Hakuna jipya wala la ajabu kiasi cha kusema eti utawala awamu ya Tano uliyabariki hayo
Alipoingia Kikwete madarakani aliwafungulia mashtaka Basil Mramba na Daniel Yona ambao walihudumu ktk nyadhifa za uwaziri awamu ya Mkapa, na walikutwa na hatia
Alipoingia Magufuli viongozi kadhaa wa Serikali na Taasisi zake wa awamu ya Kikwete walifunguliwa mashtaka kama Mwaimu wa Nida, Mchechu Nhc, Malinzi TFF etc.
Na sasa Mamá yupo Ikulu si ajabu kuona baadhi ya watendaji wa awamu ya Magufuli wakipandishwa kizimbani.
Na hakuna tawala iliyopigiwa kelele za wizi, ufisadi, rushwa, uhujumu uchumi na ukwepaji kodi kama tawala ya Kikwete. Na kama Magufuli angesema adili nao nado to nado basi nakuhakikishia zaidi ya 60% ya watendaji wakuu wa taasisi za Serikali wangefikishwa kizimbani, ila ndio hvyo Magu aliona wengine inatosha kuwatumbua tu.
Fikiria scandal za Escrow, mradi wa majengo pacha ya BOT, EPA, Richmond, Chenji ya Radar, mishahara ya watumishi hewa etc zilivyoichachafya Serikali ya JK.