Kuzuia Bunge live ni moja ya sababu ya mimi kutoupenda utawala wa Magufuli

Salary Slip

Platinum Member
Apr 3, 2012
49,323
152,131
Kukatisha matangazo ya Bunge baada ya kipindi cha maswali na majibu ni jambo linalokera na kuumiza sana na hili ni moja ya mambo yanayonifanye nisifurahiahwe kabisa na huu utawala wa sasa.

Kitendo hiki mimi nakiona ni kama ukatili kwa wanaopenda kufuatilia shughuli za Bunge na kwakweli hakina justification yoyote.

Alafu kama mmeamua kuzuia Bunge kive,kuna haja gani ya kutuonyesha kipindi cha maswali na majibu alafu baadae mnakata matangazo kipindi cha maswali na majibu kinapoisha?Hamuoni huku ni kutuuongezea hasira tu?

Hivi ni lini na wapi mlifanya utafiti mkagundua kuwa watanzania wengi wanapenda zaidi kutazama kipindi cha maswali na majibu kuliko vipindi vingine vya Bunge?

Kuzuia Bunge live ni moja ya sababu kuwa ya CCM kupoteza kura nyingi mwaka 2020 hata kama mtakuja kurudisha huu utaratibu mwaka mmoja au miwilo kabla ya uchaguzi.

Wapinzani,swala kurudisha utaratibu wa Bunge live liwe ni moja ya agenda /ahadi yenu mwaka wa 2020.
 
Ni bora uuchukie utawala kuliko kuliko kuangalia upuuzi wa baadhi ya wawakilishi wasiojiheshimu na kutambua dhamana waliopewa na wananchi waliowachagua
 
Upuuzi UPI?bunge lolote duniani Lina challenges....unashangaa matusi?Mara ngapi mabunge mfano Kenya,Nigeria wamepigana mpaka kutoana damu lakini mpaka sasa watu wao wanatazama bunge live
 
sasa kwakuwa hao kenya na nigeria wanafanya utoto na ujinga bungeni nasi ndio tuige? maadili yetu, utamaduni wetu ni tofauti ns hao, kwetu sisi mtu mzima hatukani mbele ya mtoto sasa wabunge wetu wanatukana bila kujali kwamba watoto wanaona na hata kuiga wanachokitazama. ni vema wabunge wajitathmini mienendo yao bungeni kabla sijaunga mkono bunge kurejeshwa live.na kama wabunge wetu wataendelea kubehave hovyo kama sasa ni bora bunge lisionyeshwe kabisa .ni mtazamo tu.
 
Ndg bila challenges usitegemee maendeleo!q
Basi bora turudi chama kimoja tu maana bila demokrasia vipi mtasonga mbele?
 
Kukatisha matangazo ya Bunge baada ya kipindi cha maswali na majibu ni jambo linalokera na kuumiza sana na hili ni moja ya mambo yanayonifanye nisifurahiahwe kabisa na huu utawala wa sasa.

Kitendo hiki mimi nakiona ni kama ukatili kwa wanaopenda kufuatilia shughuli za Bunge na kwakweli hakina justification yoyote.

Alafu kama mmeamua kuzuia Bunge kive,kuna haja gani ya kutuonyesha kipindi cha maswali na majibu alafu baadae mnakata matangazo kipindi cha maswali na majibu kinapoisha?Hamuoni huku ni kutuuongezea hasira tu?

Hivi ni lini na wapi mlifanya utafiti mkagundua kuwa watanzania wengi wanapenda zaidi kutazama kipindi cha maswali na majibu kuliko vipindi vingine vya Bunge?

Kuzuia Bunge live ni moja ya sababu kuwa ya CCM kupoteza kura nyingi mwaka 2020 hata kama mtakuja kurudisha huu utaratibu mwaka mmoja au miwilo kabla ya uchaguzi.

Wapinzani,swala kurudisha utaratibu wa Bunge live liwe ni moja ya agenda /ahadi yenu mwaka wa 2020.

Raisi wetu hahitaji upendo wako, baki nao tu au ugawie kwingine kama ukipenda!
 
Ni bora uuchukie utawala kuliko kuliko kuangalia upuuzi wa baadhi ya wawakilishi wasiojiheshimu na kutambua dhamana waliopewa na wananchi waliowachagua
Siku nataka zinyukwe ngumi ndani ya bunge ili heshima irudi kudadeki , tunawaomba polisi msiingilie .

Maendeleo hayaletwi kilelemama , ni muhimu watu kuheshimiana .
 
Bunge gani la kuangalia huku kidole kikiwa kwenye "mute" button ya remote. Hawa akina Lusinde,Lissu na Mdee hawafainkabisa ni bora bunge mubashara likafutwa kabisa.
 
Endelea kuuchukia utawala tu kuliko kutuonyesha upuuzi wa hao kondoo wa magwanda, kurpoka na matusi, kushadadia ujinga pasi nakujua kama huku wananchi tunanufaikaje na huo upuuzi wao
 
Back
Top Bottom