Kwa haya, Rais Magufuli hatufai kama ni wenye kutafakari

Man Mvua

JF-Expert Member
Apr 12, 2016
2,184
3,517
Habari za asubuhi.

Sisi watanzania tuna tatizo kubwa sana la kufikiri na kuchambua mambo. Uzuri wa Rais haupimwi kwa

1. Kujenga miundombinu maana ndio kazi yao na wana tumia kodi zetu. Mtu hana hata aibu kusema Rais kajenga barabara, flyover na madaraja sasa wewe ulitaka afanye nini kama Rais.

2. Kudhibiti ufisadi na matumizi mabaya ya serikali ni kazi ya Rais wala sio favour kwa Watanzania.

3. Kuhamia Dodoma ni utashi wake binafsi wala halina impact yoyote kwa maisha ya mtanzania ila ni kutaka sifa tuu

4. Kujenga hospitali au mashule ni kazi ya serikali kwa kutumia kodi za wananchi.

TUKITOA HAYO RAIS MAGUFULI KAFANYA NINI CHA MAANA ??

RAIS MZURI HUPIMWA KWA :

1. Kuboresha maisha ya watu hasa mtu mmoja mmoja.

2. Kutengeneza ajira za kutosha nchini ( sote mashuhuda kwa hili jinsi Rais Trump anavyojivunia)

3. Kulinda usalama wa wananchi na Mali zao. ( hapa kafeli vibaya sanaa maana kuna wenzetu wameumizwa vibaya na wengine kuuwawa au kupotea)

4. Kulinda katiba na sheria

5. Uhuru wa wananchi, media na vyombo vya habari.

RAIS MAGUFULI KAFANYA YEPI KATI YA HAYO HAPO JUU ???

Watanzania tuache ujinga tuipende na kuilinda Nchi yetu tusiwe wanyonge kwenye Nchi yetu wenyewe na kuleta sifa za kijinga kisa wewe umeshiba ugali wa Jana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magufuli Ni rais mzuri Sana ila ibada za wachawi 1000 wa Gamboshi na Uchawi wa Mwenge wa Uhuru vinafanya aonekane mtu wa ajabu
Ukisoma vizuri post yangu jamaa hajafanya lolote, Ajira hakuna,,, maisha magumu, usalama wa raia hovyo. Sisi tu na ujinga wetu kumshabikia na kutojua kazi za Rais.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukisoma vizuri post yangu jamaa hajafanya lolote, Ajira hakuna,,, maisha magumu, usalama wa raia hovyo. Sisi tu na ujinga wetu kumshabikia na kutojua kazi za Rais.

Sent using Jamii Forums mobile app
Uko sahihi, hayupo kwa ajili ya kutimiza matakwa ya watz ndio maana ananunua mabundi kwa cash wakati hakuna vyumba vya madarasa vya kutosha
 
Badala ya kukuza uchumi na kujenga misingi imara ya kuelendelea kukua kwa uchumi wetu yeye ndo yuko busy kuharibu kwa kutumia mihemko yake ya kishamba,Kaua soko la zao la korosho, kahawa, mbaazi,tumbaku,Kaua sector ya madini kisa definition zake za catalysit na smelter, kaua kilimo kaua sector binafsi,kaharibu mahusiano na wadau wetu wa maendeleo and as a result ujenzi wa barabara ya njia sita Dar chalinze umeahirishwa kwa muda usiojulikana, yaani kwa kifupi he is so good for petty issues and so poor in all must do things
 
Badala ya kukuza uchumi na kujenga misingi imara ya kuelendelea kukua kwa uchumi wetu yeye ndo yuko busy kuharibu kwa kutumia mihemko yake ya kishamba,Kaua soko la zao la korosho, kahawa, mbaazi,tumbaku,Kaua sector ya madini kisa definition zake za catalysit na smelter, kaua kilimo kaua sector binafsi,karibu mahusiano na wadau wetu wa maendeleo, yaani kwa kifupi he is so good for petty issue and so poor to all must do things
Halafu kuna mijitu eti inampima kwa barabara, madaraja na flyovers as if hizo pesa katoa kwenye mfuko wake..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi watanzania tumempima Rais Magufuli na tumeamua kuwa pekee anatosha 2020, kwa sababu:

1. Miaka minne ya utawala wake imeonekana hali ya màisha ya mtanzania mnyonge imeboreka kuliko wakati wowote na hii ni kutokàna na hulka ya Rais wetu kujali kundi hilo kubwa la watanzania. Baadhi ya watanzania walizoea kuishi kiujanjaujanja kwa kukwepa Kodi na kufanya shughuli zisizo rasmi. Watu Hawa ndio wanàona Magufuli kàbana

2. Kwa maana ya ajira ,Serikali ya awamu ya tano imejitahidi kuboresha mazingira ya sekta binafsi kukua hasa kuzalisha ajira kupitia sekta isiyo rasmi kama ujasiriamali na biashara ndogondogo. Pamoja na hili, Serikali pia imejitahidi kutoa ajira za muda mfupi na zile za kudumu.

3. Suala la usalama ni jukumu la kila mtu kwa sababu wanaohatàrisha usalama ni wanajamii wenzatu tunaishi nao na wengine wanafichwa na sisi wenyewe, hatushirikiani na serikali kuwafichua hii inaaminisha hao watu kuwa wapo salama. Tukija kwenye matukio kama Kibiti na mapango ya amboni tumeona kwa kiasi gani Serikali ipo makini kukomesha vitendo viovu.

4. Chombo chà kutazamia kuwa Kuna utawala wa sheria na katiba inaheshimiwa ni mahakàmà. Hakuna uthibitisho wowote wa kesi yeyote ya kimahakama kuhusu kesi iliyofunguliwa kwamba Serikali imevunja sheria na katiba. Kinachofanyika ni kuchagua Serikali kupitia siasa za majitaka.

4. Hakuna uhuru usio na mipaka na mipaka ya media na watu unàwekwa nà sheria na katiba. Kama taifa ,tutaonekana hatuko makini kama tutaruhusu watu au media kuropoka uzushi nà uzandiki kila wanapotaka kufanya hivyo.
 
Huyu mpuuzi ni kwa vile tu aliingia madarakani kwa MABAVU, huyu alipaswa kuwa NYAMPARA si Rais. Rais anapaswa kuhakikisha usalama wa Raia wake, huduma za kijamii kwa Wananchi wake wote bila ya UBAGUZI, Utawala unaoheshimu KATIBA YA NCHI, Haki za Binadamu n.k
Huyu MWENDAWAZIMU hakuna hata moja analolizingatia kati ya hayo, badala yake amejikita kwenye UBABE, VITISHO, KUGAWA WANANCHI, KUPOTEZA WAKOSOAJI, UKATILI KWA WANANCHI na mambo mengine mengi ya hovyo hovyo.
 
Amesambaratisha utaifa wetu. Tofauti za kikanda na kikabila utaziona kwenye teuzi zake anaanza kupendelea familia/ kabila, kisha wilaya, halafu mkoa na mwishowe kanda anayotoka yeye.

Ni aghalabu kuteua Waisalmu, ila yuko tayari kumfuta kazi Muislamu mchapa kazi kama Prof Mussa Assad kwa kuwa ana msimamo na maadili ya kazi.

HATUFAI kwa Oktoba 2020
 
Back
Top Bottom