Katika Jamii ya Kidemokrasia, uwazi na uhuru wa Vyombo vya Habari ni nguzo muhimu za uwajibikaji. Hata hivyo, pale ambapo Tume ya Uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Inapoamua kuzuia Vyombo vya Habari kushuhudia ushuhuda wa waathirika wa matukio ya wakati na baada ya uchaguzi, maswali mazito huibuka: Je, hatua hiyo inalenga kulinda waathirika na mchakato wa uchunguzi, au ni njia ya kuficha ukweli usionekane hadharani?
Makala hii inakusanya mitazamo kutoka kwa wananchi, mtaalamu wa habari (mtangazaji), na wachambuzi wa masuala ya siasa, ili kutafakari kwa kina maana ya uamuzi huo kwa mustakabali wa uwazi, haki na demokrasia.
Wananchi wengi hawa wa kizazi cha sasa, hawa wanatumia Mitandao (netizens) wanaamini kuwa vyombo vya habari ni sauti yao. Kwao, kufungwa kwa milango ya habari wakati wa ushuhuda wa waathirika kunawanyima fursa ya kujua kilichotokea na kutathmini haki inatendeka vipi.
“Kama hakuna kinachofichwa, kwa nini vyombo vya habari vizuiwe? Tunahitaji kuona na kusikia ukweli ili tuamini kuwa haki inatendeka,” anasema mwananchi (jina linahifadhiwa kwa sababu maalum).
Hata hivyo, wengine wanatambua umuhimu wa kulinda waathirika, hasa pale ushuhuda unapohusisha mateso, vitisho, au unyanyasaji wa kijinsia. Kwa mtazamo huu, faragha inaweza kuwa kinga muhimu dhidi ya kuumizwa kisaikolojia au kisiasa.
Kwa mujibu wa Felix Mwakembe Mwandishi Mkongwe wa Habari, anasema kazi ya vyombo vya habari si kusisimua hadhira, bali kutoa taarifa sahihi kwa maslahi ya umma.
Anasisitiza kuwa: Uwazi huongeza imani ya umma katika tume za uchunguzi. Kuzuia habari hujenga pengo la taarifa linaloweza kujazwa na uvumi.
Hata hivyo, kuna mazingira maalum yanayohitaji mipaka ya kimaadili, hususan kulinda usalama na utu wa waathirika.
“Suluhisho si kufunga kabisa vyombo vya habari, bali kuweka utaratibu wa kuripoti kwa kuzingatia maadili—kama kuficha sura/majina ya waathirika au kutoa muhtasari wa ushuhuda kwa umma,” anashauri mtangazaji huyo.
Mtaalamu WA Habari
Wachambuzi wa siasa wanaona suala hili likigusa mizani ya nguvu kati ya dola, tume za uchunguzi, na umma. Wanasema:
Katika mazingira ya uchaguzi, taarifa huwa nyeti kisiasa; kuzuia vyombo vya habari kunaweza kutafsiriwa kama udhibiti wa simulizi
Ikiwa hakuna vigezo wazi vya kisheria vinavyoeleza sababu za kuzuia habari, hatua hiyo inaweza kuonekana kama kutoroka uwajibikaji.
Lakini pia, nchi nyingi hutumia vikao vya faragha kulinda mashahidi—mradi taarifa za jumla zitolewe kwa umma baadaye.
Kwa mfano, wachambuzi hutaja kuwa katika mifumo ya kidemokrasia iliyoimarika kama Uingereza na Afrika Kusini, tume za uchunguzi huweka mizani kati ya uwazi wa umma na usalama wa mashahidi, kwa kutoa ripoti za kina kwa umma hata kama baadhi ya ushuhuda hufanyika kwa faragha.
Lakini pia amesema inawezakana kufichwa kwa mashaidi ni kuzuia kutonesha vidonda na ukizingatia kunamchakato WA maridhiano.
MCHAMBUZI
Hitimisho
Kuzuia Vyombo vya Habari kushuhudia ushuhuda wa waathirika wakati na baada ya uchaguzi kunaweza kuwa hatua ya ulinzi, lakini pia kunaweza kutafsiriwa kama kukwepa ukweli kuonekana hadharani iwapo hakutakuwa na uwazi wa kutosha kwa umma.
Suluhisho la kudumu ni kuweka mizani: Kulinda utu na usalama wa waathirika, huku haki na ukweli vikionekana kutendeka mbele ya macho ya jamii.