Kwa hili Namuunga mkono rais kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa hili Namuunga mkono rais kikwete

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Magezi, Aug 4, 2009.

 1. M

  Magezi JF-Expert Member

  #1
  Aug 4, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kikwete ashauri Watanzania kununua matrekta badala magari ya anasa

  Na Mwandishi Wetu

  RAIS Jakaya Kikwete ametaja anasa za Watanzania kuwa moja ya mambo yanayofanya sekta ya kilimo kushindwa kufikia malengo ya kuwa uti wa mgongo kwa uchumi wa Tanzania.

  Akizungumza katika uzinduzi wa maonyesho ya Nanenane katika viwanja vya Nzuguni nje kidogo ya mji wa Dodoma jana, Rais Kikwete alisema baadhi ya Watanzania wanapenda zaidi kununua magari ya kifahari badala ya matrekta kwa ajili ya kilimo.

  Rais Kikwete alitaja sababu zingine zinazofanya kilimo kisifanikiwe kuwa ni pamoja na ukosefu wa wataalamu wa kufanya utafiti katika sekta ya kilimo
  "Watafiti wengi wanaamini kuwa mbegu nzuri ya kupandwa ni ile iliyozalishwa katika maeneo husika sio ya kuagiza kutoka nje, sasa sisi tunaagiza nje asilimia 75 ya mbegu bora zote tunazopanda hapa nchini hiyo ni hatari kwetu" alisema Kikwete.

  Katika maonyesho hayo ambayo kaulimbiu yake ni ‘Kilimo kwanza'Mapinduzi ya kijana uhakika wa chakula na kipato,rais alisema haiwezekani kukosa chakula kila mwaka kana kwamba Watanzania wamelaaniwa.
  Alisema kila mwaka Tanzania imekuwa ikikosa chakula wakati ardhi ya kutosha ipo pamoja na baadhi ya maeneo kuwa na mvua za uhakika kitu ambacho ni ndoto katika maeneo ya nchi nyingine duniani lakini bado wanazalisha chakula cha kutosha.

  Hata hivyo aliponda kwa Watanzania kuendelea kutumia jembe la mkono na akasema kuwa hicho ni kikwazo kingine cha kuwafanya waendelee kubaki katika hali ya umasikini mkubwa ambao utaendelea kuisumbua nchi.
  Pamoja na kusema kuwa kilimo cha jembe la mkono kimepitwa na wakati, aliwaacha hoi wakulima pale aliposema kuwa hata kilimo cha jembe la kukokotwa na ng'ombe ni cha zaidi ya miaka 2000 iliyopita.

  "Sisi tunahimiza kilimo cha jembe la kukokotwa na wanyama huku tukisahahu kuwa kilimo hicho kilikuwepo tangu hata kabla ya Yesu Kristo kuzaliwa ambayo ni zaidi ya miaka 2000 iliyopita, lakini sisi ndio kwanza tunaanza"

  Katika hatua nyingine rais Kikwete amesema Benki ya Wakulima nchini itaanzishwa kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya China na tajiri maarufu wa Kimarekani Bill Gates.

  Rais Kikwete alisema, mkakati huo umekuja kutoka na ukosefu wa vyombo vya fedha vya uhakika vya kutoa mitaji kwa wakulima hapa nchini.
  Kikwete alisema serikali imeamua kuchukua hatua hiyo kwa kuwa ukosefu wa mitaji kwa wakulima umekuwa ni kikwazo kikubwa kinarudisha nyuma maendeleo ya kilimo nchini.

  Aliongeza kuwa wakulima wengi hawana uwezo wa kununua matrekta kutokana na kuuzwa kwa bei ya juu pamoja na serikali kuondoa kodi kwenye nyenzo hiyo ya kilimo.

  "Serikali iligundua uwezo mdogo wa wakulima kununua matreka.Pamoja na kuondoa kodi katika matrekta ili kuwasaidia wakulima lakini bei bado iko juu" alisema Rais Kikwete.

  Source: Mwananchi 4/8/2009

  Kwa hili namuunga mkono Rais. Ni kweli waTZ tumeendekeza sana kununua vigari vya anasa visivyo zalisha na wakati huo huo tunalalama maisha magumu.
   
 2. M

  Magezi JF-Expert Member

  #2
  Aug 4, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  kumbe kweli........mtanzania hapendi kuambiwa ukweli
   
 3. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #3
  Aug 4, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Huo ukweli angeanza kuutekeleza yeye. Angepunguza safari zisizo na tija na hizo pesa zinunue matreka yawekwe Mwanza, Moshi, Arusha, Moro, Mbeya, Iringa, Rukwa na Ruvuma uone kama hajakaa wiki moja na kununuliwa yote.

