Consigliere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 12,037
- 24,626
Nilipata kusema wakati nachangia uzi fulani kwamba, kama rais anahitaji kupata front page basi itamlazima kufanya matukio yanayohitajika na watumiaji wa habari na hivyo kupelekea magazeti kununuliwa kwa wingi. Suala hili nililisisitiza sana, kwa kuwa ndiyo ukweli wenyewe.
Pamoja na kujinasibu kwamba yeye hashauriki wala kupangiwa cha kufanya, binafsi nimegundua kuwa rais magufuli anapokuwa katika hali ya utulivu huwa anawaza na kutafakari kwa kutumia moyo wake. Ni bahati mbaya tu kwamba mazingira yazumngukayo kwa sasa yametawaliwa na audience ichocheayo majivuno na hivyo kujikuta akifanya kile ambacho tumekuwa tukikitafsiri kama 'kukurupuka', 'udikteta' n.k.
Kitendo cha rais kutoa maagizo kwa jeshi la Polisi kumuachia msanii Ney wa Mitego ni kitendo cha kufikirisha sana, hasa kinapofanya na mtu ambaye amekua anaeleweka na kutafsirika kwa sifa nilizo zitaja. Ney wa Mitego alikua aliimba kile watu walikua wakihofia kusema, ameimba kile ambacho kinajadiliwa sana Jamii forum kwa kuwa tu kule watu wa kinga ya majina ya bandia watumiayo, ameimba kile watu wanataka kusikia. Hivyo basi kitendo cha Ney wa Mitego kukamatwa na jeshi la Polisi kiliamsha hisia kali sana na kelele kutoka kila kona ya nchi hata kwa wale ambao hawakua wakimfahamu hapo kabla.
Rais ameingilia suala hili, kitendo hicho cha kuingilia imekua ni timing na karata nzuri sana. Kwa kuwa Ney wa Miteg0 aliongea kile watu walichotaka kukisikia, na baadae akakamatwa, mpaka rais akaingilia, hakika rais anastahili front page hapo kesho.
Kukaa front page si jambo dogo, ikumbukwe kuwa kitendo cha marais wawili kukosa front page halikua jambo dogo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais Benki ya Dunia wanafanya tukio la kihistoria linalogharimu mabilioni ya shilingi lakini, sababu ya mpumbavu mmoja kutoka Koromije anapelekea rais na mgeni wake kukosa front page, maana ilibidiwanahabari wafuatilie hatma yao na hivyo front page ikachukuliwa na waziri wake wa habari (Na hiii ndiyo sababu wa Nape kutumbuliwa, wala siyo ile kamati. Yeye kama msemaje wa serikali tena akiwa ndani ya mkoa shughuli inapofanyika, alipaswa kuwepo katika shughuli ile badala ya yeye kutengeneza activity nyingine iliyoifunika shughulli ya mkubwa wake...adabu ya wapi hii!!?).
Siku nyingine nayo, rais anakwenda bandarini kwa ziara ya kustukiza, na kuibua aliyoyaibua lakini wamiliki wa front page wakamsikiliza wakaipima habari hiyo na ile ya Pale Protea ambapo Nape alikua akinyanyaswa huku akilazimika kuhutubia akiwa juu ya gari (Hili suala la Nape kunyanyaswa nalo litaondoka na mtu, maana mkuu lilimksirisha sana, kama alivyoagizwa Mwakyembe kuhusu Ney wa Mitego, katika hili nalo Waziri Mwigulu aliagizwa kulifuatilia...nawaapieni kwamba hili suala la Nape linakwenda kung'oa himaya ya Koromije), wakaona ya bandarini yanafaa kuwekwa ukarasa wa matangazo madogomadogo na front page wakamtunukia yule aliyesulubiwa akisamamia maslahi na uhuru wao. Haya yote kwa pamoja yalimsononesha sana rais na hakuweza kuficha uchungu na hisia zake.
Hili la Ney wa Mitego rais kaonyesha ukomavu wa hali ya juu sana, amelazimishwa kwenda maili moja yeye kaamua kwenda mbili, kaombwa shati yeye akagawa na joho pia. Hapa rais umefanya jambo ambalo hakika ni habari inayouzika na hili linawaacha wahariri bila ya option zaidi ya kukupa front page hapo kesho, katika hili umepuliza vizuri sana (Ingawa BASATA nao watatakiwa watufafanulie sheria zao zinasemaje katika hili).
Yapo mengi sana ambayo wananchi wapo tayari kukuunga mkono, nikushauri tu kwamba ungejiepusha na tabia ya majibizano, si jambo la busara kwa rais kuwa na tabia ya majibizano. Najua unapenda kuwa au kuonekana kuwa ni rais mwenye maamuzi na misimamo basi jifunze kutoka kwa rais Mkapa, hakika utafanya vizuri. Huwezi ukatufurahisha wote lakini angalau nchi itakua imesogea mahala fulani, kinyume na hapo ni hatua za kurudi nyuma.