tikatika
JF-Expert Member
- May 6, 2011
- 2,330
- 4,124
Nilikua nasikia sikia tu kumbe kweli, leo hii baadhi ya maduka ya vifaa vya umeme yamefungwa kwa kuhofia kukamatwa na vyombo vya ulinzi kwa kosa la kuuza mitumba ya vifaa vya umeme. Katazo hilo limetolewa na uongozi wa mkoa wa Dar. Je ni sahihi.
Serikali ya awamu hii hata sijui wanaendesha nchi kwa kupitia nini maana wakilala wakiamka wanatoa tamko. Hivi sisi watanzania ndio wa kukataza kompyuta mtumba kweli?? Hivi sisi ndio wa kukataza radio mtumba kweli. Kweli et Tanzania hatuhitajia cm mitumba kweli?? Hata hao tunaowaiga sehem vinakotoka hivyo vifaa kuna maduka ya vifaa vilivyowahi kutumika. Sembuse sisi tunaoagiza hata stiki toka china?
Magar tunaagiza mtumba. Nguo tunavaa mtumba. Wao wanaagiza mpaka matren mtumba. Meri mtumba.mfano mv bagamoyo. Ndege mtumba, Mfano bombadia , Ila kumpyuta used hapana. Daaaaaa!! Tv mtumba hapana.
Nasikitika sana kwa usumbufu tunaofanyiwa wafanya biashara awamu hii maana najua litakuja kutenguliwa. Hata huelewi ni lini hela yako itapotea baada ya tamko kutoka kwa viongoz wa kisiasa. Wauza viroba wamepoteza mitaji yao kwa tamko tu!! Tukumbuke hakuna sheria inayokataza vifaa hivyo vya mitumba ukiachana na viroba. Na hata kama hatuhitaji hivyo vitu tulitakiwa kwanza kutunga sheria ya kuvikataza hivyo vitu na kutoa muda wa kumaliza stoke. Ili watu wetu wasiagize tena. Sasa mtu anaamka toka kwake na kusema kuanzia jumatatu hatak kuona vifaa vya umeme mitumba. Kwa vile tu yeye kwa sasa kapata hela za kunua vitu vipya bas anahis kila mmoja anaweza kumudu. Tuko sirious na nchi yetu kweli?? Nina was was na hawa viongoz wetu hawajawahi kufanya hata biashara ya nyanya.
Nimepitisha kontena langu mwezi uliopita bandarini nimelipia mapato. Leo naambiwa nisiuze huu si ukichaa wa madaraka unaotumika kutuumiza sisi wafanya biashara??? Kiukweli tuna safari ndefu sana watanzania kwa uongoz huu unaotuongoza kutufikisha nchi ya ahadi.