Kwa hali hii, kwanini housegirl asimchukue mumeo?

Kitena

JF-Expert Member
May 28, 2012
339
255
Kwa nini House girl asimchukue mumeo....



MUME: darl ninakikao mkoani kesho naomba niandalie vitu plz

MKE: dada zile nguo za baba pmj na soksi ulifua?

DADA: ndio nimepanga kabatini.

(Mama anarudi chumbani na
kumuomba hubby wakacheki TV
sebulen,, lakn baada ya muda mama anamuita dada akapange suruali kadhaa na mashati kwa ajili ya safari ya kesho,,

dada anapanga kila kitu anatoka.)

MKE: kama tayari hakikisha unarekebisha yale mashuka pale kitandan weka na maji bafuni.
(Dada anafanya na kwenda zake

kulala,, asubuhi dada anaamka
mapema na kuandaa kila kitu
ikiwamo na chai,, baba anakunywa chai na kutaka kuondoka.)
MKE: dada msindikize baba ili ufunge geti sababu bado ni giza

DADA: sawa mama.
(Dada anatoka na begi la baba hadi nje kwavile mkewe yupo ndani,, baba anamtaka dada abaki vizuri na watoto,, dada anaitika na kusema nawao wanamuombea safari njema.
Baada ya muda baba anarudi toka safari.)

MKE: (huku akitabasam) dada si umemuona baba amerudi vipi chakula tayari?

DADA: ndio.

MKE: haya kapange meza vizuri mimi nandaa juice.

(Baada ya muda wanakula na baba anagundua juice sio nzuri anaamua kuiacha na kusema leo wamesahau kuweka baadhi ya vitu hivyo hataweza kuinywa. Baadae baba anakumbuka kuwa aliacha boxer zake kwenye ndoo ya maji chumban na kufunika mfuniko, anamuuliza mama vipi zile nguo zangu kwenye
ndoo zilifuliwa? Maana nilisahau
kusema kama zina maji.)

MKE: (dada njoo hapa) hivi zile nguo za baba chumbani ulifua?

DADA: ndio mama
(lakin hasemi kama alianua na kuweka chumbani kwake akidhan atakunja baada ya kazi
kupungua)

MKE: darling zilifuliwa.

MUME: na watoto vipi wameshalala?

MKE: anajibu wamelala darl.

MUME: vipi dereva wao alifika kuchukua pesa yake?

MKE: dada eti uncle Hassan amechukua pesa yake?

DADA: hapana wamembadilishia gari uncle Hassan amesafiri kwa muda.

MKE: tutampatia darl siku akirudi acha dada aendelee kuitunza

MUME: basi vizuri, ehee vipi na tution walienda leo?

MKE: ndio walienda
(anamgeukia dada, si eti ee walienda si eti)

DADA: hapana Kelvin anaumwa leo siku ya pili nilinunua dawa dukan nimempa lkn hajambo.

MKE: (anashangaa) heeE! mtoto mgumu huyu kumbe jana alikua
mgonjwa halafu wala!!! alikua anacheza tu jamani watoto!! Asante dada umefanya vizuri!!

MUME: haya mimi niwaache nataka nikapumzike lkn darl nitaomba zile boxer nichome kabla ya kulala sababu zimeanza kuchoka!
(mke anaingia chumbani anafungua kabati na kuzikosa lkn kabla hajajieleza anamuona dada analeta mzigo wa boxer zikiwemo chupi za mama na mataulo)

MUME: basi dada zirudishe tutachambua kesho nenda kafanye kazi zako.

(mume anainuka na kuelekea kulala, lkn anagundua mke wake alimwaga nguo
itandan wkt anatafuta boxer hivyo anaamua kurudi sebuleni ili aombe kuandaliwa kitanda,,
kwavile chumba cha dada kipo jiran na chao anagundua dada ameacha mlango wazi,, anaamua kuufunga ili mbu wasiingie lkn anaona baadhi ya mashati na suruali zake zikiwa zimenyooshwa na kuwekwa pemben huku kitanda kikiwa kimetandikwa kwa ustadi anaamua kufunga mlango na kutoka,, anafika sebuleni anakuta mama anatazama tamthilia anamwambia akatandike kitanda.)

