Elections 2010 Kwa hili chadema hamtaeleweka

Kuna watu hapa jamvini wanajiunga na jamvi kwa makusudi ya kutuchanganya tu na halafu watatoweka wakimaliza kazi walizotumwa na mabwana zao. Inakuwa taabu hata kuchangia maana ni muhimu kuangalia lini mleta hoja amejiunga jamvini kabla hujasoma alichokileta. Wanatafuta mahali pa kupumulia pressure zao kwani wanajisuta mioyoni mwao. Utawajua kwa hoja zao.
 
Hamna uchakachuzi huyo ni Dr asiyekubali kushindwa!
Wahenga walisema Asiyekubali kushindwa..... na Kinana leo TBC Taifa amesema pamoja na kuupata Udokta wa Dini (canon law) safari hii ameupata udokta wa Uzushi...kazi kwelikweli
 
Kufuatia kauli aliyoitoa dr slaa kua hawatakubaliana na matokeo ya uraisi na ubunge kwa kile anachokidai kua kuna wizi wa waziwazi umefanyika. nategemea yafuatayo yafanyike kama kweli anataka sisi tuliompigia kura tujue kweli chadema ipo kwa ajiri ya watu na sio mtu binafsi.1; wabunge waliochaguliwa kupititia chama hicho wasikubali kuingia bungeni kwa kua zoezi zima halikua huru na haki. la sivyo tutajua kua kila mtu alikua anatafuta kula na sio kura,
2.kama alivyojibu jaji makame kua hajapata malalamiko yoyote toka kwa chadema tafadhali wafanye haraka kulifisha hilo wakiwa na vielelezo vya kutosha.
3. jammii za kimataifa zijulishwe upesi kilichotokea kwa vielelezo maana tayari wameshasema uchaguzi ulikua huru na haki.
4. wajitoe kwa hari na mali kupigania haki yao hiyo mpaka tone la mwisho la damu.

Dr Slaa hajasema kila aliyechaguliwa katika uchaguzi mkuu 2010 hakuchaguliwa kwa uhuru na haki bali anazungumzia baadhi ya matokeo, ambayo ana ushahidi nayo kuwa kura zilizopatikana kwenye baadhi ya vituo vya wapiga kura ni tofauti na zile zilizotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Taifa. Kwa hiyo, anazungumzia matokeo, ambayo ana ushahidi nayo na siyo yote. Maana itakuwa vigumu kukataa kile ambacho mtu hana ushahidi wake. Ila wewe kama una ushahidi pia wa hao wabunge wa Chadema unaweza kuutoa ili wajulikane ni akina nani hao ili makosa kama hayo yarekebishwe. Kwa kifupi kinacholalamikiwa ni kuona kuwa 2 + 2 siyo 4 bali ni 3 au 7. Hesabu za namna hii ni ngeni katika hisabati tunazojifunza na kama kuna kanuni mpya inayotumika kuonesha 2 + 2 = 3 au 7, basi hiyo kanuni ndiyo tunayoomba ielezwe kwa wote.

Kwa hiyo, mjadala ulenge zaidi 'facts' kuliko ushabiki au hisia. Sisi wengine hapa hatuna chama tunachounga mkono na tunaunga mkono kila kitu kizuri kilicho katika kila chama na tunakosoa pale tunapoona ukweli na haki vinapindishwa. Wote tuajili hoja kwa kuzingatia maslahi ya nchi na siyo ushabiki wa vyama. Udhaifu wa kimfumo au utawala tunaouendekeza utatugharimu kwa baadaye - kama siyo kwetu sisi itakuwa kwa watoto na wajukuu wetu. Turekebishe pale tunapokosea ili mambo yetu yaende vizuri!
 
wahenga walisema asiyekubali kushindwa..... Na kinana leo tbc taifa amesema pamoja na kuupata udokta wa dini (canon law) safari hii ameupata udokta wa uzushi...kazi kwelikweli

alipotoa tuhuma za epa kwa mara ya kwanza walisema hivyohivyo, lakini mwisho wa siku ukweli umedhihiri, na siku ukweli wa kuchakachua kura ukidhihirika sijui kinana atasemaje????
 
