Kwa hili Qatar wameupiga mwingi

Forgotten

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
3,346
10,220
Mwishoni mwa mwaka huu mashabiki wa soka watapata nafasi nyingine kushuhudia fainali za kombe la dunia zitakazofanyika nchini Qatar.

Qatar ni moja ya nchi inayopingwa vikali na mashabiki wengi wa soka duniani kwa kuwa chanzo cha vifo vya wafanyakazi wengi waliotokea nchi masikini kwenda nchini Qatar kujenga miundombinu itakayotumika kufanyia kombe la dunia.

Qatar inashutumiwa kuajiri cheap labour kutoka mataifa kama India wanaofanyishwa kazi ngumu na kupata ujira mdogo kitu kinachopelekea mamia ya wafanyakazi kufariki huku familia zao zikibaki na huzuni kwa kurudishiwa miili ya wapendwa wao waliofariki katika utafutaji.

Lakini ukiachana na yote hayo jambo moja kubwa la kuheshimiwa na kuwaunga mkono Qatar ni katika kupinga harakati za jamii ya LGBTQ (Mapenzi ya jinsia moja) kwasababu Qatar ni nchi yenye jamii kubwa ya dini ya watu wa Kiislam na kushiriki mapenzi ya jinsia moja kwao ni haram.

"Whoever lift the LGBTQ flag in the world cup, will be arrested for 7 or 11 years, we're here in an Islamic country you should respect our religion, beliefs and culture." -Qatar spokesperson

Adhabu kali itatolewa kwa yeyote yule atakayenyanyua bendera ya LGBTQ (Upinde wa mvua) anakula mvua ya miaka 7 mpaka 11.

Haya yatakuwa mashindano bora ya kombe la dunia, naamini LGBTQ ni community ya kishetani inayotakiwa kukemewa, kibaya zaidi nchi yetu ya Tanzania mwaka huu tulipeperusha bendera ya LGBTQ.

Qatar wameutendea haki Uislam pamoja na dini zote zinazopinga ushetani huu. FIFA na UEFA wanapaswa kupinga huu ushetani, wanajificha nyuma ya kivuli cha HUMANITY ila ubaguzi wa rangi pekee ndiyo movement inapaswa kupewa haki ya kuhusishwa kwenye soka.
 
hii ilinipita, ni wapi au lini Tanzania ilipeperusha bendera
20220627_105230.jpg
 
WAtu wa Dini Gani ambao kushiriki mapenzi ya jinsia moja kwao ni halali?
"Qatar ni nchi yenye jamii kubwa ya dini ya watu wa Kiislam na kushiriki mapenzi ya jinsia moja kwao ni haram."

Soma vizuri nilichoandika, mimi siyo muumini wa dini ya Kiislam najua kwao ni haram na kwenye dini yangu pia ni dhambi. Zipo dini za imani nyingi na siwezi kuzijua zote.

Kama majadiliano haya yatafikia kwenye majibizano ya udini sitachangia chochote.
 
Sio Ushoga tyuuh, hata Ngono, Ulevi pia Imekatazwa kwani hujaona? Au ushoga ndo unakutesa? Poleeeeeeh sanaaa.

Ngono, ulevi, ushoga, ni marufuku wakati wa fainali za kombe la dunia, Mashabiki wanaoenda huko kazi wanayo.

Yaani hawa jamaa wanasema kwamba watu hawatakiwi kugeggedana ata kama timu yao ya taifa imeshinda?
 
Habari ndio hiyo,
hawa hawawajui wadhungu, watu watabadilisha gear angani washangae, fasta wau wanasema ngoma ya world cup inapikwa pale wembley.
sasa wao wakati wana bid world cup walikuwa hawajui kuwa watu wa kila aina wataingia kwenye nchi yao? haya mambo ya kijinga sana. ni kutaka ugomvi na watu tuu bure. mambo ya boli na religion au siasa wapi na wapi jamani mbona wanataka kuspoil this beautiful game that has be bequeathed to us
 
hawa hawawajui wadhungu, watu watabadilisha gear angani washangae, fasta wau wanasema ngoma ya world cup inapikwa pale wembley.
sasa wao wakati wana bid world cup walikuwa hawajui kuwa watu wa kila aina wataingia kwenye nchi yao? haya mambo ya kijinga sana. ni kutaka ugomvi na watu tuu bure. mambo ya boli na religion au siasa wapi na wapi jamani mbona wanataka kuspoil this beautiful game that has be bequeathed to us
Ugomvi na mashoga? Bora wagombane tu
 
Chanzo cha taarifa yako hiyo ni kipi? Pengine labda ulimsikiliza ukamuelewa tofauti. Kwa misingi ya kikatoliki ilivyo sio jambo linaloweza kupata uhalali huo.
Dini zote zimekataa hata ukija kijamii pia tatizo ni baadhi ya watu kujifanya wanajua haki sana haswa marekani na uingereza
 
Dhambi haipingwi kwa kuweka sheria wala kumzuia mtu anayebeba mabendera tiba ya dhambi inaanzia ndani kabisa yaani moyoni mwa mtu

Hadi sasa duniani kote kuna watu wanatenda dhambi hiyo na hawajidhihirishi wazi ,Yesu alishasema

15 Hakuna kitu kilicho nje ya mtu ambacho kikimwingia chaweza kumtia unajisi, bali vile vimtokavyo, ndivyo vimtiavyo unajisi yule mtu.
Marko 7:15

21 Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati,
Marko 7:21

22 wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu.
Marko 7:22

23 Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi.
Marko 7:23

Muslims eg.mimi sehemu ya kwanza kumwona shoga alikuwa ni mwislamu na ilikuwa hapo jijini Tanga nikashangaa mno maana nilidhani hayo mambo yapo huko ng'ambo kumbe yamo katika jamii zinazotuzunguka na wengine ni mashoga na wasagaji na wana heshima zao mtaani.

Though siungi mkono ishu hii bado nadhani dhambi haishindwi na kuzuiwa mabango , tena kuna uwezekano mkubwa wa dhambi kuwa kubwa zaidi kadri unavyopambana kuizuia kwa nguvu badala yake mwache Yesu awafundishe wasipojifunza basi ni sikio la kufa.
Saudia ilikuwa inazuia wanawake kuendesha magari leo hii isharuhusu

Wafundishe wanao namna ya kujiepusha na dhambi ,nguvu za kimwili hazijawahi kuishinda dhambi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom