Kwa hili, nitasimama na Askofu Gwajima

Kwa hili, nitasimama na Askofu Gwajima

Joined
Apr 8, 2023
Posts
43
Reaction score
29
Nitasimama na Gwajima. Wakati alipojitokeza Askofu Josephat Gwajima kupinga ulazima wa chanjo ya Korona, niliandika kusema nitasimama na Gwajima na hoja zangu zilikuwa dhahiri, ingawa pia wakati alipoamua kugombea Ubunge niliandika kusema sitasimama na uamuzi wake huo na hoja zangu zilikuwa dhahiri, na kwa hili la Usalama wa nchi na watu wake, nitasimama na Gwajima.

Kuwa na akili ni jambo moja na kuitumia akili katika kufikiri na hivyo kuathiri matendo na maneno (kumbuka maneno ni mawazo yaliyosemwa na matendo ni mawazo yaliyotendwa) ni mambo mawili tofauti; kwa hili Askofu Josephat Gwajima anatuita sote kutumia akili badala ya mihemko na ushabiki wa kipumbavu tunapotafakari masuala yahusuyo taifa letu, na hiyo ni hoja aihitaji 'degree' kuielewa.

Kama dereva mwenye mafunzo, leseni na chombo kizima cha usafiri, anaacha barabara na kuingia mtaroni akihatarisha usalama wa chombo na abiria, jambo la kwanza kujiuliza au kupima ni ikiwa akili yake ilikuwa timamu katika kuendesha chombo wakati jambo hili linatokea. Ndiyo maana tutajiuliza ikiwa alikuwa amelewa aina yoyote ya kilevi, au alikuwa anazungumza na simu ama kuandika ujumbe kwenye simu, ama kwa sababu yoyote (ikiwamo kuzidia na msongo wa mawazo na kadhalika) umakini wake haukumakinika na hivyo amesababisha ajali husika. Ndivyo katika taifa ambalo watu wanashikwa kama Kuku, wanauawa kweupe, na bado Waziri anakwenda kuhudhuria msiba anafukuzwa na ndugu kiasi inabidi zitafutwe "busara" za "kulinda heshima" ya 'Mheshimiwa' ambaye jambo lisilo heshimu utu wa mtu limefanywa on his watch, halafu tunaambiwa "watu wanakufa tangu zamani, kufa ni kawaida" kana kwamba kinachoibua sintofahamu ni kufa ama kuuawa kiholela kwa Wananchi kwenye nchi yenye vyombo vya Ulinzi na usalama!!?

Wakati anapotokea mtu akahoji juu ya namna ambavyo vyombo vyetu ambavyo tuna imani navyo kwamba vimepikwa kutoka vyuo bora kabisa Afrika Mashariki na Kati (tunafahamu kwamba hapa kwetu wamefundwa mabingwa wa usalama karibia Afrika Mashariki na Kati yote kwenye vyuo vyetu wenyewe), vyombo ambavyo hatuna mashaka na weledi wake, kanuni zake za utendaji, mfumo wake wa kupata rasilimali watu, mfumo wake wa kuchagua, kufundisha na kupandisha vyeo maafisa na viongozi wake wengine, na bado yanatokea mambo ambayo hata mtoto mdogo anaweza kukwambia kuna kitu hakiko sawa, halafu yakisemwa wanaibuka watu kujivunia usomi wa "fasihi", unawaza ikiwa ni usomi huu wa fasihi unafanya wasahau kwamba hata hao waliouawa, wengine hadharani, hao waliotekwa mbele za wake na watoto wao, na hao waliopotea nao ni watoto, baba, Kaka na ndugu wa watu!!? Unawaza labda ni kwa fasihi kwamba wao ni watu 'wabaya' ndiyo maana wamekufa kwa vile "watu wema hawafi!?" Unawaza fasihi nyingi na muktadha wake, katika eneo ambalo aliyetoa mfano wa kudhurika mtoto wa mtu, katoa pia mfano wa kudhurika mtoto wake mwenyewe halafu anaulizwa ikiwa anafahamu kuhusu "kuzaa na kulea mtoto" na kadhalika, unajiuliza kuhusu fasihi ya ikiwa watoto wa baadhi yetu ni watoto na watoto wa wengine ni Kenge wa ndani!!? Unajihoji mengi kuhusu fasihi na majibu hayapatikani!!?

Kwanini tumevuka Sasa hata kiwango cha yule Kadhi dhalimu ambaye hata yeye nafsi yake ilifahamu na akakiri kwamba "...simchi Mungu na sijali watu..., lakini nitampa mama huyu Haki yake...." (Luka 18:4-5) na hivyo tumebakia kuzungumza Amani na tumeamua kuipata 'amani' kwa njia ya vitisho na hofu badala ya njia ya HAKI na bado tunaamini kwamba wananchi wa Tanzania ni wapumbavu kiasi cha kuendelea kutuamini na kutuona sisi ni viongozi wastahivu kwao!!?.

Kwa hili, kila mwananchi mwenye akili njema, kila mtu anayeipenda nchi yetu kwa dhati badala ya kujipenda yeye na dynasty yake, kila anayelitumikia taifa letu siyo tu kwa mshahara bali kwa kujenga kesho ya watoto wake na watoto wao baada yao kwa vizazi vingi, kila aliyeapa kwa dhati kuitetea na kuilinda Katiba ya Tanzania, ni wakati wake aonyeshe Uzalendo wake kwa kutekeleza wajibu wake huo wa kiutu, na kikatiba kuhakikisha kwamba Tanzania haigeuki taifa ambalo uovu ni wema na wema ni uovu.

Anasema Mwanazuoni Al Ragheb Al Asfahaniy kusema: “Uovu ni kila kitendo ambacho akili sahihi zinaweza kutoa hukumu ya kubainisha ubaya wake, au akili zikiacha kukijali, sheria inatoa hukumu ya kubainisha ubaya wake” na ameamrusha Mtume Muhammad (SAW) kusema ". Yeyote miongoni mwenu atayeona jambo ovu na baya basi aliondoshe kwa mkono wake, ikiwa hawezi kuliondoa kwa mkono wake basi aliondoe kwa ulimi wake, na ikiwa hawezi kuliondoa kwa ulimi basi na alichukie kutoka moyoni mwake, na kuchukia moyoni ni udhaifu wa imani ",

Askofu Gwajima amekataa "udhaifu wa imani". Udhaifu wa imani ya kuamini katika Tanzania ya Amani, Tanzania ambayo Mwalimu Julius Kambarage Nyerere anasema "Watu wanataka kulala majumbani mwao wakijua kwamba wanatawaliwa na kulindwa na sheria....", Tanzania ambayo Siasa, Mamlaka, "Kokasi" za vyama na kadhalika haziwezi kuwa juu ya maisha na uhai wa Watanzania wenyewe. Kama hatuwezi kuuona uovu katika watu wetu kuuawa na wataalamu wetu kutochukua hatua, basi siyo tu tumeshindwa kuuondoa uovu, lakini tumekuwa vipofu hata hatuoni uovu katika kumwaga damu za watu wasio na hatia ya kumwagwa damu zao na hilo ni ovu zaidi, na Gwajima amekataa kushiriki ovu hilo na sisi wengine wote wenye kuipenda Tanzania, hatuna budi kusimama na Gwajima kwenye hili.
 
Mfumo wa kutengeneza machawa ndio uliothiri vyombo vya utendaji na kuzalisha wajinga ambao hawachukuliwi hatua kwani kuanzia 2015 Kuna vitu vilianza kutoka na tukachukulia kawaida lakini Leo tunaona madhara yake kwa umama ambao hauna sauti .lazima tupambanie na tuungane na wote wanaopiga kelelle na hatua zochukulowe kwa isiyo mkubwa kwa kuunda kamati huru ili ije na majibu .
 
Wapo watu wanaona shida ipo ila wakitoka hadharani kwa maslahi ya matumbo yao wanajiweka upande wa tatizo.
 
Back
Top Bottom