Kufuatia kauli aliyoitoa dr slaa kua hawatakubaliana na matokeo ya uraisi na ubunge kwa kile anachokidai kua kuna wizi wa waziwazi umefanyika. nategemea yafuatayo yafanyike kama kweli anataka sisi tuliompigia kura tujue kweli chadema ipo kwa ajiri ya watu na sio mtu binafsi.1; wabunge waliochaguliwa kupititia chama hicho wasikubali kuingia bungeni kwa kua zoezi zima halikua huru na haki. la sivyo tutajua kua kila mtu alikua anatafuta kula na sio kura,
2.kama alivyojibu jaji makame kua hajapata malalamiko yoyote toka kwa chadema tafadhali wafanye haraka kulifisha hilo wakiwa na vielelezo vya kutosha.
3. jammii za kimataifa zijulishwe upesi kilichotokea kwa vielelezo maana tayari wameshasema uchaguzi ulikua huru na haki.
4. wajitoe kwa hari na mali kupigania haki yao hiyo mpaka tone la mwisho la damu.

Wewe ndiye ambaye hautawaelewa CHADEMA na hatutaki uwaelewe kwa sababu Tanzania itakuwa salama zaidi ikikosa watu kama wewe
 
wewe unaeijua tueleze unaijua vipi kulingana na mada iliyopo sebuleni
 
kufuatia kauli aliyoitoa dr slaa kua hawatakubaliana na matokeo ya uraisi na ubunge kwa kile anachokidai kua kuna wizi wa waziwazi umefanyika. Nategemea yafuatayo yafanyike kama kweli anataka sisi tuliompigia kura tujue kweli chadema ipo kwa ajiri ya watu na sio mtu binafsi.1; wabunge waliochaguliwa kupititia chama hicho wasikubali kuingia bungeni kwa kua zoezi zima halikua huru na haki. La sivyo tutajua kua kila mtu alikua anatafuta kula na sio kura,
2.kama alivyojibu jaji makame kua hajapata malalamiko yoyote toka kwa chadema tafadhali wafanye haraka kulifisha hilo wakiwa na vielelezo vya kutosha.
3. Jammii za kimataifa zijulishwe upesi kilichotokea kwa vielelezo maana tayari wameshasema uchaguzi ulikua huru na haki.
4. Wajitoe kwa hari na mali kupigania haki yao hiyo mpaka tone la mwisho la damu.

kusua kuingia bungeni ndio upuuzi kabisa. Toka lini ccm waliacha kuiba kura? Lakini kidogo kidogo ukombozi umeendelea kupatikana kila baada ya uchaguzi licha ya wizi wa kura uliofanyika. Mathalani mwaka 2000 kama akina dr slaa, zitto na wabunge wengine wa upinzania wangesusa kuingia bungeni kwa madai ya wizi wa kurakama unavyoshauri kashafa zote zilizofichuliwa yaani epa, richnmond, n.k zisingejulikana na raslimali za tanzania hususan madini visingeboreshewa utaratibu wa ke kwa nia ya kuliongezea taifa mapato.

Yaani timu ya chadema ikisusa kuingia bungeni ndio mafisadi watasherehekea.

Nina wasi wasi hoja ya kususa kuingia bungeni inaanzishwa na uwt waliohusika kuiba kura zetu kwa nia ya kuvunja nguvu na mshikamano wa wanachadema
.
 
Gazeti la jana la MWananchi na hata Nipashe yaliandika yafuatayo: Mwananchi:· 1. EU: CCM imebebwa na vyombo vya dola· 2. Madola wakosoa sheria za uchaguzi IPP Media· Waangalizi Madola: Uchaguzi haukuwa na uwanja sawa · Ucheleweshaji wa matokeo wasikitisha waangalizi. Tuwe wakweli jamani hayo yamesemwa na watu wa nje bado wewe Mtanzania unakataa huo ukweli!
 
kusua kuingia bungeni ndio upuuzi kabisa. Toka lini ccm waliacha kuiba kura? Lakini kidogo kidogo ukombozi umeendelea kupatikana kila baada ya uchaguzi licha ya wizi wa kura uliofanyika. Mathalani mwaka 2000 kama akina dr slaa, zitto na wabunge wengine wa upinzania wangesusa kuingia bungeni kwa madai ya wizi wa kurakama unavyoshauri kashafa zote zilizofichuliwa yaani epa, richnmond, n.k zisingejulikana na raslimali za tanzania hususan madini visingeboreshewa utaratibu wa ke kwa nia ya kuliongezea taifa mapato.

Yaani timu ya chadema ikisusa kuingia bungeni ndio mafisadi watasherehekea.

Nina wasi wasi hoja ya kususa kuingia bungeni inaanzishwa na uwt waliohusika kuiba kura zetu kwa nia ya kuvunja nguvu na mshikamano wa wanachadema
.

