Kwa hili la maduka ya dawa, TFDA mnatakiwa kwenda zaidi ya hapo. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa hili la maduka ya dawa, TFDA mnatakiwa kwenda zaidi ya hapo.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mrimi, Mar 22, 2012.

 1. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Wizara ya Afya kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa, wanaendelea na zoezi la ukaguzi wa maduka yanayouza dawa za binadamu nchi nzima. Tumeona juzi maduka kadhaa yakifungwa kufuatia kuendeshwa bila kufuata utaratibu, kama vile kuendeshwa na watu wasiokuwa na taaluma ya mambo ya dawa.

  Mimi naipongeza serikali ktk hili, ila hii hainifanyi kusahau mapungungufu kadhaa yaliyopo ambayo ni hatari kwa afya zetu. Ikumbukwe kuwa kwa sasa kuna zoezi linaloendeshwa nchini la kuwapa mafunzo maalum wamiliki na wauzaji wa dawa za binadamu. Huu ni mpango unaopelekea kubadilishwa kutoka maduka ya dawa baridi kuwa maduka ya dawa muhimu.

  Tatizo ninaloona hapa ni, je, kweli serikali(wizara ya afya) inafahamu huduma zinazotolewa ktk maduka haya? Je, serikali inatambua wamiliki na wauzaji ktk maduka haya uwezo wao ktk huduma hii? Ninachoelewa ni kwamba serikali inajua kiwango cha elimu kinachofaa ktk kuendesha huduma hii. Sasa ktk zoezi hili la kutoa elimu kwa kwa wamiliki wa maduka haya, inaeleweka kwamba mafunzo haya hutolewa kwa muda mfupi sana(6-8weeks). Kwa tafsiri nyepesi ni kwamba ufamasia/udaktari unafundishwa kwa muda wa wiki 6! Ni nani asiyejua kuwa wauzaji(wanaopata mafunzo) wengi wao ni wale wenye mafunzo ya Red Cross na nurse assistance(ambao nao wengine wamesoma vyuo bubu!)

  Kiukweli mafunzo yanayotolewa ni kuwawezesha wauzaji na wamiliki kujua aina za dawa kwa mfano antibiotics, antipains, antiworms nk. Wanafundishwa pia kusoma prescriptions(mwandiko wa daktari!) na mambo megine madogo madogo. Nina hakika 100% hawafundishwi kutambua(diagnosis) ugonjwa wa mteja wake(client).Sasa kinachofanyika ni kwamba mtu anapatiwa mafunzo hayo ya wiki 6, kisha anapewa kibali cha kuendesha huduma hii.

  Hebu turudi ktk uhalisia jamani, haihitaji rocket science kujua kuwa wananchi wengi wanapoenda ktk haya maduka, hufika na kuelezea matatizo yao kwa muhudumu(huyu aliyepata mafunzo ya wiki 6!). Wanachi wengi huamini kuwa hawa wauzaji ni madaktari na kwamba wana uwezo wa kuwatibu kwa usahihi kabisa. Swali langu, je, serikali imeridhika wananchi wake tutibiwe na hawa madaktari na wafamasia wa wiki 6? Jirani yangu ni fundi umeme mwajiriwa wa TANESCO anamiliki duka kubwa la dawa ambalo linaendeshwa na binti yake ambaye ni form IV failure, alipata cheti cha red cross kwa njia anazofahamu mwenyewe(maana sikuwahi kumwona akipata mafunzo hayo). Hivi karibuni alipata mafuzo hayo ya wiki 6 na sasa anatibu watu kwa roho nyeupe kabisa!


  Kwa mtazamo wangu, kutupatia madaktari na wafamasia wa wiki 6, serikali inatakiwa kwenda mbali zaidi ya hapo. Hawa watu watatuua. Taaluma ya kutibu watu si kitu cha mzaha. Si kila mtu anaweza kutibu jamani. Haya maduka yanatibu watu, kinyume na makusudio yake. Maduka haya yapo ili kutoa dawa kwa kufuata mwongozo wa madaktari.
  Serikali inatakiwa kujiridhisha kabisa kwamba huduma hii inatolewa kwa kufuata masharti ya leseni.Wajaribu kufanya follow up kila mara ili kuhakikisha kwamba huduma inayotolewa ktk maduka haya inaendana na makusudio yake na si vinginevyo.

  Wamiliki wawe profesionals na kama sivyo basi huduma hii itolewa under supervision of profesionals. Haiingi akilini kukuta muhudumu ni mwanafunzi wa kidato cha pili anayetoa huduma tena kwa kujiamini kabisa.
  Lakini na sisi wananchi ufike wakati tuzijali afya zetu. Tutambue kwamba si kila mtu anaweza kutibu. Hebu tuwe tunajiridisha kwanza na uwezo wa mtoa huduma kabla ya kumkabidhi afya zetu.

  Nawasilisha...
   
Loading...