Kwa Hali hii ni Hatari Tuombe Huruma ya Mungu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa Hali hii ni Hatari Tuombe Huruma ya Mungu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by bemg, May 24, 2011.

 1. bemg

  bemg JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2011
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,706
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Wana JF bila kujali dini zetu tuombe Mungu atuhurumie maana watawala wetu na vyombo vya kulinda usalama wetu vimekuwa adui wa uhai wetu. Maisha magumu,ukame,ajali,ufisadi,maneno matamu kwa watawala na askari wanaua raia mchana kweupe hakuna anayeajibishwa.Inauma sana nainatia huruma sana.

  Mungu utukumbe mambo yaliyotupa na yanayoendelea kutupa tangu tumekuwa chini ya uhuru wetu,atuangalie aone jinsi tunavyozidi kuabishwa na utawala tulionao kwa sasa.

  Maliasili na nchi yetu imekabidhiwa wageni na nyumba zetu watu wengine.Tumekuwa kama yatima bila baba wakututetea na mama zetu wanaonekana kama wajane.Wanapotokea watu wenye huruma na tunavyoteseka ili watutetee wananchi watawala wanawaita ni wahaini.Ee Mungu tuhurumie.

  Maji yetu tunayapata kwa fedha kuni zetu zinazotokana na miti yetu pia twanunua.Tunalazimishwa kulipa kodi kubwa lakini mafisadi yanazitafuna mchana kweupe hakuna wakuyakamata na kuyatia haitani.Watetezi wa walala hoi ndiyo wanakamatwa kila wakiinuka kutetea haki.Ee Mungu tuhurumie.

  Mabepari ndiyo wanaotutawala wala hakuna wa kutuokoa mikononi mwao ni wewe peke yako Mungu ndiyo mwenye uwezo kupitia watu wako walionahuruma ya mateso haya.Chakula chetu twapata kwa kuhatarisha maisha yetu maana wauaji wanazurura huko mashambani,ofisini, kwenye vyombo vya usafiri na mitaani.Ee Mungu tuhurumie.

  Vijana wetu na nguvu kazi ya taifa wanauwawa kwa nguvu kwenye ardhi yao na katika vijiji vyao kwasababu ya kulinda maslahi ya wageni.Furaha ya mioyo yetu imetoweka kwa chama tulichokipa matumaini ya kututoa kwenye umaskini,na ngoma zetu zimegeuzwa kuwa maombolezo.

  Tufariji Mungu na ututee .Mungu usituache muda mrefu hivi tuendelee kuteseka na hali hii.Ee Mungu utawala wa wafalme wa dunia hii ni wa muda tu lakini wewe watawala milele na utawala wako wadumu vizazi vyote.Tunaomba huruma yako na ushuke katika nchi yetu na utusamehe pale kama taifa tumekukosea na uturudishie umoja wetu na tufaidike na maliasili zetu.Ee Mungu tuhurumie.
   
 2. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #2
  May 24, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,246
  Likes Received: 3,836
  Trophy Points: 280
  Mungu yu pamoja nasi!
   
 3. Maarko

  Maarko JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,030
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Mwisho wa ubaya Aibu.
   
 4. kibakwe

  kibakwe Senior Member

  #4
  May 24, 2011
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tumuombe MUNGU huku tukiwa katika mstari wa mbele mapambanoni
   
 5. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kama maisha magumu fanya kazi kwa bidii ndugu yangu asiyefanya kazi na asile!!
   
 6. Y

  Yakuonea JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 601
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  hapa ni zaidi ya sala na maombi
   
 7. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #7
  May 24, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  "Mungu ibariki Tanzania. wabariki Viongozi wake...." Hili ni dua la kuku au Mungu bado anatupima? AU ndo viongozi aliowabariki hawa kwa ajili yetu?
   
Loading...