Jk katika utawala wake kaweka rekodi ya kufanya madudu mengi sana,siwezi kuyaorodhesha hapa kwani watu washayazungumza sana! Ila huyu jamaa kajitahidi sana kukuza demokrasia na kupunguza kuogopana katika jamii,ijapokuwa ana mapungufu ya kuchakachua kura! Nakumbuka katika tawala zilizopita kuna watu walikuwa ni miungu watu,hawashikiki! Wote 2nakumbuka ukilaza wa sumaye enzi zake lakini kazi ya kupambana na watu kama hao 2limwachia lyatonga peke yake! Siku hizi ni ful kujiachia,mtu unaweza kusema chochote kuhusu chochote na ukapeta tu! Magazeti ni kama utitiri na kila cku baadhi yao yanaandika mambo kinyume ya maadili au yanatukana watu,lakini yanapeta streetz! Pamoja na matatizo yake lakini ndani ya tanzania ss ni kujimwaga tu,sema chochote! Sasa najaribu kujiuliza kama hizi ni juhudi binafsi za kikwete katika kukuza demokrasia au kabanwa kwenye angle ana jinsi ya kufanya??inambidi 2 awe mpole?