MKE: dada njoo... (kwa sauti ya
kunong'ona) naomba ukatandike
kitanda haraka

DADA: tayari nilipeleka viatu vya baba nikaamua kutoa na zile nguo
(mke anaamka na kwenda kuhakikisha anarudi na kumwambia mumewe tayari aende akalale...
mume anaenda kulala lkn huku

akijuiliza sana ni nini amfanyie huyu dada kwa ukarimu anaowafanyia hapo nyumban,,
kwanza anajua ni vitu gani baba anabeba akiwa safarini,,

ndio pekee anaemtakia safari njema na kumuombea,,

ndio anaefua boxer zake na kutunza vizuri,,

ndio anaepika chakula kitamu,,

ndio anaetandika kitanda chake,,

ndio anaejua juice gani baba anapenda,,

ndio anaejua kama watoto wamerudi vipi kutoka shule,,

vilevile ndio anaejua kama watoto wake wanaumwa ama vipi....)

Sasa Unafikiri baba atamzawadia nini huyu binti.. ???

Na mama amebakisha kumfundisha nini dada ili kesho asimsumbue tena mume wake ambae kila kitu lzm amuulize dada...?????

tunajifunza nini!!

wanawake wengi huwatengenezea wadada wa kazi mazingira ya kuvuruga ndoa zao bila wao kujua...
sambaza ujumbe huu kwa wanandoa wote na wanaojiandaa kuoa na kuolewa...
 
Hii kitu kina reflection lkn kwa karne hii km umeoa mfanyakazi na hasa siye tunaishi mbezi makabe na kazi posta haiepukiki hata, wife anafikahome saa 3 saa 10 subuhi ameamka atapata wapi mda wa kufua mkuu?
Vinginevyo aache kazi awe golokipa
 
Kizuri kula na housegirl mama watoto ni kumzalisha mwanzo mwisho.Kwa uvivu huo mchepuko lazima ukuhusu.
 
Hii kitu kina reflection lkn kwa karne hii km umeoa mfanyakazi na hasa siye tunaishi mbezi makabe na kazi posta haiepukiki hata, wife anafikahome saa 3 saa 10 subuhi ameamka atapata wapi mda wa kufua mkuu?
Vinginevyo aache kazi awe golokipa

Muelewe hoja hapo sio kurudi usiku au bize anapata wapi muda wa kuangalia tv na wa kutoa amri ambayo kapewa na mumewe.Mbaya zaidi watoto wanaumwa hata hajui.
 
Hii kitu kina reflection lkn kwa karne hii km umeoa mfanyakazi na hasa siye tunaishi mbezi makabe na kazi posta haiepukiki hata, wife anafikahome saa 3 saa 10 subuhi ameamka atapata wapi mda wa kufua mkuu?
Vinginevyo aache kazi awe golokipa

sasa kwani mwanamke aliwekwa duniani kuajiriwa kazini au kazi yake ni kugegedwa nakulea familia. wewe mwanaume unatakiwa uweze kumuhudumia mkeo pasipo yeye kuhitaji kufanya kazi apart from kulea watoto
 
Me tangu nipo O Level nine chaps sana housgirls yani kuna mmoja wa Mnyaturu wa Singida balaa I was 18 by age ye alikuwa kama 24 hiv yani mtoto ana sex balaa shanga Maunooo acha kabisaa
 
Hii kitu kina reflection lkn kwa karne hii km umeoa mfanyakazi na hasa siye tunaishi mbezi makabe na kazi posta haiepukiki hata, wife anafikahome saa 3 saa 10 subuhi ameamka atapata wapi mda wa kufua mkuu?
Vinginevyo aache kazi awe golokipa
Mpangilio wa muda,mwanamke anapaswa kumuhudumia mumewe
 
Kuoa golikipa hawataki mana anakua omba omba wa pesa,wanataka anaefanya kazi/biashara
Wakishamuoa wanataka aendelee na kazi yake na afanye kazi kama housegirl
Sitetei uzembe lakini maisha yamebadilika...na baadhi ya wanawake wanafanya kazi ngumu kuliko waume zao
 
Haiepukiki sawa.. na kugonga housegirl hakutaepukika[/QUOTE

na huyo mke na yeye ykute anahudumiwa na boss wake hapa kuna wanaume hata ukiwayliza size ya mguu ya mke wake hajui wala hata nguo anazovaa hujui zinatoka wapi wala hata nauli ya basi au mafuta ya gari hujui anatoa wapi una assume anafanya kazi unaona anarembeka tu kila jmosi salonunafikiri ni mshahara wake. kumbeeee
 
Huo utumwa ulikuwa zamani, kwa sasa huwezi kuwa Na mke anafanya kazi usubiri paka boxer ufuliwe!
 
Back
Top Bottom