You have a point!
 
data hizi hapa chache

Kwa mujibu wa Dk Slaa, ambaye pia ni katibu mkuu wa Chadema, chama chake kimekuwa kikifuatilia kwa makini matokeo hayo na kugundua wizi mkubwa wa kura kwenye nafasi za urais na ubunge.
Mgombea huyo wa urais, ambaye mara nyingi hujenga hoja kwa kutumia ushahidi, alisema moja ya maeneo waliyogundua kuwepo kwa wizi wa kura ni matokeo ya Jimbo la Geita lililo mkoani Mwanza ambako alidai Nec ilitangaza kuwa kwenye uchaguzi wa rais, CCM imepata kura 17,792 na Chadema kura 3,789.
Lakini akasema kwa mujibu wa fomu walizonazo ambazo zilisainiwa na mawakala wao kwenye kata 20 za jimbo hilo, CCM ilipata kura 30,960 na Chadema 15,736.
"Nashangaa Nec wanatangaza matokeo haya kutoka wapi? Hayo ya Geita ni moja tu. Kule Hai, fomu zinaonyesha kwenye urais CCM ina kura 20,120 na Chadema 26,724, lakini Nec imetangaza kuwa CCM ina kura 35,910 na Chadema kura 18,513," alisema Dk Slaa huku akionyesha baadhi ya fomu kwa waandishi wa habari.
Dk Slaa pia alitoa mfano aliodai kuwa wizi wa kura katika kituo namba 00070103 cha Ubungo jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa fomu 24A inaonyesha CCM wamepata kura 68,727 na Chadema 65,450, lakini matokeo ya kata za Ubungo yanaonyesha CCM ina kura 70,472 na Chadema 72,252.
Dk Slaa alisema mbali na Ubungo, tatizo hilo pia alidai liko Kigoma Mjini ambako Chadema imeshinda kwa zaidi ya kura 500, lakini "matokeo yalichakachuliwa na kusababisha vurugu hadi askari wakawapiga mabomu wafuasi wa Chadema".
Pia alisema kwenye Jimbo la Segerea, ambako matokeo yalicheleweshwa kwa siku mbili na kutangazwa usiku wa manane juzi, mambo ni mabaya zaidi kwa kuwa fomu 21 A na B hazikuwepo na wasimamizi walikwenda nazo majumbani kulala.
"Kiwalani fomu hazikuwepo na matokeo hayakuonekana. Kipawa vituo vinne matokeo hayakuonekana na Vingunguti kuna vituo saba na Tabata vituo viwili ambako matokeo hayakuonekana," alisema Dk Slaa.
Aliongeza kusema: "Hali kama hiyo pia imetokea Morogoro Mjini. Matokeo hayajaonekana na yametangazwa tu. Kibakwe na Kiteto mgombea hakushirikishwa katika kutangaza matokeo.
"Hayo ni majimbo ya mifano tu. Yapo majimbo mengi na kutokana na hali hiyo, Chadema imetoa tahadhari kwa Tume na vyombo vya ulinzi na usalama kuwa taratibu hazijafuatwa na nyingi zimevunjwa."
Dk Slaa alisema kuwa ni muhimu waangalizi wote wa uchaguzi wakatoa taarifa zao hadharani ili kusaidia nchi na kumtaka mkuu wa Jeshi la Polisi kuendesha chombo hicho cha dola kwa haki na maadili waliyosaini.
Baadaye mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema kuwa kauli hiyo ya Dk Slaa ni tamko rasmi la Chadema.

Kutoka Mwananchi la leo

More data pls
 
Azipeleke mahakamani zikathibitishwe, hatutaki RAW DATA hapa , please !

Mahakama yenyewe ya bongo, inayo amrishwa ni yupi apewe ushindi ama askilizwe?, mahakama kuu kuliko zote Bongo ni sisi wananchi,

Asante Dr wa ukweli kutuwekea data halisi, endelea kukusanya zote na vidhibitisho vyote ili waumbukE hadi wakose pa kuficha nyuso zao!
Hakuna adhabu iliyo kubwa kama fedheha ya mtu mzima kuumbuliwa mchana kweupe

HONGERA SANA DR. WA UKWELI, KUPITIA KWAKO TUMEPATA MASLAA MENGI BUNGENI, MADIWANI HAO NDO USISEME. MUNGU AKUBARIKI SANA!
 
Back
Top Bottom