Kwa hili la nguo za mitumba Serikali mmekurupuka

Figoo

Member
May 7, 2016
80
49
Hata kama tunahitaji kuongeza mapato kupitia kodi, kitendo cha serikali katili ya CCM kuongeza kodi kwa nguo za mitumba bila kuwa na viwanda vya kutengeneza nguo ni jipu.

Ikumbukwe 98% ya watanzania tunavaa mitumba ndo kimbilio la masikini na sii wote tunaweza kununua mitumba.

Huko vijijini hali ni mbaya watu wanashona viraka leo hii mitumba inapanda tutegemee watu kutembea nusu utupu.Ni vema serikali muwe na huruma na masikini wavijijini mnakurupuka mno mnaongeza chuki na raia.
 
Maendeleo yanatutaka kuvaa nguo mpya. Watanzania hatupaswi kuendelea kuvaa mitumba. Zungumza mipango ya kazi, masoko ya mazao na mfumo wa mapato kuhakikishia Watanzania uwezo wa kununua nguo mpya. Tunasonga mbele.
 
Sasa kama walipitisha sheria mafao ya wastaafu kwenye mifuko ya jamii ikatwe kodi ila ya kwao hawatiki unategemea mna wawakilishi au tuna wachumia tumbo zao? Halafu ati huruhusiwi kutoa hela yako hadi uwe na miaka 55 lakini wao wakimaliza tu term ya miaka mitano hata kama una miaka 20 unashika mwanja wako. Hizi ni sheria za upande mmoja. Tunatakiwa nasi tuwaulize wabunge walitumwa nini bungeni
 
Hata kama tunahitaji kuongeza mapato kupitia kodi, kitendo cha serikali katili ya CCM kuongeza kodi kwa nguo za mitumba bila kuwa na viwanda vya kutengeneza nguo ni jipu.

Ikumbukwe 98% ya watanzania tunavaa mitumba ndo kimbilio la masikini na sii wote tunaweza kununua mitumba.

Huko vijijini hali ni mbaya watu wanashona viraka leo hii mitumba inapanda tutegemee watu kutembea nusu utupu.Ni vema serikali muwe na huruma na masikini wavijijini mnakurupuka mno mnaongeza chuki na raia.
Ebu eleza kwa kina ni wapi huko vijijini ambako wanashindwa kununua nguo za mitumba. Ikiwezekana weka picha. Umasikini wao unatokana na nini? Tuanzie hapo kwanza.
 
Back
Top Bottom