Ahsante Joblube kwa kuleta thread hii. Ni jambo la msingi sana. Timing is everything. CHADEMA wametumiwa na Rostam Aziz na Edward Lowassa bila wao kujijua. List of Shame hii mpya waitoe baada ya siku 90 walizopewa mafisadi hawa ili tusije kuwasaidia katika mbinu zao chafu za kuzuia wasifukuzwe CCM. Lengo lao ni kuibua tuhuma mpya dhidi ya viongozi wengi CCM ili defence yao kwenye kikao kijacho cha NEC kiwe mbona tumetuhumiwa wengi, ikiwemo Kikwete, Sumaye, Magufuli, na wengine basi hatua zichukuliwe kwa wote.
Ukweli ni kuwa tuhuma dhidi ya Lowassa, Rostam na Chenge ni very serious, zimeenea nchi nzima na wenyewe ndani ya serikali na CCM wanajua ni za kweli. Wangetakiwa kuwa jela hawa watu, ila bado kuna kulindana serikalini.
Mimi nilileta thread inayofanana na hii ila moderators kwa "busara" zao waliamua kuitoa na kuificha ndani ya thread nyingine.
Chonde chonde moderators msifute thread hii wala kuificha ndani ya thread nyingine. Ni muhimu kujalidi suala hili kwa kina kwa maslahi ya taifa.
Thread yangu iliyotolewa na moderators ni hii hapa:
CHADEMA yatumika kuwaokoa Rostam, Lowassa wasifukuzwe CCM!
CHADEMA sasa imeanza kutumika kuwasafisha Rostam Aziz, Edward Lowassa na Andrew Chenge wasifukuzwe kwenye nafasi zao za uongozi ndani ya CCM.
Kutumika kwa CHADEMA ni sehemu ya mkakati wa Rostam, Lowassa na wenzake kuzuia wasifukuzwe kuwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) na nafasi zao nyingine za uongozi.
Mkakati huo unahusu kuitumia CHADEMA na viongozi wa vyama vingine vya upinzani, kama CUF, NCCR Mageuzi, UDP, TLP na DP ya Christopher Mtikila, kutoa tuhuma za kupikwa kwa viongozi wengi zaidi ndani ya CCM ili ionekane kuwa viongozi wote wa CCM wana tuhuma za ufisadi na si Lowassa, Rostam na Chenge tu.
Tuhuma hizo za kutengenezwa sasa zimeanza kusambazwa na kina Rostam dhidi ya Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Jakaya Kikwete, na viongozi wengine waandamizi wa chama ambao wanaheshimika katika jamii, akiwemo John Magufuli, Samuel Malecela, Frederick Sumaye, Samuel Sitta, Bernard Membe na wengine.
Rostam na Lowassa wanaitumia CHADEMA ili kuzuia kufukuzwa kwenye CCM kupitia LIST OF SHAME mpya ya chama hicho cha upinzani ambayo imewataja kina Magufuli na Malecela. Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilibrod Slaa, ameingizwa mkenge
na viongozi wenzake ndani ya chama hicho kuitoa LIST OF SHAME mpya bila kujua kuwa mpango huo umepikwa na kina Rostam.
Rostam na Lowassa kwa kutumia viongozi wa CHADEMA ambao wako nao karibu wamemuingiza mkenge Dk. Slaa aitoe List of Shame mpya ili kuleta mvurugano ndani ya CCM.
Siyo "coincidence" hata kidogo kuwa CHADEMA waliibuka na LIST OF SHAME yenye majina mapya siku chache tu baada ya CCM kuwataka kina Rostam, Lowassa na Chenge wajiuzulu.
Inaeleweka wazi kuwa Rostam na Lowassa wako karibu sana na baadhi ya viongozi wakuu wa CHADEMA (siyo Dk. SLAA) na wamekuwa na mawasiliano ya mara kwa mara nao.
"Wanachotaka kufanya kina Rostam, Lowassa na Chenge ni kuibua tuhuma mpya za uongo dhidi ya Kikwete, Magufuli, Malecela, Sitta, Mwakyembe, Sumaye na viongozi wengine wa CCM ili wapate kujitetea kwenye vikao vya NEC vijavyo kuwa mbona kuna viongozi wengi za CCM wenye tuhuma lakini wanatakiwa wajiuzulu wao tu," alisema mpambe mmoja wa Lowassa.
Pia, Rostam na Lowassa wamekuwa wakitumia baadhi ya magazeti, likiwemo Tanzania Daima linalomilikiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, katika mkakati huo wa kuibua tuhuma za kupikwa za ufisadi dhidi ya viongozi wengi zaidi ndani ya CCM ili wajinurusu kufukuzwa.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, wiki hii CHADEMA ililazimika kukanusha habari za Tanzania Daima, gazeti la mwenyekiti wa chama hicho, zilizodai kuwa Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, ametajwa kwenye List of Shame mpya ya CHADEMA.
Lowassa amemuajiri mhariri mkuu wa Tanzania Daima, Absalom Kibanda, kwenye jarida lake la UMOJA na amekuwa akimtumia Kibanda mara kwa mara kutoa habari na makala za kumsafisha Lowassa, Rostam na Chenge kwenye Tanzania Daima.
Inafahamika wazi kuwa Kibanda ana urafiki wa karibu sana na Lowassa na Rostam na amekuwa akitumiwa mara kadhaa kuwachafua maadui zao, ikiwemo Samuel Sitta, Bernard Membe, Harisson Mwakyembe, na wengine.
Mafisadi wamekuwa wakipenda kulitumia sana Tanzania Daima mara nyingi kujaribu kujisafisha kwa kuwa linaheshimika kwenye jamii kwa kuonekana kuwa gazeti "huru" kuliko magazeti ya RAI na Mtanzania yanayomilikwa na Rostam.
Kwa kufuata maelekezo ya Lowassa, Tanzania Daima juzi iliandika habari ya uongo kwa makusudi kuwa CHADEMA imemtaja Sumaye kwenye List of Shame mpya.
Bado ni kitendawili kikubwa kwa nini Mbowe anamruhusu mhariri wake mkuu, Kibanda, kuwa mwajiriwa wa Lowassa na hivyo kuwa na mgongano wa kimaslahi na kimaadili (conflict of interest/ethical dilemma) katika kazi zake Tanzania Daima.