Kwa ccm ya sasa, nafuu Lowassa kuliko wengine | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa ccm ya sasa, nafuu Lowassa kuliko wengine

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JATELO1, Nov 18, 2011.

 1. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #1
  Nov 18, 2011
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  WanaJF,Kwanza naomba kudeclare interest kwamba; mimi ni mwana-CCM anayekaribia kuasi Chama na hii ni kutokana na kile kilichofanywa na Wabunge wa CCM Dodoma leo kwa kupitisha Muswada wa Katiba Mpya.Sasa wanaJF, Kwa upande wa CCM na wote wanaotajwa kuwania Urais hata mimi naona nafuu LOWASSA. Kwanza ana ujasiri kidogo kulinganisha na wengine. Pia ni mtendaji si mtu wa hadithi kama wale wengine. Tuwe tu fair na tuangalie ndani ya CCM kwasasa, je ni nani ana unafuu kuliko Lowassa? Mtu akisema Prof. Tibaijuka au Dr. Rose Migiro, mimi nawaambieni kabisa hakuna lolote jema watakaloweza kuwafanyia Watanzania, na nina wasiwasi kama watanzania wanaweza kumchagua Mwanamke hasa baada ya utendaji wa Spika wa sasa ambaye ni Mwanamke. Pia wale wanaume wanaofikiriwa hakuna wa kumlinganisha na Lowassa ktk uongozi na utendaji. Labda Dr. John Magufuli, lkn nina wasiwasi kwamba Dr.Magufuli ni MTENDAJI na si kiongozi. Nina wasiwasi mkubwa sana kuhusu uwezo wa kiuongozi wa Dr. Magufuli lkn sina wasiwasi kabisa kuhusu utendaji wa Dr. Magufuli.Mimi tatizo langu kubwa na Lowassa ni kwamba kuna uwezekano mkubwa sana huu mtandao walioujenga toka mwaka 2005 unaotafuna nchi ataweza vipi kupambana nao wakati na yeye ni kati ya watu muhimu waliowezesha mtandao huo? Hivi ni kweli ataweza kupambana na kufuatilia haya madhila na ufisadi unaofanywa na viongozi wetu wakuu wa sasa na watendaji wengine serikalini? Je, ataweza vipi kulinda au kurudisha rasilimali zetu au matunda yake mikononi mwa Watanzania?Suala la pili kwa Lowassa; Kama nlivyotangulia kusema hapo juu kwamba mimi ni mwana-CCM anayekaribia kuondoka kwenye Chama kwasasbabu ya yaliyotokea Dodoma Leo; Je nini msimamo wa Lowassa kuhusu Katiba Mpya kwa Watanzania?WanaJF, najua kuna watu watakasirika na kunitukana sana ktk hili lkn ombi langu kwako ni kwamba kabla hujampinga mtu naomba unipe option/options ya mtu/watu ambao unafikiri wana unafuu pale CCM, ambao hawana doa? na mwenye uwezo wa KIUONGOZI NA KIUTENDAJI kama Lowassa. Hivi ndivyo ninavyoona kwa upande wangu, kwni hata huyo Lowassa hanijui na simjui na hata sina undugu naye isipokuwa nimesukumwa na ukweli ninaouoana kwenye nafsi yangu, kwani hata hao wengine wanaongea wakionyesha wao ni Miungu watu, ni hakika kama JF ingekuwa inaruhusu kuweka mambo machafu waliyoyafanyia Tanzania, ni hakika Watanzania tungefunguka macho. Lkn sitaki kuwa banned, hivyo sitoweza kuweka mambo yao hapa.Pia naomba ieleweke kwamba, kwasasa mimi nahitaji RAIS ambaye ana VISION hata kama ni DICTATOR lkn ana UZALENDO na ana uchungu na Resources zetu; huyo ndiye Rais tunayemuhitaji kwa sasa Tanzania bila kujali anatoka CHAMA GANI, KABILA GANI, KANDA GANI? UWEZO WAKE KIUCHUMI, NA HATA SURA YAKE NI MBAYA AU NZURI. Ipo siku nitawaambia ni kwanini wakati umefika Watanzania tunamuhitaji RAIS kama huyo na si kila mtu anafaa kuwa Rais.Nawasilisha WanaJF.RDI.
   
