Kwa anaepafahamu Nshamba Muleba

Kwa anaepafahamu Nshamba Muleba

lyajody

Senior Member
Joined
Aug 16, 2024
Posts
158
Reaction score
224
Wakuu habari za muda huu..

Ninaomba kwa mwenye wenyeji wa Katabya Nshamba wilaya ya Muleba anijuze kuhusu maisha kiujumla kwanzia watu wake, uchumi na mazingira
 
Wakuu habari za muda huu..

Ninaomba kwa mwenye wenyeji wa Katabya Nshamba wilaya ya Muleba anijuze kuhusu maisha kiujumla kwanzia watu wake, uchumi na mazingira
Kwani kuna habari gani?
 
Ni moja ya kata kongwe na maarufu katika wilaya ya Muleba, inapakana na kata ya Buganguzi nyumbani kwa Alfred Tibaigana aliyekuwa mkuu wa polisi kanda maalum ya Dar es-salaam pia inapakana kwa karibu sana na makao makuu ya wilaya ya Muleba.
Wenyeji wa huko ni Wanyayangiro( ni mojawapo ya koo katika kabila la wahaya)kwa ujumla ni watu ambao ukijua jinsi ya kuishi nao ni watu poa sana
Ni kata ambayo ina miundombinu yote/ huduma zote za jamii zinapatikana hapo , umeme upo hapo tangu mwaka 1994, kuna nyumba nyingi za kisasa za kuishi za wazawa , wageni na za kupangisha.
Zao kuu la biashara ni kahawa huku ya chakula ni ndizi , mihogo, karanga, viazi, n.k, ardhi yake ni ya rutuba pia kuna hali nzuri ya hewa.
Usafiri wa uhakika wa kwenda, Muleba, Bukoba mjini, kamachumu, Ndolage hospital, Rubya hospital na maeneo mengine ni wa uhakika na upo kwa muda mwingi
Mengine wataongezea Wenyeji wa huko, mi ni mkazi wa eneo jirani. Karibu sana Nshamba
 
Kwa Nilivyosisitizwa na bi mkubwa"Wahaya sio jamii nzuri Sana kuishi Nao wakiwa kwao"nendako utatusimulia ukishakaako(Kwa sauti ya watu wa kanda ya ziwa)🤓🤓🤓🤓
 
Kwa Nilivyosisitizwa na bi mkubwa"Wahaya sio jamii nzuri Sana kuishi Nao wakiwa kwao"nendako utatusimulia ukishakaako(Kwa sauti ya watu wa kanda ya ziwa)🤓🤓🤓🤓
Wee unachukia wahaya nakujua! Walikukosea nini?
 
Wakuu habari za muda huu..

Ninaomba kwa mwenye wenyeji wa Katabya Nshamba wilaya ya Muleba anijuze kuhusu maisha kiujumla kwanzia watu wake, uchumi na mazingira
Huko mm ni kwetu.Ukifika hapo Nshamba mjini mtafute Mkiza Sebastian na Alice au Elias Msona kisha unipm.Ni pazuri sana kuna ndizi na senene.Isalimie familia ya Masilingi,Mathias Mushuti.Kyeju na Katarama.
 
Wakuu habari za muda huu..

Ninaomba kwa mwenye wenyeji wa Katabya Nshamba wilaya ya Muleba anijuze kuhusu maisha kiujumla kwanzia watu wake, uchumi na mazingira
Shikamo mwaalimuu.
 
Wakuu habari za muda huu..

Ninaomba kwa mwenye wenyeji wa Katabya Nshamba wilaya ya Muleba anijuze kuhusu maisha kiujumla kwanzia watu wake, uchumi na mazingira
Nshamba ni huko Muleba unapandisha mlimani hiv upande wa kushoto wa barabara ya kutokea biharamulo kuelekea Bukoba.Kuna onekana kuna baridi muda mwingi.

Nilifika huko 2022.wenyeji niliwaona kama ni watu wenye dharau kupita kiasi hasa kama wewe siyo mhaya.

Nshamba ni ka mji kadogo hiv ila kamechangamka kidogo.wakati huo walikuwa wanajenga barabara nadhani labda sasa itakuwa ni lami.
 
Wakuu habari za muda huu..

Ninaomba kwa mwenye wenyeji wa Katabya Nshamba wilaya ya Muleba anijuze kuhusu maisha kiujumla kwanzia watu wake, uchumi na mazingira
Kama hujui kupiga katerero wala usijisumbue kwenda Muleba. Maisha ya kule ni mwendo wa kumwaga maji kwa kwenda mbele, hakuna kazi nyingine unakula bishoro unarudi kumwaga maji.
 
Back
Top Bottom