Man Mvua
JF-Expert Member
- Apr 12, 2016
- 2,184
- 3,517
- Thread starter
- #21
Hata wewe unaandika hali ya kuwa unajua kuwa unadanganya, tena unadanganya waziwazi. Hizo points zako kawaambie UVCCM wenzio.Sisi watanzania tumempima Rais Magufuli na tumeamua kuwa pekee anatosha 2020, kwa sababu:
1. Miaka minne ya utawala wake imeonekana hali ya màisha ya mtanzania mnyonge imeboreka kuliko wakati wowote na hii ni kutokàna na hulka ya Rais wetu kujali kundi hilo kubwa la watanzania. Baadhi ya watanzania walizoea kuishi kiujanjaujanja kwa kukwepa Kodi na kufanya shughuli zisizo rasmi. Watu Hawa ndio wanàona Magufuli kàbana
2. Kwa maana ya ajira ,Serikali ya awamu ya tano imejitahidi kuboresha mazingira ya sekta binafsi kukua hasa kuzalisha ajira kupitia sekta isiyo rasmi kama ujasiriamali na biashara ndogondogo. Pamoja na hili, Serikali pia imejitahidi kutoa ajira za muda mfupi na zile za kudumu.
3. Suala la usalama ni jukumu la kila mtu kwa sababu wanaohatàrisha usalama ni wanajamii wenzatu tunaishi nao na wengine wanafichwa na sisi wenyewe, hatushirikiani na serikali kuwafichua hii inaaminisha hao watu kuwa wapo salama. Tukija kwenye matukio kama Kibiti na mapango ya amboni tumeona kwa kiasi gani Serikali ipo makini kukomesha vitendo viovu.
4. Chombo chà kutazamia kuwa Kuna utawala wa sheria na katiba inaheshimiwa ni mahakàmà. Hakuna uthibitisho wowote wa kesi yeyote ya kimahakama kuhusu kesi iliyofunguliwa kwamba Serikali imevunja sheria na katiba. Kinachofanyika ni kuchagua Serikali kupitia siasa za majitaka.
4. Hakuna uhuru usio na mipaka na mipaka ya media na watu unàwekwa nà sheria na katiba. Kama taifa ,tutaonekana hatuko makini kama tutaruhusu watu au media kuropoka uzushi nà uzandiki kila wanapotaka kufanya hivyo.
Sent using Jamii Forums mobile app