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
mh hongera lakini sisi tutajuaje kuwa hukutoa rushwa? Kama walioshindwa ndo wangesema haya maneno ningekubali lakini wewe uliyeshinda napata hofu kidgo
 
mh hongera lakini sisi tutajuaje kuwa hukutoa rushwa? Kama walioshindwa ndo wangesema haya maneno ningekubali lakini wewe uliyeshinda napata hofu kidgo

mkuu emmasa wewe umenena!.
hapo kwenye red hapo, jana kuna pepa ilifanyika, WATU WALIKUA NA MASWALI yaliyotoka kwenye pepa, halafu huyo jamaa sijui anaongea nini.
hakunaga taasisi ya serikali ambayo ni CLEAN, ngumu sana kutokea kwa Tanzania.
 
Last edited by a moderator:
Tena sio Zimbabwe ya sasa hivi,itakuwa niyakipindi kile Mgabe anapambana na nchi za wenyewe.Ila hongera na kumbuka kuwatumikia wananchi ambao wanakulipa hela hizo usije ukaanza kuwafanyia viburi kama vile njoo baadaye,kesho...........................
 
Hapo umenena. nadhani amepata ile nafasi ya office Manager, ubalozi wa Tanzania nchini Zimbabwe. Mke wangu ana zaidi ya miaka mitano serikalini (senior Officer), tena kwenye Agency, ndio kwanza amepata mshahara huo juzi, sembuse aliyetoka shule juzi!!! Jamani acheni uongo kwenye mitandao

Inategemea sehemu na sehemu, mi ndo nimeanzia! Inategemea na sector yenyewe
 
Its true jamani hata mie rafiki yangu mmoja amepata kupitia sekretarieti na hamjui mtu , analipwa 1.3 kapata atomic energy comission arusha, sekretarieti wamejitahidi kilichomsaidia HADI AKAPATA NI GPA
YAKE inawezekana mkuu pia amefaulu vizuri

Uko sawa kabisa!
 
Back
Top Bottom