  Hiyo ni demagogue politics ambayo ni trick ya zamani sana, unawaambia watu wasifanye ambacho wewe unafanya sijui maana yake nini. Yeye mwenye anauwezi mkubwa wa kununua hayo matrekta sijui amenunua mangapi. Na sijui kama kuna hata moja huko Chalinze au bagamayo. Mkuu anatakiwa aoneshe mfano yeye.
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Aug 4, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hivi yale ma BMW anayotumia katika msafara wake ni ya bei rahisi au?sijamuelewa anamaanisha mtanzania/watanzania wepi wanaopenda anasa
   
 5. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #5
  Aug 4, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Nadhani Rais wetu alikwa anazungumza siasa zaidi kuliko ukweli. Ukweli ni kwamba sio kila mtu anaweza kuwa mkulima. Kulima ni proffesion kama zilivyo proffesion zingine. Unaweza ukawa na pesa lakini kama hukujaliwa kuwa na karama ya kuwa mkulima ikiwemo na ufugaji basi kilimo kitakushinda. Sasa mtu ukiwa na pesa yako kutokana na karama yako nyingine kwa nini ununue tractor ambalo hutalitumia ipasavyo Sio kila mlowezi (wazungu) wa Zimbabwe alikuwa mkulima. In fact wakulima walikuwa wachache lakini nchi ilizalisha kweli kweli. Kinachotakiwa ni kuwa na sera nzuri za kilimo wajasiriamali wenye wito wa kulima watanunua hayo matrekta watazalisha. Wengine wachimba madini na kununua magari ya kifahari. Ce la vie!
   
 6. M

  Magezi JF-Expert Member

  #6
  Aug 4, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  labda na yeye ni miongoni mwa wapenda anasa kwa sababu hakueleza bayana.
   
 7. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #7
  Aug 4, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kilimo kimekuwa uti wa mgongo wa tanzania toka uhuru. Sijui kama kampeni hiyo ya kilimo kwanza itafanikiwa. kwani nyuma kulishakuwa na azimio la kilimo. nalo likafa.

  Kwa Tanzania, ufisadi kwanza ili ue tajiri
   
 8. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #8
  Aug 4, 2009
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,276
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  lakini ukweli uko pale pale kuwa hivi ni asilimia ngapi ya watz tunaheshimu kilimo? wengi tunafikiria kufanya biashara ndogondogo ambazo ni rahisi za kuuza vitu ready made kutoka china.

  tuna manpower kubwa lakini ipo under utilized. kuna vijana huko barabarani ana kifuko kimoja cha apples, mwingine ana sabuni 2 za kuogea na wengi wapo tu wanazunguka zunguka kuibia watu. hivi kweli tunatarajia miujiza kwamba kuna Rais atatokea abadilishe haya mazingira kirahisi?
  LETS THINK TWICE
  nafikiri changes/atitude zibadilike kwa pande zote watu &serikali
   
 9. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #9
  Aug 4, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ataiuza na hiyo LIMUSON lake kama la Obama vile atayauza mana yako mengi kweli yameandikwa STATECAR
   
 10. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #10
  Aug 4, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Rais wetu kweli kaongea kitu cha maana, lakini angeanza yeye. Apunguze mawaziri wasio na tija, awe na baraza la mawaziri dogo lenye watu makini 8 (yaani kuwe na wizara nane) tu bila manaibu. Serikali iache kuagiza mashangingi, serikali ianze kuagiza mtrekta mengi na kuyakodisha kwa wananchi kwa bei nafuu.

  Serikali ihakikishe inatoa ushauri wa kitaalamu kwa wakulima na kutafuta soko la kimataifa kwa bidhaa za wakulima. Juzi roho iliniuma sana nimeenza supermarket nikakuta njegere mbichi kutoka Kenya robo kilo karibu shs 2500 za Tanzania wakati bongo tuna njegere tena zenye ubora zaidi ya hizi nilizonunua za Kenya. Serikali ingekuwa makini kwanza katika kutafuta masoko ya kimataifa ya bidhaa za Kilimo halafu ione kama hata hilo tamko la kununua matrekta kama atatoa tena, watu wenyewe watanunua.
   
 11. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #11
  Aug 5, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Kikwete mpaka sasa hajui maana ya kuongoza; nyie washauri wake mwambieni arejee hotuba za hayati mwalimu atajifunza mengi ya maana ya uongozi! Kiongozi anatakiwa awe mfano kwa watu anawaongoza; anatakiwa kuonesha njia na watu anaowaongoza wamkubali na wamfuate. Kama anasema watanzania wanapenda anasa ajue wanamuiga yeye na MABW anayopanda nao wanaleta hayo hayo; enzi za mwalimu hakukuwa na magari ya anasa kama yalivyosheheni sasa, ingawa idadi ya wanaoishi below the poverty line ni wengi zaidi sasa kuliko ilivyokuwa enzi za mwalimu!!
   
 12. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #12
  Aug 5, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Serikali ni lazima iongoze mabadiloko ya nchi, watu watafuata. Kama viongozi wa dola wana vision si vigumu kuibadilisha Tanzania. Miaka mitano tu inatosha sana, tatizo liko kwenye uongozi serikali haiwezi kukwepa wajibu wake.
   
 13. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #13
  Aug 5, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naona kama katimiza wajibu na bado maana hata hiyo kilimo kwanza niya kisiasa angalia budget ndg ndio utajua wanasiasa huwa wanasema zaidi kuliko kutenda; hakuna kitu kibaya kama kuwa na serikali yenye mikampeni kibao ya uongo uongo
   
Loading...