The Businessman
JF-Expert Member
- Jan 9, 2014
- 7,396
- 9,264
Post deleted by author!
Mnawasingizia americans . Jina Ebola ni la Kizaire yaani mto (river) mgonjwa wa kwanza alitokea eneo la mto huko zaire ndio wakaita ugonjwa wa ebola.
Ni Ukweli Ambao Unafahamika Na Wengi Kuwa Waafrika Hawatakiwi Hapa Duniani,na Zinafanyika Juhudi Za Kila Namna Ili Kuwapunguza Waafrika. Yanatengenezwa Magonjwa Ya Ajabuajabu Yenye Kuua Polepole Na Haraka Mfano Ni UKIMWI NA EBOLA.
Wabaguzi Wa Rangi Wazungu Ktk Juhudi Zao Za Kuhakikisha Wanaaminisha Jamii Ya Kimataifa Kuwa Chimbuko La EBOLA NI AFRIKA. Walifanikiwa Kupandikiza Kirusi Cha Ebola Kwa Baadhi Ya Kima Huko Afrika Ya Kati. Na Kama Kawaida Ya Wenyeji Walipowinda Na Kula Hao Kima Na Wao Waliambukizwa EBOLA, Ugonjwa Huu Ulikuwa Wa Ajabu Na Hadi Hapo Haukujulikana Kabisa Ktk Eneo Lile Na Duniani Kwa Ujumla.
Lakini Jambo La Kushangaza Watu Wa Kwanza Kuutambua Ugonjwa Huo Na Hata Kuupa Jina EBOLA Walikuwa Ni Madaktari Wa Kizungu. Ilikuwaje Waufahamu Ugonjwa Ambao Ulikuwa Asili Wa Eneo La Afrika? Ilikuwaje Wakakipa Jina Kirusi Hicho Kwa Haraka Kiasi Kile Kama Hawakuwa Na Ufahamu Wa Jambo Hilo Kabla? NI WAZI WALIKUWA WANAELEWA KINACHOENDELEA. EBOLA NI UGONJWA ULIOTENGENEZWA MAABARA KWA MAKUSUDI.
Nliwahi sikia kuwa unatokana na tabia ya kula mizoga sijuhi ya nyani...sina hakika...kuna ajuaye hili...maana watu wa central na west Afrika wanakula vitu vingi kama wachina...
na kula popo piaNliwahi sikia kuwa unatokana na tabia ya kula mizoga sijuhi ya nyani...sina hakika...kuna ajuaye hili...maana watu wa central na west Afrika wanakula vitu vingi kama wachina...
Wanajamvi
Sisi tumezoea kuishi kwa hisia iwe za kichawi au kusingizia.
Leo ni miaka 100 tokea mfereji wa Panama Canal ulipofunguliwa. Tembelea uzi wa simplemind kusoma kwa uchache tu.
Mradi ule ulianza miaka 1889 na ukafeli kwa mara ya kwanza. Watu 22,000 walikufa kutokana na Malari na Yellow fever
Miaka 15 baadaye Marekani walianza kuangalia sababu za vifo na kumtuma Daktari kwanza kwenda kuangalia namna ya
kupambana na maradhi. Mwaka 1906Yellow fever ilikuwa karibia imefutwa Panama, na malaria yalipungua sana.
Hii ni kutokana na dawa za kupulizia kuua mbu, kusafisha mazingira na kujua malaria na maradhi hayo kwa undani.
Leo miaka 108 tangu Wamarekani wafanikiwe kule Panama, sisi Waafrika tunauana kwasababu huyu ni dini fulani.
Waafrika bado hatujui kuwa net zinazuia mbu, na wala hatuna habari ya matumizi ya vyoo.
Viongozi wetu wamebeba matumbo kama ndoo za maji kwasababu ya kubugia. Kodi wanaelekeza kujenga mahekalu badala ya kufanya utafiti.
Ebola ilikuwepo, wenzetu wakaelekeza nguvu na pesa zao kutafiti. Wazungu wakiona tatizo wanalifanyia kazi.
Leo tunawalaumu kwa maarifa yao.
Hivi wewe hushangai kuwa Marekani hakuna kipindu pindu lakini dawa zinatoka huko.
Uingereza hakuna kuhara damu lakini dawa zote nzuri zinatoka huko
Laiti mngekuwa mumetembea na kuona wenzetu wanatumia vipi maarifa kufikia maendeleo msingekuwa na hisia hizo.
Leo badala ya kupeleka pesa kwenye utafiti, Samwel Sitta anaalika wafugaji ili akidhi haja yake.
Samwel Sitta hasikii maoni ya wataalamu, kaweka mbele mshahara wa bunge la katiba unaosema ni ''milioni 150 kwa siku 84''
Msiwasingizie Wamarekani na wazungu, wenzetu wanawekeza katika maarifa sisi tunawekeza katika ujinga.
Hakuna lolote baya, kama jina ebola wametoa wao, vipi leo George bush aje kugawa vyandarua kwa nchi iliyopata uhuru miaka 50 iliyopita? Kama hauwezi kusafisha mitaro mwaka 2014 akili ya kugundua dawa ipo wapi.