Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
Wiki mbili zilizopita katika maadhimisho ya Wiki ya Sheria, Rais John Pombe Magufuli alisisitiza kuwa serikali imejipanga kuanzisha mahakama ya kushughulikia mafisadi na watu wanaohujumu uchumi wa nchi.
Hii ni kauli au ahadi aliyoitoa wakati wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu uliomuweka madarakani mwaka 2015 na kila mara anapopata wasaa amekuwa akiirudia kusisitiza msimamo wa serikali yake katika kukabiliana na wimbi la wala rushwa na mafisadi.
Lakini haukupita hata mwezi mmoja mawaziri wawili katika awamu ya tatu waliofungwa jela kwa kuisababisha hasara serikali ya Shs. 11 bilioni na matumizi mabaya ya madaraka Basil Mramba na Daniel Yona, wakapunguziwa adhabu kwa kutakiwa kutumikia kifungo cha nje, jambo ambalo Watanzania wengi wamelitafsiri kama mzaha uliofanyika mbele ya Rais na wananchi ambao wako makini wakitaka waone kazi.
...ENDELEA