Kwa hili sakata la mapacha watatu historia uenda ikajirudia.

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
56
Mwanzoni mwa miaka ya 1980 halmashauri kuu ya CCM ilitangaza vita dhidi ya wale iliowahita wahujumu uchumi. Lakini kabla ya kuanza utekelezaji wa vita hiyo ulichukuliwa uamuzi kwamba wajumbe wa halmashauri hiyo wajichunguze wao wenyewe kwanza, ili kujiridhisha ya kwamba hakuna hata mmoja wao aliyekuwa anahusika katika tuhuma hizo. Zoezi hilo la kujichunguza wao wenyewe lilikuwa limepangwa kufanyika chini ya uenyekiti wa mzee aboud Jumbe, wakati huo akiwa makamu mwenyekiti wa CCM. Hata hivyo zoezi hilo alikuweza kufanyika kwasababu marehemu Rashid Kawawa ambaye alikuwa hawe wa kwanza kujaduiliwa, ilikataa kutoka nje kwa madai ya kuwa mjadala huo unatakiwa hufanyike kwa uwazi kila mtu akiwepo, ili kutoa fursa nzuri ya kusemana vilivyo, kwakuwa kila mtu alikuwa akiyaelewa madhambi ya wenzake. Hoja hiyo ilizua mabishano makali, na iliposhindikana kufikia muafaka, suala hilo likapelekwa kwa Mwalimu ambaye hatimaye aliamua kusitisha zoezi hilo. Kwa kadri mambo yanavyoanza kujitokeza hata hili suala la kuwataka mafisadi waachie ngazi ndani ya CCM litakucha kusitishwa hivi karibuni. Hii inatokana na ukweli kwamba viongozi wengi ndani ya chama hicho wanashiriki kwenye ufisadi wa namna moja au nyingine, na hivyo haiwezekani wakachukuliwa wachache tu wakatolewa kitambo, na hali ikabakia shwari kwenye chama hicho.
 
Kwa hilo nakuunga mkono mkuu, CCM hawana ubavu wa kuwaondoa Rostam, Lowassa na Chenge. Kipindi cha Nyerere iliwezekana kuwatosa akina Kambona, Babu na wengineo kwa sababu nyerere alikuwa pure clean hivyo kuwasafisha wenzake iliwezekana. Je Kikwette ana sifa hiyo?
 
Back
Top Bottom