 2. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #2
  Nov 18, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,112
  Likes Received: 461
  Trophy Points: 180
  Hivi ni lini tutafikiria kizazi kipya. Mbona tunafikiria wazee tu
   
 3. Escobar

  Escobar JF-Expert Member

  #3
  Nov 18, 2011
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 576
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 60
  Mimi binafsi ninamkubali sana LOWASA kwa mantiki ya kwamba ni binadamu na binadamu yeyote anamapungufu yake hivyo anaweza kukosea ama kwa bahati mbaya au kwa kukusudia au akatafasiriwa kuwa ametenda kosa wakati yeye akidhania anatenda jema. Naamini Mh. Lowassa akipewa nafasi nyingine ataitumia vizuri kuonyesha mazuri yake na kuwafanya wengi wafute na kusahau kabisa yaliyopita! Sijawahi kukaa naye karibu huyu jemedari but naamini ipo siku nitaonana naye nitamwambia mabo machache tu kuhusu alivyokuwa ananiinspire tangu enzi zile mpaka leo.
   
 4. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #4
  Nov 18, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Lowassa ni mjanja, anajua kucheza na akili za watu
   
 5. A

  Abdul Mwanji New Member

  #5
  Nov 18, 2011
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu nenda kajipange tena kama umetumwa kumpigia kampeni fisadi Lowasa u waste you time.CCM c wapumbavu kumchagua Lowassa eti awe rais never,CCM ni chama makini sana kinachotaka na kuwa na uwezo mkubwa kwa kuwa na watu makini zaidi wa kutawala Taifa hili.Hili c taifa la kila mtu kuwa rais,ni mtu kmakini pekee ndo CCM chama changu kinaweza kumkabidhi majukumu alonayo Rais Kikwete sasa andeleze jahazi.

  Ungenambia Mh Dr John Pombe Maghufuli walau nangekuelewa au Dr Asha Rose Migiro ningekuelewa fikra zako zimeona watu wenye sifa lakini c fisadi Lowassa.

  Kajipange tena na fikra zako mgando kaka.
   
 6. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #6
  Nov 18, 2011
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Ndugu yangu Abdul;Naomba usome tena maoni yangu. Ni kweli Magufuli na Rose Migiro nimewaona na naendelea kuamini kwamba ni watu wazuri sana kwenye Chama lkn nina wasiwasi na uwezo wao katika upande wa ujasiri na uwezo wao wa KI-UONGOZI. Naamini kabisa kwamba hawa wawili wanaweza wakawa watendaji vizuri serikalini LKN NINA WASIWASI NA UWEZO WAO WA KUWA RAIS WA NCHI. Narudia kauli yangu; kama hili jukwaa lingekuwa linaruhusu kuandika mambo yao hapa, ni hakika hata wewe ungeshangaa na kuamini kwamba kwenye Chama chetu-CCM hakuna mtu safi hata mmoja na ndiyo maana tunajaribu kuangalia ni nani mwenye uwezo wa KI-UONGOZI NA KI-UTENDAJI.Lkn pamoja na hayo yote bado nasisitiza; mimi msimamo wangu ni kwamba kwasasa mimi nahitaji RAIS ambaye ana VISION hata kama ni DICTATOR lkn ana UZALENDO na ana uchungu na Resources zetu; huyo ndiye Rais tunayemuhitaji kwa sasa Tanzania bila kujali anatoka CHAMA GANI, KABILA GANI, KANDA GANI? UWEZO WAKE KIUCHUMI, NA HATA SURA YAKE NI MBAYA AU NZURI. Narudia tena; Ipo siku nitawaambia ni kwanini wakati umefika Watanzania tunamuhitaji RAIS kama huyo na si kila mtu anafaa kuwa Rais.
   
 7. R

  RMA JF-Expert Member

  #7
  Nov 18, 2011
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umetumwa ili umpigie kampeni Lowasa? Ndani ya ccm hakuna aliye msafi!
   
 8. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #8
  Nov 19, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,953
  Likes Received: 1,509
  Trophy Points: 280
  Jamani tumuombee Mwakyembe,halafu ndio tuje kwa hao wasafi(sick) na wanaoweza kutoa maamuzi magumu
   
Loading...