Sijui kama umefanya utafiti wa kutosha juu ya uliyoyaandika. Lakini jinsi ninavyojua juu ya kustaafu kwa wachungaji wa KKKT ni kama formalities lakini kwa hakika wanakuwa bado wapo katika huduma hata mavazi ya kichungaji huwa wanazikwa nayo.Mfano ninaye baba yangu mdogo amestaafu toka 1999 lakini toka wakati huwo amekuwa akipelekwa na kanisa kuhudumia sehemu mbalimbali kama mchungaji wa usharika na hata akirudi kijijini kwetu bado anaendelea kutoa huduma za kiroho.Na amewahi sema toka astaafu ndio wakati ambao amekuwa na kazi nyingi za kanisa kuliko wakati mwingine wa utumishi wake. Na hata sasa hayupo kijijini kwetu kapangiwa usharika anaendelea kuhudumia. Hivyo ndivyo itakuwa hata kwa mchungaji Mwaisapile kwani wote wapo KKKT na si kama unavyotaka watu waamini vinginevyo.Ingawa si msemaji wa KKKT wala Mwaisapile lakini kama muumini nimetimiza wajibu wangu.Kwani neno linasema mavuno ni mengi lakini watendakazi ni wachche...Ndio maana hawa wazee wanaendelea kutumika.
wewe unaonekana huna taarifa, tomas laiza alipokua anamrudisha kwenye huduma alisema anachofanya mwasapile ni zaidi hata ya uchungaji so kwa kuzingatia huduma anayoitoa tunamrudisha kwenye utumishi na tutampa ushirikiano which means atapewa mshahara na huduma zingine za kitumishi. Sasa wewe ulitaka arudishwe lini?
sijawaelewa KKKT kwa kuunga mkono huduma hii hadi watakapotueleza vizuri sababu za kuamini ufunuo kama huu bila kuujaribu kama umetoka kwa Mungu. kama wameoishaujaribu na kujiridhisha, kwa nini wasifundishe makanisani na kutoa elimu kwa watu wote? si ndio maana ya injili na wito walioitiwa?
hayo ya kutoa ushirikiano na eti anafanya zaidi ya wachungaji kwa kweli kauli kama hizi zinasikitisha sana zinapotolewa na watumishi wa Mungu.
Mungu atainuliwa daima katika nchi na miisho ya dunia itauona utukufu wake
utukufu una yeye hata milele na milele
Kitu kinachotoka kwa Mungu hakina majaribio. Nuhu alipoambiwa ajenge lile safina kuna watu walimwona chizi, mpaka maji ya mvua yalipowafika kifuani wakaanza kumpigia kelele awafungulie. It was too late.sijawaelewa KKKT kwa kuunga mkono huduma hii hadi watakapotueleza vizuri sababu za kuamini ufunuo kama huu bila kuujaribu kama umetoka kwa Mungu. kama wameoishaujaribu na kujiridhisha, kwa nini wasifundishe makanisani na kutoa elimu kwa watu wote? si ndio maana ya injili na wito walioitiwa?
hayo ya kutoa ushirikiano na eti anafanya zaidi ya wachungaji kwa kweli kauli kama hizi zinasikitisha sana zinapotolewa na watumishi wa Mungu.
Mungu atainuliwa daima katika nchi na miisho ya dunia itauona utukufu wake
utukufu una yeye hata milele na milele
Naomba nijuzwe...
Nimeelezwa na kuwa kwa kawaida wachungaji ni watu wenye elimu kubwa katika masuala mbalimbali pia na mishahara yao ni mikubwa. Pia wanatunzwa vizuri sana na Kanisa.
Swali: Iweje kwa utumishi uliotukuka wa Mwasapila aishie kuishi kwenye kibanda kile?
Kanisa lilikuwa wapi siku zote?
Alitengwa?
Kwa nini?