Kwa hili ACT Wazalendo wanafaulu, ni mkakati mzuri kurudi kwenye Media spotlights

Mtimbo

JF-Expert Member
Jan 18, 2012
1,392
796
Habari wakuu! Poleni na majukumu ya kila siku yakuhakikisha watoto wetu wanapishana kwenda njia ya chooni.
Nirudi kwenye mada;

Mtakumbuka tangu CHADEMA kutangaza vuguvugu la UKUTA chama cha ACT wazalendo kimepotea kabisa kwenye media,ndio kusema hawana ajenda (iwe mbaya au nzuri) ya kuvivutia vyombo vya habari ili ku cover habari zao.

Kuelekea ile tarehe moja September ya UKUTA, ZZK Kiaongozi wa chama alijaribu mara kadhaa bila mafanikio kukirudisha chama kweye midomo ya watu na media mbalimbali kama magazeti lakini bado hali ikawa mbaya,

ZZK alifikia hatua kabisa ya kutoa tamko kuwa chama chake hakitashiriki kwenye maandamano ya UKUTA isipokuwa watashiriki katika zoezi la utoaji wa damu kwa majeruhi wa vuguvugu,pamoja na statement hiyo bado media hazikumpa ushirikiano wa kutosha.

Hata pale Vuguvugu la UKAWA lilipokwama na kughairishwa na waanzilishi wa vuguvugu hilo kweli mwangwi wa UKAWA ukapungua kwenye media lakini kufumba na kufumbua Mara mgogoro wa CUF huoo. ACT Ikaendelea kuwa taabani kwenye media na CUF ndio topic kwa sasa kwenye media.

Tarehe 8 mwezi huu October tayari Chama cha ACT wazalendo wametangaza kuwa na mjadala wa kujadili Katiba mpya, tayari mialiko mabalimbali imeshatumwa kwa watu mbalimbali wa ndani na wa nje, Pamoja na umuhimu wa mjadala huo bado media haujaupa covarage ya kutosha ukizangatia hadi leo zimebaki siku mbili tu.

Ndipo napoona mfalme wa vina
( Selemani Msindi) Akifanya yake kwa kushirikiana na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT, ZZK kukirudisha chama kwenye Media na tayari wanaonekana kufaulu kwenye hilo kwani leo karibia robo tatu ya magazeti yameripoti habari za ACT.

Media wameripoti eti Afande selle afunguka juu ya ukigeugeu wa Viongozi wa ACT, Wakimnukuu maelezo yake yaliowekwa kwenye ukurasa wake wa instagram.

Kwenye hili wala uhitaji kuwa na elimu ya chuo unachohitaji ni kuwa tu na akili za kukupeleka tu msalani na kurudi bila harufu kugundua kuwa kinachoendela ni promotion na hakika promotion inafana na itaendelea kufana na hatimae wanamkakati kufanikiwa.

Kitakachokuwamsha akili ni hiki kwamba wakati Afande sele akilalamikia Ukigeugeu wa viongozi wake ACT lakini kubwa sidhani kama anaweza kuthubutu kusahau ukigeugeu wa viongozi wa CHADEMA dhidi ya LOWASSA.
 
Tunasonga mbele,sisi sio wataalam wa fitna, kama chadema kuutwa kazi yao ni kuchochea mgogoro wa kafu
 
Mkuu hata mie nimeona hili suala limekaa kama la kutengenezwa,alichokiongea Afande sele hata hakina maana ila Zitto ana sema atakifanyia kazi.
 
Back
Top Bottom