moghasa
JF-Expert Member
- May 7, 2013
- 1,084
- 1,253
Wanajamvi umofia kwenu!!
Napenda kuipongeza serikali kwa michakato yote ambayo wanaendelea nayo na niwapongeze zaidi kwa kuwa ni viongozi wachache lakini wanaongoza wadanganyika zaidi ya milioni 45, akiwemo Deogratius Kisandu, unaweza kujenga picha mwenyewe.
Mimi ni mwalimu, yes, English teacher ( not from England bt from Rorya teaching english as a subject). Napenda kuonesha masikitiko yangu waziwazi dhidi ya serikali yetu pendeka baada ya kutoa tamko kuwa hii Arts hawatapewa ajira, wakiwemo waalimu wa kiingereza.
Kwanini nalalamika, ?
Ndugu zangu na walimu wenzangu hasa wale wanaofundisha hii lugha ya Malkia watakuwa wanaelewa, Mashuleni kuna uhaba mkubwa sana wa walimu wa kiingereza, hii hutokana na watu wengi ( wanavyuo) kutopendelea kusoma hili somo kwasababu kadha wa kadha ikiwemo na idadi kubwa ya vipindi, pamoja na ugeni wa lugha yenyewe.
Utakuta kwa mfano shule ninayofundisha ina wanafunzi 630 lakini walimu wa somo hilo ni watatu tu!! Tunabaki tu kufundisha bora liende tena bila ufanisi kwa sababu ya mzigo wa vipindi tulionao.
Nizidi kuiomba serikali, kutoa tamko jingine kuhusu walimu wa kiingereza sioni kama ni kazi ngumu.
Kabla ya kuhamia katika matumizi ya kiswahili katika ngazi zote za kufundishia, basi tujitahidi kwanza kuboresha mazingira ya kiingereza huku mashuleni. Tofauti na hapo PhD mtakuwa Nazo na kiingereza mtakuwa hamjui
Najuwa serikali yangu in sikivu sina wasiwasi na hili.