Mchokoo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2015
- 1,179
- 1,579
1) Wasitoe matamshi mengi ya kuufariji uma, bali waupishe muda uitafsiri hali hii, ili baadaye wasijekujiingiza katika jaribu la kurekebisha yale yasiyorekebishika, kwa kusudi la kutoonekana waongo kwa wananchi.
2) Wasijiingize kwenye propaganda zinazosambazwa na makasuku wa kisiasa, ambao baada ya kuona wadau wa maendeleo wanajitenga nasi kwa sababu walizozibainisha wazi kwetu; eti ndipo mahubiri ya kujitegemea kwa watu hawa kiuchumi yanapoanzia!
3) Ni vizuri tukatafakari kuwa kuna mahali fulani hatuko sawa. Na kwa sababu hiyo ni uungwana kurekebisha mapungufu yetu. Na kama taifa lililojinasibu kwa muda mrefu kuwa la watetea haki za binadamu tumevuliwa nguo; na aibu utupu wetu imeonekana!
Hivyo basi badala ya kupiga makelele huku tuiwa hatuna nguo; Ni salama zaidi kwetu kuchutama ikiwa bado tunazo akili timamu, kwa maana ya kuyajenga yale yaliyobomoka.
Wewe unasemaje?
Toa maoni yako! kumbuka kuendeleza mtiririko wa namba.