Kilemakyaaro
JF-Expert Member
- Jul 19, 2016
- 5,051
- 5,094
Habari zenu wanajamvi, leo ninajitokeza kusema kwa kifupi sana juu ya magazeti ya michezo hapa nchini. Ni jana tu vijana wetu wa timu ya Taifa ya Serengeti Boys walishinda 2-1 dhidi ya Angola, kusema kweli ni furaha sana maana nna uhakika kwa miaka ya karibuni hatuna timu iliyobeba nembo ya Taifa letu iliyowahi kuongoza kundi ktk michezo. Sasa jambo lakusikitisha sana eti leo vichwa vya habari vya magazeti ya michezo vimeandika habari za Yanga na kuipotezea au kuiandika kwa vimaandishi vidogo habar ya vijana wetu. Sina maana nna ogomvi au kuichukia Yanga ila kwakweli kwangu mimi habari ya hawa vijana ingekua namba moja...Au labda iwe hawa wenye magazeti siyo Watanzania au ni Watz lkn siyo Wazalendo. Nihitimishe kwakuwaasa tu kuwa mapenzi mema kwa nchi hii ni muhimu maana hakuna pengine patakapokufanya ujivune zaidi ya hapa ulipozaliwa...Mungu ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Serengeti boys.